Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Hii tabia ya Ndugai kumsemea Magufuli kwa watu anaokuwa na bifu nao inakera sana. Mtu yeyote mwenye akili anaelewa wazi hii ni saikoloji Ndugai anatumia kuchochea moto kati ya Magufuli na watu ambao Ndugai ana tatizo nao, hasa baada ya kumjua Magufuli ana silka ya namna gani.
Ndugai anajipendekeza kwa Magufuli kitoto sana, huwezi kuamini mwanaume mwenye cheo cha heshima namna ile anaweza kufanya anayofanya.
Mfano ni pale alipokuwa na issue na CAG aliyepita Prof. Assad ambapo kila wakati alitoa matamko ya kumsema GAG dhidi ya raisi katika namna ya kumpandisha mori Magufuli dhidi ya Prof. Assad. Pia amefanya hivyo dhidi ya watu fulani ndani ya CCM ambao hapatani nao.
Na sasa yuko kwa Mbowe, yale yale ya wewe Mbowe raisi akishatamka usijifanye una mamlaka zaidi ya raisi, usijipime ubavu na raisi, nk. Toka lini Spika umekuwa msemaji au mteteaji rasmi wa raisi? Wenye akili tunajua Ndugai anachofanya hapa - kwamba hii ni saikoloji ya mtu dhaifu kumgonganisha mtu aliye na ugomvi naye dhidi ya mtu mwenye nguvu zaidi kwa faida yake mwenyewe.
Ndugai kama una tatizo na watu kabiliana nao bila ya kujifanya wewe unajua sana kumsemea na kumtetetea raisi dhidi yao. Siyo kazi ya Spika kumsemea na kumtetea raisi. Kazi zako za kuwa Spika wa Bunge zinakushinda sasa unaingilia madaraka yasiyo yako. Kama Mbowe kama mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani anakiuka utaratibu wa protokali dhidi ya kauli za Raisi wapo wanaostahili kushughulikia hilo, sio Spika.
Na kumbuka kwamba Mbowe kama mwenyekiti wa chama cha siasa kama alivyo Magufuli, ana wigo unaomruhusu kukosoa hadharani kauli za raisi - ndio maana ya siasa za upinzani ambazo wewe Ndugai unaonekana huzifahamu sawasawa.
Na tafadhali, tumia lugha ya kistaarabu unapoongelea viongozi ukiwa kama spika. Kuna maneno ambayo yanakuonyesha kuwa huna staha na unayatamka ukiwa na mavazi ya uspika. Inatia aibu. Kwa mfano, suala la mbunge fulani kuwa mtu wa ovyo, au hatarudi bungeni, ni fedhaha sana Spika kufikia kiwango cha chini kiasi hicho katika heshima ya kiti cha Spika. Ukisema mbunge fulani ni wa ovyo unatukana hata waliomchagua. Sasa spika huna uwezo wa kuona hilo?
Ulisamehewa kwa kumpiga mtu wa chama chako fimbo kichwani hadi akazimia kwa sababu tu za ushindani wa kisiasa. Ule ulikuwa ni utovu mkubwa na nidhamu kuliko wowote ambao Mbowe amewahi kuonyesha kwa raisi. Sasa jaribu kujiendesha kwa namna ambayo itawaonyesha wale waliokupa second chance kwamba hawakukosea.
Hata kama viongozi au wabunge wanakosea, wawe upinzani au chama chako, kuna namna ya nidhamu ya uspika inayotakiwa katika kushughulikia mambo kama hayo badala ya wewe kutumia nafasi hizo kujipendekeza kwa Magufuli. Hii ni pamoja na kutowasema kama watoto wadogo - mfano eti wanatangaza ugonjwa wa wabunge wanaokufa. Acha kuongozwa na hisia (emotions) unapokalia kiti cha spika.