Ndoto Yaisha Vibaya, Amnyonga Mkewe Usingizini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndoto Yaisha Vibaya, Amnyonga Mkewe Usingizini

Discussion in 'International Forum' started by Mbonea, Nov 19, 2009.

 1. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  </SPAN>


  Brian Thomas na mkewe Christine anayetuhumiwa kumuua usingizini

  Ndoto ya mwanaume mmoja nchini Uingereza imeisha vibaya baada ya kumuua mkewe wa ndoa ya miaka 40 kwa kumnyonga akiwa usingizini wakati alipoota anamkaba koo mwizi aliyeingia kwenye chumba chao.


  Mwanaume mmoja nchini Uingereza amemuua mkewe usingizini baada ya kuota mkewe ni mwizi aliyeingia kwenye chumba chao na kuanza kumkaba koo, mahakama nchini Uingereza iliambiwa.

  Brian Thomas, 59, na mke wake Christine, 57, ambaye ameishi naye kwa miaka 40 walikuwa kwenye vakesheni ndani ya gari lao aina ya caravan wakati Brian alimponyonga mkewe usiku wa manane.

  Mahakama iliambiwa kuwa Brian aliota ndoto mwizi amevunja na kuingia ndani ya gari lao la vakesheni.

  Alikuwa akiota anapambana na mwizi huyo na matokeo yake kumbe alikuwa akimkaba koo mpenzi wake wa tangia utotoni ambaye ameishi naye maisha ya ndoa kwa miaka 40.

  Mahakama ya mji wa Swansea iliambiwa jana kuwa Brian alikuwa akisumbuliwa na matatizo sugu ya usingizi na alikuwa hajijui wakati huo anafanya kitendo hicho.

  "Hii ni kesi ya aina yake, sio ya kawaida", alisema mwendesha mashtaka Paul Thomas.

  "Wataalamu wa usingizi wamemfanyia uchunguzi Brian na wametoa ripoti kuwa hakufanya kitendo hicho kwa kukusudia".

  "Hawezi kutiwa hatiani kwa kitendo chake", alisema mwendesha mashtaka huyo.

  Mahakama iliambiwa kuwa Brian na mkewe walionekana siku ya tukio hilo wakila nyama na chipsi pamoja mbele ya gari lao.

  Siku hiyo walienda kulala mapema lakini usiku wa manane, Brian alianza kuota ndoto amevamiwa na mwizi.

  Hapo ndipo Brian alipoanza kumkaba koo mkewe akiota anapambana na mwizi huyo aliyeingia kwenye caravan lao.

  Polisi walimkuta Christine akiwa ameishafariki baada ya kukabwa sana koo.

  Wanandoa hao ambao wana watoto wawili wa kike na walikuwa wapo kwenye hatua za mwisho za kuanza likizo kwenye meli kubwa ya kifahari kuzunguka bahari ya Mediterranean katika kusherehekea ndoa yao kutimiza miaka 40.

  Kesi hiyo inaendelea,  Source: Daily Mail
   
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Ndoto zingine, kaazi kweli kweli,

  I think huyu jamaa alikuwa na nia mbaya!
   
Loading...