mkubhi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2015
- 2,216
- 3,319
Wakuu habari zenu,
Mimi naitwa Elias. Nikiwa chuoni mwaka wa kwanza mwaka 2012 nilipoteza kaka yangu niliyekuwa namfatia kuzaliwa, ifikapo tena mwaka 2014 nikiwa bado chuoni nikafiwa tena na baba mzazi kabisa. Ila kinachoniumiza zaidi nikuendelea kumuota kaka yangu nikiwa nae tangia kwa kipindi chote hicho.
Na ikumbukwe baba ndo ametoka mda wa karibuni kuliko hata kaka simuoti kabisa japo nilikuwa nampenda sana pia.
Kwa mda wote wa kuanzia 2012 nilipoteza kaka wiki ikisha bila kumuota niko naye inakuwa bahati ila karibia kila wiki ni lazima nimuote Mara mbili au zaidi ya. Inafikia wakati naogopa labda na mimi nimekaribia kumfata huko alipo yaani na mimi kufariki.
Wadau naombeni msaada wenu wa kujinasua katika ndoto hii kwa sababu na nyanyasika sana yaani kila siku baada ya kushituka kwenye hii ndoto msiba unakuwa kama umeanza upya.
Natanguliza shukurani na naomba mtu asiweke utani katika hili!
Post sent using JamiiForums mobile app