Ndoto Ya Seif Sharif Hamad Kuingia Ikulu Ya Zanzibar

Watu waache unafiki, mnadiriki kusema kashinda kihalali? Mtu hawezi kushinda urais hadi atangazwe. Atakoma tu na hawezi kuwa rais wa Zanzibar. Huyu na Jambazi Sugu hawana tofauti, makuwadi wake wanaoandamana Ulaya wampokee kama mkimbizi.
 
Kwa jinsi shein anavyokagua miradi ya naendekeo toka atoke dodoma nahisi kama anataka kukabidhi nchi kwa seif ili awe na aman baba wa watu.

Sio kwamba ameahidiwa hakuna kutoka
 
Suala sio historia wote twaijua. Issue in Seifu kashinda na ape we haki yake full stop achana na longo longo nyingi
 
Ndugu zangu,

Historia ni Mwalimu Mzuri. Nimelisema hilo mara kadhaa.

Wakati fulani mwaka 1984, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar walikutana pale Kisiwandui chini ya Alhaj Aboud Jumbe, aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa JMT.


Ndani ya kikao kile walikuwamo wanasiasa wa aina ya Ramadhan Haji Fakhi, huyu alikuwa Waziri Kiongozi, alikuwamo pia Hamad Rashid, Hamis Shabaan Mloo, na Seif Sharif Hamad.
Wajumbe walizungumza jasho likiwatoka juu ya hali isiyo sawa kwenye Muungano yakiwemo madai kuwa Zanzibar haikuwa hata na fursa ya kukopa nje ya nchi kwa vile imo ndani ya Muungano. Ikajengwa hoja ya Serikali Tatu. Wajumbe wote wakaafiki. Ikafika siku ya kuwasilisha hoja Dodoma.

Ajabu ya jambo lile, Julius Nyerere, alionekana kulijua hilo mapema sana. Alhaj Jumbe mkutanoni Dodoma akawa na wakati mgumu.

Wenzake wote akiwamo Seif Sharif Hamad waliikana hoja isipokuwa Ramadhan Haji Fakhi, Waziri Kiongozi.

Inasemwa, Julius Nyerere alimuuliza Ramadhan Haji Fakhi; " Moja jumlisha moja ni ngapi?" Jibu: " Tatu!" Inasemwa pia, Julius Nyerere aliwachekesha wajumbe alipohoji ni shule gani aliyesoma Ramadhan Haji Fakhi yenye kufundisha hesabu kwa namna hiyo!

Hatma ya kikao kile cha Dodoma ni Alhaj Jumbe kuvuliwa nyadhifa zake zote ndani ya chama ikiwamo kuachia Urais wa zanzibar. Ramadhan Haji Fakhi pia akunusurika, alikwenda na maji. Ali Hassan Mwinyi akafanywa kuwa Rais wa Zanzibar na Seif Sharif Hamad akawa Waziri Kiongozi.

Mwaka mmoja na nusu baadae, mwaka 1985, Ali Hassan Mwinyi akateuliwa kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano na akawa Rais kwa kuchaguliwa na Wananchi.
Inasemwa, kwa vile Ali Hassan Mwinyi alipata fursa hiyo, basi, Seif Sharif Hamad alitumaini angekuwa Rais wa Zanzibar.

Hapana, CCM ikamteua Idrissa Abdul Wakil kugombea nafasi ya Rais wa Zanzibar. Seif Sharif Hamad akawa ameukosa Urais na akafanywa kuwa Waziri Kiongozi. Kukawa na minong'ono ya Seif kulalamika chini chini.

Ikafika wakati kukawa na ' Hali ya Hewa ya kisiasa Iliyochafuka Visiwani'. Nilikuwa mwanafunzi pale Tambaza Sekondari. Ilinong'onwa mjini kuwa Rais wa Zanzibar, Abdul Wakil, kutokana na hali ya hewa kuchafuka, akawa anafanya kazi Unguja na anarudi kulala Dar es Salaam.

Siku moja wakati nikitoka shule na kupita maeneo ya Upanga kuelekea kituo cha mabasi cha Palm Beach, kwenye moja ya nyumba za eneo hilo, nikamwona kwa macho yangu Rais wa Zanzibar, Idrissa Abdul Wakil. Nikafahamu baadae, kuwa aliishi kwenye moja ya nyumba za eneo hilo.

Mwaka 1988, akina Seif Sharif Hamad , Hamad Rashid na wenzao, walitaka hoja ya Serikali Tatu ipelekwe tena Dodoma. Safari hii Idrissa Abdul Wakil aliipinga kutokana na uzoefu wa 1984.

Seif Sharif Hamad naye akaishia kupokonywa kadi yake ya uanachama CCM. Vuguvugu la mageuzi ya kisiasa duniani likaanza kwenye kipindi hicho. Lilitokea Ulaya Mashariki.

Ndipo akina Seif Sharif Hamad wakapata fursa ya kuanzisha KAMAHURU. Na baadae CUF ikaja pia. Na ndoto ya Seif Sharif Hamad ikabaki hai, ndoto ya siku moja kuwa Rais wa Visiwa vya Zanzibar.

Mwaka huu wa 2015, Seif Sharif Hamad amerusha tena karata yake. Anaweka rekodi, ya kuwa mgombea mkongwe kushinda wote, na mwenye uzoefu wa kugombea Urais kwa zaidi ya miaka 20. Kuna tunachojifunza.

Ndugu zangu Wajumbe, Nimejaribu kukumbuka hayo. Nakaribisha maoni yenu pia

Mjengwa blog.

Tanzania kwa maoni yangu demokrasia ipo kwenye makablasha tuu na sio kwa vitendo.
Kwa tanzania, demokrasia nipale ccm inashinda tuu. Wakishinda wapinzani, ccm lazima ifanye figusufigisu ili mradi tu wao waendelee.
Kwa ccm na viongozi wa staaf yaani ma rais, nadhani hawaitaki meema hii nchi. Demokrasia itabidi iangaliwe upya na kwa mapana zaidi. Na mie naona ndo maana watu wengi watafika mahali wataacha hata kupiga kura kwa sababu ya vitendo vya kuminya demokrasia.
Kuna watu nchini hapa walizaliwa na watakufa kwakuufahamu uongozi wa ccm tuu, kitu ambacho sio kizuri. Ndo maana leo unazungumzia ya Jumbe.
 
Tungekua na Demokrasia ya kweli jamaa alikua Raisi tangu 1995

Haya yote ni sawa ila sasa ni kwanini ajitangazie ushindi ndo utaratibu wa wapi huu au ndo kiu kali ya kutawala Zanzibar?
 
Suala sio historia wrote twaijua. Issue in Seifu kashinda na ape we haki yake full stop achana na longo longo nyingi

"Idadi ya wapiga kura walioandikishwa Pemba kaskazini ni 4500. Matokeo. Seif Sharif Sharif Hamad Kura 4120, Dr. Shein kura 2315" Duuh! hayo matokeo hats ningekuwa Mimi mkurugenzi Wa ZEC ningefuta tu matokeo, tuchunguze nini kilitokea.
 
Haya yote ni sawa ila sasa ni kwanini ajitangazie ushindi ndo utaratibu wa wapi huu au ndo kiu kali ya kutawala Zanzibar?

Seif alikusanya Matokeo kutoka vituo na majimbo yote. Pia anaelewa mchezo mchafu wa CCM na ZEC kupika (kuchakachua) matokeo, ameibiwa 1995, 2000, 2005 na 2010. Mara hii alilofanya Seif ni kuzuia goli la mkono kwa kuweka hadharani idadi ya kura alizokusanya kupitia fomu za matokeo kutoka majimbo na kuiomba ZEC iharakishe kutoa matokeo kulingana na fomu zilizotumwa kutoka majimboni na sio matokeo aliyonayo Jecha mfukoni. Ukiita hiyo ni "kujitangaza" mshindi, kosa la kujitangaza mshindi ni kosa la jinai na lina adhabu zake kisheria.

Kwa hiyo, hiyo sio sababu kwa ZEC ifute uchaguzi na matokeo yake.

Kwa nini ZEC haijafikisha malalamiko polisi ili Seif akamatwe na afikishwe mbele ya vyombo vya Sheria?

CCM inatafuta njia mbadala tu ya kufunga goli la mkono.
 
"Idadi ya wapiga kura walioandikishwa Pemba kaskazini ni 4500. Matokeo. Seif Sharif Sharif Hamad Kura 4120, Dr. Shein kura 2315" Duuh! hayo matokeo hats ningekuwa Mimi mkurugenzi Wa ZEC ningefuta tu matokeo, tuchunguze nini kilitokea.
Watu waache unafiki, mnadiriki kusema kashinda kihalali? Mtu hawezi kushinda urais hadi atangazwe. Atakoma tu na hawezi kuwa rais wa Zanzibar. Huyu na Jambazi Sugu hawana tofauti, makuwadi wake wanaoandamana Ulaya wampokee kama mkimbizi.
Tuache ushabiki, tutumie akili, kufikiri.



 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom