Ndondondo si...

Qzam

Member
Mar 5, 2023
26
22
Huu msemo ni wa kawaida sana. Ukiutafakari una maana nzito sana.

Kinachoingia kidogokidogo huchukua muda mrefu ila hakilingani na kinachoingia haraka. Kinachoingia kdgkdg kinadumu sana kuliko cha haraka na mengine mengi.

Maana yangu nini, watu wengi wanapenda vitu vinavyotoa majibu ya haraka,biashara ya faida kubwa kwa muda mfupi, ulime shamba msimu mmoja utajirike.

Kiuhalisia hivi vitu haviwezekani.Tunapaswa tujifunze uvumilivu na malezi sahihi ya kila tunachofanya biashara,familia,kazi hata akiba,usidharau kuweka mia ukitegemea kuanza na mia ambayo huna UTAFELI.
Ndo maana watu wanapoteza pesa kwa wingi sana sababu ya kutaka faida kubwa kwa muda mfupi.

Anza kidogo Lea jambo lako hatua kwa hatua,hata ukianguka hutaumia sana ni rahisi kuanza tena,utajenga nidhamu na falsafa ambayo itasimama kwa vizazi.Hawa wenzetu wahindi nk mambo yao hudumu muda mrefu sababu ya hii ambayo kwao imekuwa ni utamaduni.

TUBADILIKE.
 
Wahenga walisema ndondondo si churuuruu, ipo siku moja utafanikiwa, siku ikifika utapata nawee

Sauti ya MTAMILE kutoka BANA MWAMBE..nyimbo maisha ya kila siku.
 
Back
Top Bottom