Ndoto zilizogeuka kuwa kweli

Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,863
2,000
NDOTO KUTOKA MTAA WA KIUNGANI GEREZANI 1957

Ali umenirudisha nyuma mbali sana katika maisha ya utoto wangu.

Nilikuwa nakaa Manhattan jirani na Hudson River New York.

Mwenyeji wangu akaniambia kuwa tukitoka hapo nje tu tukavuka mto tutafika nyumbani kwa Harry Belafonte.

Bahati mbaya yeye hafahamianinae kwa hiyo hakuweza kunipeleka.

Bibi yangu Zena bint Farijallah aliiona movie ya Harry Belafonte, "Island in the Sun," katika miaka ya 1950 na kila ikipatikana nafasi atanihadithia senema ile.

Kitu alichokipenda bibi yangu katika senema ile ni msichana wa Kizungu kumpenda Belafonte mtu mweusi.

1957 nina miaka 5 tunaishi Mtaa wa Kiungani, Gerezani nasikia radio ikipiga, "Round the Bay of Mexico," nyimbo ya Harry Belafonte na mimi nikijitahidi kuimba.

Natazama picha katika gazeti la Drum kutoka Johannesburg linachukua fikra zangu kwa zile suti walizovaa watu mle.

Niko katika ndoto.

Sikujua kuwa ipo siku nitakutana na mwenye gazeti hili la Drum Jim Bailey Dar es Salaam mimi nikiwa kijana na tutafanya kazi pamoja ya kuchapa kitabu kutoka Drum mimi nikiwa mhariri wake.

Ally Sykes ndiye aliyenikutanisha na Jim Bailey.

Wala haikunipitikia kuwa iko siku nitafika Johannesburg na nitatembea kwenye mitaa yake na kusikiliza South African Jazz ya kina Sipho na Hugh Masekela.

Hizi zote zilikuwa ndoto zangu utotoni wala haikunipitikia kuwa hizi ndoto siku moja zitakuwa kweli.

Nilikuwa kwenye ndege nakwenda Mbabane Swaziland safari yangu ya kwanza na nikimaliza shughuli zangu baada ya kiasi cha mwezi nitakwenda Johannesburg nikamuone Jim Bailey.

Nimekaa na Mzungu Muafrika Kusini katika mazungumzo nikamfahamisha kuwa nitakwenda Johannesburg akaniuliza kinachonipeleka nikamwambia matembezi na kumuona rafiki yangu Jim Bailey.

Akashangaa sana akataka kujua nimejuana vipi na Jim Bailey.

Akanipa pole akaniambia, "Jim Bailey alikuwa jirani yangu tumemzika mwezi uliopita."

Jim Bailey ndiye aliyenipatia picha za Julius Nyerere na Sheikh Suleiman Takadir na picha ya Julius Nyerere na Mama Sakina, Bi. Titi Mohamed na Tatu bint Mzee wako uwanja wa ndege wanamsindikiza Nyerere safari ya kwanza UNO February, 1955.

Ali Boxer ahsante sana.

Ali Boxer ahsante sana.
Screenshot_20200909-173906.jpg
20200909_165921.jpg
 

Zawadini

JF-Expert Member
Feb 2, 2012
1,498
2,000
Mkuu Mohamed;
Hii lugha kwa mara ya kwanza naiona ngumu! Sijafahamu! Lakini ni kosa langu mwenyewe na wala sio lako wewe.
 

julaibibi

JF-Expert Member
Jun 16, 2020
956
1,000
Shehe twaomba na habari za daimond jubilee
twasikia sisi vijana wa sasa ya kuwa eti alipimwa aga khan na almas kwenye mizan ndio ikawa kiswat cha kuitwa diamond jubilee?
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
56,863
2,000
Shehe twaomba na habari za daimond jubilee
twasikia sisi vijana wa sasa ya kuwa eti alipimwa aga khan na almas kwenye mizan ndio ikawa kiswat cha kuitwa diamond jubilee?
Diamond Jubilee ni maadhimisho ya miaka 60 ya tukio muhimu, kama vile kuanzishwa kwa taasisi, miaka ya mfalme/ kiongozi wa dini kuwa mtawala/ kiongozi kufikia 60, au hata ndoa kufikisha miaka 60.

Pia kuna Golden Jubilee (miaka 50) Silver Jubilee (miaka 25) nk.

Hilo hall inaonekana lilijengwa katika maadhimisho ya miaka 60 ya uongozi wa Aga Khan kama sijakosea.
 
  • Thanks
Reactions: T11

Gagnija

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
8,850
2,000
NDOTO KUTOKA MTAA WA KIUNGANI GEREZANI 19571957 nina miaka 5 tunaishi Mtaa wa Kiungani, Gerezani nasikia radio ikipiga, "Round the Bay of Mexico," nyimbo ya Harry Belafonte na mimi nikijitahidi kuimba.
Kiswahili safi ni "nyimbo ya...", au "Wimbo wa...!"
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom