binafsi mimi sizipendi ndoto za kutembea huku ukiwa hujitambui!
sizipendi na sipendi kuona mtu yeyote akiwa na tatizo kama hilo..
aisee nilikuwa na rafiki yangu, dada flani hivi wa kichaga, alikuwa na ndoto za kuamka na kuanza kutembea kabisa! anafungua mlango na kutoka nje huku akiwa hajelewi.. si unajua yuko ndotoni!
basi bana, siku hiyo kaamka saa sita za usiku, akiwa ndotoni, room lake lilikuwa floor ya pili juu!
basi nawaambieni, katoka chumbani kavamia balcon juu nyuma ya chumba kaanza kushuka bila kutumia njia sahihi...
nawaambieni kilichotokea hapo ni kudondoka kama gunia la mkaa.. dada wa watu mpaka leo ana ulemavu kwenye mapaja yake..!
sizipendi ndoto za hivyo mimi! japo wengine wanasema sijui unaoteshwa madawa.. lakini nyingine zina madhara makubwa