Ndoto "mpya" ya kakobe yaitesa ukawa!

Ndoto "mpya" ya kakobe yaitesa ukawa!

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Posts
7,146
Reaction score
3,829
Wana Ukumbi,

Kama ilivyo kawaida kwa askofu Kakobe kuota ndoto mbalimbali kuhusu mambo yanayohusu mstakabali wa taifa letu. Askofu Kakobe ameota ndoto nyingine ambayo inawahusu UKAWA na harakati zao za kudai katiba ya wananchi.

Katika ndoto hiyo ya askofu Kakobe ambayo ameitoa leo katika ibada ya jumapili kwenye kanisa lake, amesema kuwa, kutokana na hali ya ubaguzi uliokithiri kwenye upinzani kupitia umoja wao huo wa UKAWA, haoni kama kutakuwa na mafanikio yoyote ya malengo ya wana UKAWA.

Askofu Kakobe katika kufafanua alieleza kwamba, viongozi wa UKAWA hasa mhe Mbowe hakuwa sahihi katika maamuzi yake ya kuwatenga waasisi wa upinzani nchini, akimaanisha mhe Mrema. Hivyo, kitendo hicho cha ubaguzi kitaondoa baraka iliyokuwa imepandikizwa awali kwenye umoja huo.

My take,

Ni vyema sasa mhe Mbowe akachukua onyo hili na kufanya maamuzi sahihi ya kumuunganisha mhe Mrema na UKAWA. Kwa kuwa wote tunajua nguvu ya kiutabiri aliyonayo nabii Kakobe.
 
Kumbe Katortoise nae anatoa baraka badala ya Mungu na kumbe ndio mwenye kujua mustakabali wa harakati mbali mbali? Nahisi kawa mrithi wa yahaya mtabiri....AMEFUA
 
Ile nyingine ya CCM ishatimia? Mwache awadanganye wajinga wenzake. Anaumwa tu huyu!!!!!!!!
 
Kakobe na Mrema kuna nini...wanamakubaliano gani mpaka awe anamtetea hivi?!
 
Ukawa ni kikundi cha wanasiasa wenye lengo moja, sasa anataka Mrema awe pamoja nao wakati yeye ana malengo tofauti na wenzake? Kisa ni muanzilishi wa upinzani? Kobe kasha zeeka sasa
 
Mmh! Kama kweli Kakobe alimkusudia Mrema kwenye kauli yake, basi atakuwa anawachanganya wananchi, na pia anajichanganya mwenyewe. Mrema alijipambanua wazi kwenye BMK kuwa yeye anaunga mkono serikali 2. Sasa sioni UKAWA wanaweza kumuunganisha vipi kwenye kundi lao wakati wanatofautiana kimtazamo kuhusu muundo wa Muungano!
 
Labda kwa kuwa sikuwepo kanisani ndio mana sikupingi, lakini hebu na wewe onesha mshangao kidogo kwa kuwa malengo ya UKAWA ni rasimu ya Warioba wakati Mrema aliipinga rasimu hadharani. Je, ni kweli UKAWA wamekosea kumuacha Mrema na msimamo wake wa S2? Ila umejitahidi kuelezea kwa upeo wa akili yako
 
Kakobe ameona UKAWA tu, inamaana huyo Mrema hana sehemu nyingine yakujiunga.
 
Mustakabali wa taifa hautegemei ''NDOTO'' ,unategemea UWAJIBIKAJI wa kila mwenye WAJIBU ili kujenga taifa bora. NDOTO ni maluwe-luwe tu ambayo humtokea mtu yeyote hata mwenda-wazimu.
 
Kwa kuwa UKAWA ni watetezi wa wanyonge...naimani Mungu atazidi kuwakumbatia na kusambaratisha roho ya utengano..MATHAYO 5:9 "Heri wapatanishi; maana hao wataitwa wana wa Mungu"
 
Mh.mbowe hajatangaza baraza la mawaziri la UKAWA ika UKAMA inahusu katiba.kama Mrema anadhani ana vigezo karibu mtaani
 
Kumbe Katortoise nae anatoa baraka badala ya Mungu na kumbe ndio mwenye kujua mustakabali wa harakati mbali mbali? Nahisi kawa mrithi wa yahaya mtabiri....AMEFUA

hahaha ndoto ni maruerue asee inaonekana kabla ya kulala alkua anaifikiria sana ukawa.ajiunge na yy
 
Back
Top Bottom