Ndoto ya Urais ya Lowassa na Zitto mashakani CCM kufanya zengwe katika Katiba mpya

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
*CCM yataka Katiba iweke kikomo cha miaka 40 hadi 60
*Walioshika nafasi ya uwaziri mkuu kubanwa
*Mkakati waandaliwa kutua rasmi Tume ya Katiba

SIKU chache tangu Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), atangaze kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, huenda ndoto yake isitimie kutokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuandaa mkakati wa kumbana kupitia Katiba mpya.

Mbali na Zitto ambaye alitangaza kutogombea ubunge na badala yake anajipanga kuwania urais mwaka 2015, wengine wanaotajwa kuwania nafasi hiyo ni Waziri Mkuu mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli Edward Lowassa (CCM).

Zitto
Zitto hadi kufikia mwaka 2015 atakuwa na umri wa miaka 39 wakati Lowassa atakuwa na umri wa zaidi ya miaka 60.

Kiongozi mwingine anayetajwatajwa kutaka kuwania nafasi hiyo, ni Waziri Mkuu mstaafu mwingine, Frederick Sumaye ambaye sasa ana umri wa miaka 62.

Inaelezwa kuwa mkakati huo umelenga kuzuia vijana ambao wanaonekana wana ndoto ya kuwania nafasi hiyo ikihofiwa watatoa upinzani mkali kwa viongozi wakongwe.

Kipengele kimoja kinachotajwa ambacho huenda kikaingizwa katika Katiba mpya ni umri wa mgombea urais ambao unapendekezwa uwe miaka 40 hadi miaka 60, lengo likiwa ni kuwadhoofisha makada wa CCM ambao wanaonekana kuwa tishio ndani ya chama.

Inaelezwa kuwa hivi sasa inaendeshwa kampeni ya chini chini kuleta ushawishi kupitia mikutano ya maoni huku pia mapendekezo hayo yakiandaliwa kwa maandishi na baadaye yawasilishwe mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaendelea na kazi ya kukusanya maoni kwa wananchi.

Chanzo chetu kutoka ndani ya CCM kiliiambia MTANZANIA Jumapilikuwa mbali na harakati hizo,kipengele kingine ni kile kinachohusu viongozi walioshika cheo cha uwaziri mkuu kutakiwa wasiruhusiwe kugombea urais.

“Pamoja na kutangazwa kwa uchaguzi wa chama, lakini bado lengo la kufanya hivyo ni kujenga timu imara ya chama itakayowezesha ushindi mwaka 2015. Katika hili inaonekana wazi kuwa baadhi ya wanachama wanaonekana ni tishio hasa katika kuwania nafasi hii watakwaa kisiki.

“Siyo siri tena, Lowassa na Sumaye ni watu ambao wanatajwa kutaka kuwania nafasi hii lakini bado wanaonekana tatizo ndani ya chama… hivi sasa unaandaliwa mkakati wa kuwabana kupitia Katiba mpya ili mwanachama yeyote aliyefikisha miaka 60 asiruhusiwe kugombea nafasi hiyo.

“Lakini bado inaonekana kuna kundi kubwa la vijana wa ndani ya chama na nje ambao wanaonekana kuitamani nafasi hii, nao wanataka kubanwa kupitia umri ambao ataruhusiwa yule aliyetimiza umri wa miaka kuanzia miaka 40.

“Katika hili nataka nikwambie CCM kama itafanya jambo hili ndiyo itakuwa mwisho wake kwani linaweza likajitokeza kundi na kupambana aweze kupatikana mgombea binafsi kupitia Katiba mpya ijayo.

“Hivi sasa tunatakiwa kujenga chama imara ambacho kitaweza kutetea nafasi yake ya Urais mwak 2015,” kilisema chanzo hicho kutoka makao makuu ya CCM mjini Dodoma.

MTANZANIA Jumapili ilimtafuta Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye azungumzie mkakati huo lakini simu yake ya kijangani haikuwa hewani muda mwingi jana.

Septemba 27 mwaka huu akiwa mjini Kigoma, Zitto alitangaza kuwa mwaka 2015 hatagombea ubunge bali urais kupitia Chadema huku akitahadharisha dhamira yake hiyo isije ikavuruga chama.

“Nimefanya kazi kubwa ya ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi changu cha miaka 10.

“Kama Mungu ataniweka hai mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwani kazi niliyoifanya inatosha. Natangaza rasmi nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola.

“Nataka kuleta changamoto kubwa mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao lakini huo ndiyo msimamo wangu, iwapo chama kikiona nastahili au sifai nitakubaliana na uamuzi huo,” alisema Zitto, katika kongamano hilo lililoandaliwa na asasi ya Meza Duara.
 
kweli jamani kuandikaga mahabari ya hisia zenu ni kuhatarisha usalama wa Taifa.tuwe waadilifu
 
Sosi Mtanzania

Chama Cha Mapinduzi CCM kinaandaa dodoso na mapendekezo kama chama na kupendekeza yaingizwe katika katiba mpya kuwa na ukomo wa umri wa kugombea urais wa nchi kati ya miaka 40 Hadi 60 ikidaiwa ikiwa ni lengo la kuwaengua watu amabao wanaonekana kuwa ni mwiba kwao kama Lowassa, Zitto na Dr. Slaa.
Kweli Lowassa ni kiboko ya CCM. Lowassa ana Mungu na umma.
 
kwa hiyo CCM wanataka kuendelea kubaka demokrasia? hawajui katiba lazima izingatie haki za raia ambazo msingi wake mkuu ni haki za binadamu? Au huko CCM hata wasomi wao wote ni MBUMBUMBU!
 
Katiba ya sasa inatambua kila raia ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa.kuweka age limit ili kuwazuia baadhi ya watu wasigombee ni kuwa na akili za mgando plus udhaifu.
 
Katiba ya sasa inatambua kila raia ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa.kuweka age limit ili kuwazuia baadhi ya watu wasigombee ni kuwa na akili za mgando plus udhaifu.

Inasema ivyo ili kuwafanya wasioijua Tz kuamini hayo lakini ukweli sio
 
they can't do that coz it against the constitution and if ammendent may take place that may led the party CCM to merge into two or more pieces.Please those who wish to do that infact is not healthy to our national security and it may lead to lot of misunderstanding within public sectors.Let you find another alternative or let the mass decide on that inssue than a group of people within the party.
 
Mkuu, nilitaka kuchangia hoja yako lakini kiingeredha chako kigumu!!!. maana hata muingereza mwenyewe hawezi kukuelewa.
 
JUMAPILI, SEPTEMBA 30, 2012 09:53 NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

*CCM yataka Katiba iweke kikomo cha miaka 40 hadi 60
*Walioshika nafasi ya uwaziri mkuu kubanwa
*Mkakati waandaliwa kutua rasmi Tume ya Katiba

SIKU chache tangu Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), atangaze kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, huenda ndoto yake isitimie kutokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuandaa mkakati wa kumbana kupitia Katiba mpya.

Mbali na Zitto ambaye alitangaza kutogombea ubunge na badala yake anajipanga kuwania urais mwaka 2015, wengine wanaotajwa kuwania nafasi hiyo ni Waziri Mkuu mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli Edward Lowassa (CCM).

Zitto

Zitto hadi kufikia mwaka 2015 atakuwa na umri wa miaka 39 wakati Lowassa atakuwa na umri wa zaidi ya miaka 60.

Kiongozi mwingine anayetajwatajwa kutaka kuwania nafasi hiyo, ni Waziri Mkuu mstaafu mwingine, Frederick Sumaye ambaye sasa ana umri wa miaka 62.

Inaelezwa kuwa mkakati huo umelenga kuzuia vijana ambao wanaonekana wana ndoto ya kuwania nafasi hiyo ikihofiwa watatoa upinzani mkali kwa viongozi wakongwe.

Kipengele kimoja kinachotajwa ambacho huenda kikaingizwa katika Katiba mpya ni umri wa mgombea urais ambao unapendekezwa uwe miaka 40 hadi miaka 60, lengo likiwa ni kuwadhoofisha makada wa CCM ambao wanaonekana kuwa tishio ndani ya chama.

Inaelezwa kuwa hivi sasa inaendeshwa kampeni ya chini chini kuleta ushawishi kupitia mikutano ya maoni huku pia mapendekezo hayo yakiandaliwa kwa maandishi na baadaye yawasilishwe mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaendelea na kazi ya kukusanya maoni kwa wananchi.

Chanzo chetu kutoka ndani ya CCM kiliiambia MTANZANIA Jumapilikuwa mbali na harakati hizo,kipengele kingine ni kile kinachohusu viongozi walioshika cheo cha uwaziri mkuu kutakiwa wasiruhusiwe kugombea urais.

"Pamoja na kutangazwa kwa uchaguzi wa chama, lakini bado lengo la kufanya hivyo ni kujenga timu imara ya chama itakayowezesha ushindi mwaka 2015. Katika hili inaonekana wazi kuwa baadhi ya wanachama wanaonekana ni tishio hasa katika kuwania nafasi hii watakwaa kisiki.

"Siyo siri tena, Lowassa na Sumaye ni watu ambao wanatajwa kutaka kuwania nafasi hii lakini bado wanaonekana tatizo ndani ya chama… hivi sasa unaandaliwa mkakati wa kuwabana kupitia Katiba mpya ili mwanachama yeyote aliyefikisha miaka 60 asiruhusiwe kugombea nafasi hiyo.

"Lakini bado inaonekana kuna kundi kubwa la vijana wa ndani ya chama na nje ambao wanaonekana kuitamani nafasi hii, nao wanataka kubanwa kupitia umri ambao ataruhusiwa yule aliyetimiza umri wa miaka kuanzia miaka 40.

"Katika hili nataka nikwambie CCM kama itafanya jambo hili ndiyo itakuwa mwisho wake kwani linaweza likajitokeza kundi na kupambana aweze kupatikana mgombea binafsi kupitia Katiba mpya ijayo.

"Hivi sasa tunatakiwa kujenga chama imara ambacho kitaweza kutetea nafasi yake ya Urais mwak 2015," kilisema chanzo hicho kutoka makao makuu ya CCM mjini Dodoma.

MTANZANIA Jumapili ilimtafuta Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye azungumzie mkakati huo lakini simu yake ya kijangani haikuwa hewani muda mwingi jana.

Septemba 27 mwaka huu akiwa mjini Kigoma, Zitto alitangaza kuwa mwaka 2015 hatagombea ubunge bali urais kupitia Chadema huku akitahadharisha dhamira yake hiyo isije ikavuruga chama.

"Nimefanya kazi kubwa ya ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi changu cha miaka 10.

"Kama Mungu ataniweka hai mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwani kazi niliyoifanya inatosha. Natangaza rasmi nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola.

"Nataka kuleta changamoto kubwa mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao lakini huo ndiyo msimamo wangu, iwapo chama kikiona nastahili au sifai nitakubaliana na uamuzi huo," alisema Zitto, katika kongamano hilo lililoandaliwa na asasi ya Meza Duara.

Nitaunga Mkono hayo Mapendekezo ya CCM kwenye KATIBA tu kumg'oa ZITTO KABWE
 
stupid mentality hizi
katiba ina guide nchi miaka hata 500 ijayo
sasa wewe unataka katiba inayomlenga mtu mmoja kwa mwaka 2015 tu?
 
Sawa hadithi imefika lakini Mtanzania wangekuja na uchambuzi kuelezea wale ambao ni vijana na wana umri wa miaka kati ya 40 na 60, na ambao wanaonekana kufaa kugombea uraisi 2015.
 
398252_356935811059035_1236336384_n.jpg

Oh Where Our leaders always choose!!!
 
mbona kuna habari umu hua haziulizwi source ila ikionekena not in some guyz favor utaskia source mku au mnaleta habari za hisia zenu apa! hahahaahaha!!,kaz ipo! mi napta zangu tu bhana!
 
they can't do that coz it against the constitution and if ammendent may take place that may led the party CCM to merge into two or more pieces.Please those who wish to do that infact is not healthy to our national security and it may lead to lot of misunderstanding within public sectors.Let you find another alternative or let the mass decide on that inssue than a group of people within the party.
yalaaaaaaaaaa.......
 
Back
Top Bottom