Ndugai awagawa wabunge CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndugai awagawa wabunge CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 23, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  NA MASHAKA MGETA

  22nd July 2012

  [​IMG]
  Naibu Spika, Job Ndugai


  Hatua ya Naibu Spika, Job Ndugai, kukataa ombi la Mnadhimu Mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu, kuwasilisha hoja ya kutaka ajali ya MV Skagit, imekosolewa na kuwagawa wabunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).


  Ndugai akiongoza kikao cha Bunge juzi Ijumaa, alimzuia Lissu kuwasilisha hoja ya kutaka kusitishwa hoja ya hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Chakula, Kilimo na ushirika, ili kufanyike mjadala kuhusu ajali hiyo.

  Naibu Spika huyo, alisema ingawa hoja ya Lissu ilikuwa nzito, lakini haikutolewa kwa mujibu wa kanuni za Bunge.


  Hata hivyo, Lissu alitoa taarifa akitetea kwamba alifuata utaratibu kwa mujibu wa ibara ya kanuni ya 47 (3), ili apewe idhini na kiti cha Spika, ndipo atoe hoja.


  Lakini Ndugai alisimamia katika uelewa na tafsiri yake kuwa Lissu alipaswa kuzungumza baada ya kusimama kama ishara ya kutoa hoja, ili iungwe mkono na wabunge wengine, lakini haikuwa hivyo.


  Baadhi ya wabunge kupitia CCM wameliambia NIPASHE Jumapili kuwa, hatua ya Ndugai kuzuia hoja ya Lissu kwa kile kinachofananishwa ‘ubabe wa kisiasa', inakitia doa Chama Cha Mapinduzi.


  Hata hivyo, wabunge wengi hawataki kutajwa majina yao kwa kile wanachosema kuepuka kuandamwa, kama ilivyotokea kwa Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe.


  Filikunjombe aliyeunga mkono hoja ya ajali ya MV Skagit kujadiliwa bungeni, alifuatwa na baadhi ya mawaziri na kuulizwa kwa nini alifikia hatua hiyo huku akijua hoja iliyotolewa ilitoka kwa wapinzani.


  Mbunge huyo kijana mwenye misimamo ya kuunga hoja zenye maslahi ya umma pasipo kuathiriwa na itikadi za vyama, alisema ajali ya MV Skagit iliwaathiri Watanzania bila kujali tofauti za itikadi zao.


  Mbunge wa Nzega (CCM), Hamis Kingwangalla, aliiambia NIPASHE Jumapili kuwa ingawa Ndugai alitumia mamlaka ya Unaibu Spika, lakini alipaswa kutumia busara zaidi kuhusu hoja ya Lissu.


  "Hawa jamaa (upinzani) hawakutaka kuahirishwa kikao ama mkutano wa bunge, bali kujadili hoja ya ajali ya MV Skagit, kwa mtazamo wangu nadhani angekubali hata kwa nusu saa, isingetuathiri," alisema.


  Mbunge mwingine ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema kukataa kuijadili hoja iliyohusu maisha ya watu, iliifanya CCM ionekane haipo kwa ajili ya wananchi wanyonge.


  "Waliokufa si wageni wale, ni raia wa Tanzania sasa kuikataa hoja ile, tena kwa lugha ya mabavu ikichochewa na kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, haitoi taswira nzuri ya chama mbele ya umma," alisema.


  Hata hivyo, Mbunge mmoja kutoka jimbo moja la mkoani Kagera ambaye hakutaka pia jina lake litajwe gazetini, alisema hapakuwa na haja ya kuijadili ajali hiyo kwa vile mamlaka nyingine zilikuwa zinaendelea kuifanyia kazi.


  "Binafsi sijaona tatizo la Ndugai kuikataa hoja ya Lissu hata kama ingefuata kanuni, kwa maana tayari kuna mamlaka nyingine zinalifanyia kazi, hatuwezi kuwa taifa ambalo yakitokea majanga nchi nzima inaelekea huko," alisema.


  Mbunge huyo alisema, ndio maana licha ya kutokea ajali hiyo, taasisi nyingine kama mashule, majeshi, wizara za serikali na nyinginezo hazikufungwa, bali zilishiriki uzalishaji na utoaji huduma.


  Kusitishwa kwa Lissu kutoa hoja hiyo, kulisababisha baadhi ya wabunge wa upinzani kutoka nje, kwa madai kuwa Bunge ‘linaburuzwa' na serikali katika kuwajibika kwa umma.
  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI


   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  kwanini Speaker na Naibu Speaker wanatuharibia Demokrasia? Hivyo Sio Vyeo Vya Milele
   
 3. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,785
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Huyo mbunge toka Mkoa wa Kagera kama siyo Blandes basi ni Rweikiza!
   
 4. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hivi ulifanyika utaratibu gani wa kumpata huyu Naibu speaker kama Ndungai????

  Anayefahamu anijuze jamani maana Mi naona imekosewa kwa 95% jamani!
   
 5. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Vimbwanga hivi vya,
  kugeuza hoja za wabunge wa upinzani,
  kuwa ujinga na mzaha,
  vimekuwa vikifanyika miaka yote,
  katika level ya vijiji kata tarafa na wilaya,
  kwa wananchi bila woga.

  Huko vijijini,
  wananchi wamekuwa wakitukanwa,
  na viongozi kwamba hawajui sheria,
  wanataka sifa, ni wabishi,
  hawaelewi taratibu na kawaida,
  haana logic na dharau nyingi.

  Ukiona mtu mjinga mbumbu wa sheria,
  Kama Lukuvi anajifanya kujua,
  na hata kutoa dharau kubwa,
  dhidi ya watu waijuao fani ya sheria,
  Jiuliza Lukuvi hujifaragua kiasi gani,
  awapo Isimani,
  Mbele ya wanyalu wa kawaida wasio na shule???

  kutokana na mbinu nyingu chafu,
  za chama cha mapinduzi,
  kulegea vikazio vyake na kushindwa kabisa,
  CCM wameamua kutumia mbinu,
  za kutoa matusi hadharani dakika moja,
  huku wakisikika na Watanzania wote,
  kisha dakika mbili baadaye,
  kuruka kimanga na kusema,
  hawakusema hivyo au,
  hawakumaanisha hivyo.

  Weremani lazma awe ana funza kichwani,
  akili yake imekaa tenge,
  alisikika akitoa lugha ya mtusi,
  kwa Lissu kwamba si kila mwenye nywele kichwani,
  ana weza kufikiri,
  pia kusema kwamba Tundu Lissu hana nidhamu,
  eti meza yake kaivunja kwa sababu hiyo?

  Hakukuwa na ulazima wa Werema,
  aliye mwanasheria mkuu wa serikali ya CCM,
  kutoa matusi kisha kushindwa,
  kutoa ufafanuzi wa hoja.

  Hii wenzetu kwa kimombo wanaita "Character assasination"
  Unashindwa kujibu hoja iliyopo mezani,
  unaanza kushambulia,
  mavazi ya mtoa hoja,
  nywele za mtoa hoja,
  viatu vya mtoa hoja,
  sura ya mtoa hoja,
  hata dawati akaliao mtoa hoja.

  MR Werema even your 3years old child would have done good job.

  Wereama alitumia muda mwingi,
  nguvu nyingi sana na hata,
  akili zake zote na za kuazima,
  kutoa lugha ya matusi.

  Mimi hujiuliza maswali,
  iwapo wenzetu hawa wa CCM,
  wanaongea matusi makubwa kiasi hiki,
  mbele ya Camera za TV,
  zinazo rusha matangazo Tanania nzima?????

  Sasa wakijifungia kwenye mikutano yao ya siri,
  ya kujadili mbinu chafu za CCM au,
  ya kuwaweka sawa akina,
  Ndugulile, Filikunjombe na wengine,
  Ni matusi makubwa kiasi gani,
  hutolewa huko vikaoni humo?

  Huenda kila baada ya maneno mawili ya maana,
  hufuata neno la;
  Ucchi wa mama yako,
  Makalio ya mama yako,
  Sehemu za siri za baba yako,
  Vitendo vyote vya kwenye madangulo,
  Tendo la kufanywa kinyume na maumbile,
  na matusi mengine mengi ambayo,
  akina Werema huyavumbua vikaoni.


  Bunge la JMT limekosa adabu,
  Bunge limekosa heshima,
  Bunge hili hakika linapigwa nyuma,
  Bunge limejaa wahuni na wavuta bangi,
  Bunge limeshindwa kuwajibika kwa wananchi,
  Bunge linang'ooka meno kila siku,
  Bunge la wazembe,wehu majuha na pashikuna,
  Bunge la kudumisha wizi, ubadhirifu, ufisadi na ukoloni mambo leo.
  Bunge Sifuri, Zero,Nunge, Oo.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,882
  Likes Received: 83,364
  Trophy Points: 280
  Mafisadi ndani ya magamba walikaa chini na kuangalia ni nani ambaye atakayeweza kulinda maslahi yao ndani ya Bunge, Makinda na Ndugai ndio wakaonekana ni bora kuliko yoyote yule na kama tujuavyo kila walitakalo mafisadi ndani ya magamba basi ni lazima litekelezwe hawana mpinzani.   
 7. babuwaloliondo

  babuwaloliondo JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  WAbunge wa ccm ni wanafiki, si waamini wanaongea tu, hawana confidence waganga njaa wakubwa
   
 8. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  "Filikunjombe aliyeunga mkono hoja ya ajali ya MV Skagit kujadiliwa bungeni, alifuatwa na baadhi ya mawaziri na kuulizwa kwa nini alifikia hatua hiyo huku akijua hoja iliyotolewa ilitoka kwa wapinzani".Hiki kipande nimekisoma nikashtuka sana na kujiuliza maswali mengi sana.Ina maana kuna siku mbunge wa upinzani anaweza kuwapa tahadhari juu ya kuwepo bomu bungeni wakapuuzia kisa suala limetolewa na upinzani, wa upinzani wakatoka nje yenyewe yakabaki ndani na kulipukiwa na bomu yakisubiri hoja iletwe na magamba.Naomba niseme hii mjitu ni MIJINGA SANA.
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  lukuvi anapaswa kukaa kimya maana ni waziri aliyepata cheo kwa kujikomba komba kwa wakubwa...hana lolote kichwani mwake..ana shule nyembamba sana na isiyo na mpangilio..
  ni mara mia awe anakaa kimya tu
   
Loading...