Yegomasika
JF-Expert Member
- Mar 21, 2009
- 13,164
- 61,249
I know what you are talking about Brother, I relate your story to my story, and I'm living the American dream. Niceeeee!.Hio story ya huyo nesi mimi pia naona ni kama hadisi tu za Abunwasi au ana matatizo kibao aliyopata hapo mbeleni na sasa inabidi alipe madeni ya kale. Kazi ya Nesi inalipa kishenzi mtu asikwambie aisee! Hao watu wanachukua kuanzia dala 30 hadi arobaini kwa saa. Sasa hebu piga hayo mahesabu kama anafanya 16hrs kwa siku baada ya taxes how much is she bringing home?Mimi nasema hivi maana mke wangu ni nesi na pia anafundisha manesi University na hela yake najua.
Sasa hebu nami nitumbukize hamsini yangu kwa wale wanaokandia maisha ya ughaibuni na kuyalinganisha na ya Bongo. Jamani hii nchi maisha ukiyapatia mambo yako yanakwenda mswano kinoma! Tatizo la wengi wetu ni kua tukitoka nyumbani tuna hadisi kibao za kudanganya watu what we are going to do in the States thereby setting our expectations to be way too high. Kisha mtu akifika huku na akipigwa na hali halisi anachanganyikiwa na kukosa mwelekeo. Mie najua watu wengi sana niliokuja nao mwaka wa 1999 ambao walikua wakiwaambia washkaji kijiweni eti wanakuja kusomea mara sijui urubani, mara udaktari mara sijui u-lawyer. Mwenzenu mimi nikawa nasema nitaangalia kama digrii yangu ya ualimu itafua dafu na sikua na mengi ya kujisifia. Kama kutakua kubaya nitarudi home maana sijaua mtu wala sikufukuzwa.
Basi nilipojimiksi huku jambo la kwanza nikachangamkia shule na kupata the basics (ID na SSN) baadae nikawatumia jamaa wa EEC digrii yangu waifanyie evaluation kisha waniambie nikowapi kulingana na standards zao. Majibu yaliporudi wakaniambia kila kitu safi naeza kuapply leseni ya kufundisha. Kipindi hicho mwenzenu nafanya kazi za kuuza dukani usiku bila noma maana I had set my goals.Kuna vijana wakibongo walikua wanakuja pale wakitoka klabu huku wamebwia na zereu zao....eti wanashangaa nafanya kazi na kuajiriwa nami nikawa siwajibu kitu maana I knew what I was doing to secure my future in this country. Basi nikafanya mitihani ya kupata leseni na mambo yakatiki na mwenzenu nikaaply katika shule kadhaa. Nilipopata majibu na kuenda interview mambo tena yakakubali na nikapata kazi katika shule za serikali na nikapata sehemu napiga tuition na Sylvan Education Systems ambao ni kama private flani hivi na malipo yao poa kinoma . Hela yangu ikawa safi, bills zote nalipa, medical insurance ninayo na familia iko poa(nina mke na watoto wawili wa kike). Juzi likizo ya krismasi nimetinga vekeshen ya nguvu na kulala hotelini siku sita na tripu ya mbungani nikapiga. Hivi sasa nimerudi back to base na niko poa kishenzi.
Kwa hivyo hawa wanaosema wanarudi Africa kwa kua maisha ughaibuni hayafai au hayawezekani wana lao jambo. Mtu anaeza kusema anakampuni yake lakini ukienda kumtembelea unakuta ishu zote anafanyia chumbani kwake na amerejista jina la kampuni yake ili kujaribu kusifia watu nyumbani kua ana kampuni. Hii ni kutafuta sifa za kimpumbavu na kuwaonyesha washkaji kijiweni kua ni mkulu flani. Kumbuka alipotoka home alikua keshasema anaenda Marekani kufanya vitu vya nguvu. Anapoingia kiwanja anakuta mambo tofauti na inabidi 'akili mukichwa'. Nishaona wengi wameingia na kujifanya wao ni watoto wa wakulu bongo na kwa hivyo hawataki kazi za kuajiriwa...yaani waleta dharau wakikuona mchizi unahangaika na dei waka yako au night shift mahala flani. Anatesa miaka miwili afu hela zinapogoma kutoka home inabidi atafute usawa mwengine. At that time kumbuka mtu hakuenda shule kutimiza ahadi ya viza yake, ashachelewa kutafuta SSN na ID na pia visa ime-expire na sasa ashapoteza status. Sasa vijana wetu kama hawa ndo wanalia njaa na kufanya kazi zisizoeleweka...hata pia kuanza kuuza madawa. Hapo ndo mwisho wa barabara yake....:rip:
Kwa hivyo its upon the individual and what his/her goals are. Ukija ughaibuni kwa vile unataka 'uwakomesha' washkaji mtaani basi utaambulia patupu. Ukija na set plans na unapiga mambo yako kimpango, I can say here confidently you will definitely be better off. Mimi nimeishi uswahilini, nimepanda dalala nikienda kazini, nimekula chipsi vumbi ili mradi nistiri njaa...nimepiga kazi ya serikali ambapo mshahara ulikua wakipuzi huku ukizangatia kua viongozi ni mafisadi na hawajali maslahi ya watu wanaofanya kazi serikalini. Nikilinganisha these two situations, I can say I'm better off a thousand times where I'm at. Sio kujisifu lakini ni kwa sababu nilifanya mambo yangu kwa mpango na sasa navuna. Nikija Africa, natesa kiheshima na narudi bila hata kuenda ubalozini kuomba viza. Msiba ukitokea natoe hela ya kugharimia wageni watakaofika home na pia nasafiri kuonyesha solidarity. Vijana wetu wengi wako out of status na wanajua wazi wakirudi home, Marekani hawatoiona tena. Wako wengi tu hapa wamepoteza wazazi na wanashindwa kuenda kuzika!!!...Yaani ni huzuni mtupu. Kazi wanazofanya hazieleweki, medical insurance hawana na ole wao wapate matatizo ambayo itabidi watinge hospitalini...hio bili itabidi walipe for the rest of their lives!
My advice to people ni kwamba ukija huku, don't put your expectations too high and be real. Fanya yaliokuleta huku kulingana na viza yako for at least 2yrs huku ukiangalia maswala ya papers.
Senti yangu hamsini hio.
Mungu ibariki Africa