Ndoto ya mchana haifai, nmechukia sana.

Ndoto ya mchana haifai, nmechukia sana.

mcrounmj

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2016
Posts
379
Reaction score
903
Rebeca ni binti mrembo, huwa navutiwa sana kumwangalia japo najua mimi na yeye ni levo tofauti, mimi mwanafunzi na yeye ni lecturer kwenye chuo chetu. Rebeca ni mkorofi, anapenda kujibu dry pindi ninapomkaribia kuulizia chochote, amekuwa akinipa treatment tofauti na wenzangu na muda mwingine najikuta napata alama za chini kwenye course yake.

Sasa bahati mbaya semester hii ya mwisho, Rebeca amekuwa supervisor wa research yangu. Maumivu ninayoyapata ni makubwa. Pamoja na kuwa lecturer lakini kama bado ana utoto mwingi. Anapenda kuniita ofisini kwake, hana la maana analoniambia, basi mimi moyo unaniuma mnoo maana nampenda kumwambia nahisi nitadisco chuo.

Leo kaniita ofisini kukamilisha marekebisho ya research, bahati mbaya vifungo viwili vya juu vya shati langu havikufungwa kwa KUJISAHAU, Rebeca kanisahihisha makosa ya research yangu adi mwisho vizuri kwa lugha laini, leo nimemwelewa madam wangu. Wakati nataka kutoka ndio akanijulisha kufunga vifungo.

Nimewaza nimutokee nimpe mashairi sijui atanielewa!

Ntamweleza, tofauti na anavyoniona kama mwanafunzi, mimi ni mwanamme makini, imara na mwenye upeo wa juu. Pamoja na elimu yake ya juu nitaweza kummudu, kwani ninazo juhudi za kujituma na nina ndoto kubwa kwenye maisha. Nmejipanga naenda kumtokea madam wangu Rebeca liwalo na liwe.

Nashtuka kutoka usingizini, kumbe ilikuwa ni ndoto. Simujui Rebeca, sjawahi kumuona na wala si mwanafunzi wa chuo. Nimebaki nina hamu, natamani ingekuwa kweli. Rebeca wangu kumbe alikuwa wa kwenye ndoto, ndoto ya mchana haifai.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] hyo ndoto ..!
 
Sasa wewe lala tena ila ukianza kuota tena usisahau namba ya simu na ikiwezekana chukua namba ya simu kwa mawasiliano yaliyo rahisi
 
Back
Top Bottom