Ndugai kusimamia udhalilishwaji wa Mbunge Viti Maalum CHADEMA ndani ya Bunge ni fedheha na aibu kwa Taifa

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
18,511
68,141
Salaam,

Nimeona video muda mfupi uliopita ambapo Mh. Spika Job Ndugai jana aliamua bila aibu yoyote kusimamia udhalilishwaji kwa Mbunge wa Viti Maalum Chadema Mh. Yosepher Komba aliofanyiwa na Mbunge Viti Maalum CCM, Jackline Msongozi.

Huyu Mbunge wa CCM ki umri ni sawa na mzazi kwa Mbunge wa Chadema, lakini kuamua kuzungumza aliyozungumza kuhusu tuhuma za ngono kwamba Mbunge wa Chadema nae alimlalamikia kufanyiwa, na Spika kwa nafasi yake kuacha hilo jambo litokee bungeni ni udhalilishaji mkubwa waliomfanyia Mbunge wa Chadema, iwe ni kweli wabunge hao wawili waliongea pembeni au sio kweli.

Ieleweke wazi, hili suala bado linafanyiwa uchunguzi kwenye vyombo vya usalama, sasa kwanini Mh. Spika kwa nafasi yake aache lijadiliwe bungeni? haoni huku ni kuingilia mamlaka za kiuchunguzi zinazoendelea juu ya jambo hilo?

Binafsi nashindwa kuelewa, kwanini Spika wa Bunge letu kaamua kusimamia bunge kwa kuonesha ushabiki wa kiwango cha juu namna hiyo? kufanya bunge letu la JMT kugeuka kijiwe cha umbeya na mipasho, huku akimzuia Mbunge mwanaume wa CDM alietaka kuingilia kati suala hilo kwa kumwambia mambo ya wanawake asiingilie, yaani hapa Ndugai anaona raha kusimamia mipasho inayoendelea bungeni chini ya uongozi wake kwasababu tu inazungumzwa na Mbunge wa chama chake?

Kwanini ameamua bila aibu kulinajisi bunge letu kwa kiwango hiki? Spika amefikia kiwango cha kusimamia udhalilisha wa utu ili tu kukilinda chama chake? Spika anasimamia uonevu ili tu kujifurahisha yeye binafsi na baadhi ya wabunge wa chama chake wanaopenda kuona mambo ya kijinga kama yale!

Baada ya kumfanyia uonevu huo, anawaita askari wamtoe Mbunge wa CDM nje kwa kisingizio alileta vurugu wakati akijaribu kujitetea, halafu askari wanafika na kumtoa nje tena kwa kumsukuma!.

Aibu hii kama taifa hakika itatuaibisha kwa kipindi chote ambacho Spika Ndugai ataendelea kuwa Spika wa bunge letu.

hqdefault.jpg
 
Matokeo ya zile elimu za kupeana, madaraka ya kupeana, uspika wa kupeana ndio hayo.

Wao ccm hawaogopi chocho siku hizi

Watapewa ushindi na ubunge kupitia mabavu

Kura au wananchi hawana nafasi

Ndio maana
1. Watu wanajiundia sheria kujilinda

2. Mijadala inageuzwa mipasho

3. Mambo ya msingi yanafunikwa kwa kujadili upumbavu

Kama taifa tumepotezwa na elimu ya ujinga imetupoteza kabisaa. Aibu sana.
 
Kwani Joyce Mukya ni mbunge viti maalumu? Alikuwa na sifa za kuupata? Isije ikawa nae anavumilia tu sababu za shida.
 
Wangekataa kwanza kudhalilishwa na wale wanaowataka kimapenzi haya mengine yasingetokea.
Ukitaka kukataa udhalilishwaji basi anzia ndani kwako, unalalamika udhalilishwaji nje ya nyumba yako wakati ndani udhalilishwaji umeshamiri kwelikweli.... huu si upunguani
 
Huyu Mbunge wa CCM ki umri ni sawa na mzazi kwa Mbunge wa Chadema, lakini kuamua kuzungumza aliyozungumza kuhusu tuhuma za ngono kwamba Mbunge wa Chadema nae alimlalamikia kufanyiwa, na Spika kwa nafasi yake kuacha hilo jambo litokee bungeni ni udhalilishaji mkubwa waliomfanyia Mbunge wa Chadema, iwe ni kweli wabunge hao wawili waliongea pembeni au sio kweli
Acha kujiliza wewe,udhalilishwaji kafanyiwa mbunge wa chadema na viongozi wake,unatakiwa umshauri mbunge wako apaze sauti badala ya kulia lia na kuomba huruma
 
Jana nimeumia Sana kwa kile nilichokiona kwenye bunge letu hata Kama Ni kweli yule mbunge wa viti maalum alisema kwamba amenyanyaswa kingono haikua sawa kumuanika bungeni

Fikiria Ni wazazi wake, watoto ndugu na jamaa , viongozi wake wa dini , wazee wake mtaani ndio walikua wanaangalia hiyo taarifa walijisikiaje?!Ni aibu gani aliomsababishia?

Mambo mengine haitakiwi tuyafanye kisiasa bali tutumie akili tulizopewa na Mungu
Kwa nini spika asimamie huo udhalilishaji?

Vipi huyo anaedhalilishwa angekua ni mwanae?

Kwani bunge haliwezi kuendeshwa bila kuwajadili wapinzani kila siku?

Ndio tulichowatuma wakakifanye bungeni?

Haya mambo yanaudhi Sana Ni Bora zile tawala zetu za jadi zingeendelea kuwepo.
 
Jana nimeumia Sana kwa kile nilichokiona kwenye bunge letu hata Kama Ni kweli yule mbunge wa viti maalum alisema kwamba amenyanyaswa kingono haikua sawa kumuanika bungeni
Fikiria Ni wazazi wake, watoto ndugu na jamaa , viongozi wake wa dini , wazee wake mtaani ndio walikua wanaangalia hiyo taarifa walijisikiaje?!Ni aibu gani aliomsababishia? Mambo mengine haitakiwi tuyafanye kisiasa bali tutumie akili tulizopewa na Mungu
Kwa nini spika asimamie huo udhalilishaji? Vipi huyo anaedhalilishwa angekua ni mwanae?
Kwani bunge haliwezi kuendeshwa bila kuwajadili wapinzani kila siku?
Ndio tulichowatuma wakakifanye bungeni?
Haya mambo yanaudhi Sana Ni Bora zile tawala zetu za jadi zingeendelea kuwepo.
Sasa kama anadhalilishwa kingono kwa nn asiambiwe mkuu, nyie ndio mnakuza mambo kama aya.
 
Back
Top Bottom