NDONDI: Keith Thurman atamba kumstaafisha Man Pacquiao kesho

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
9,726
2,000
Kesho ni siku nzuri kwa wapenzi wa ndondi, dunia itashuhudia mapambano ya kuvutia kati na 'Legend' aliyegoma kustaafu Senator Man Pacquiao kutoka ufilipino dhidi ya bingwa anayeshikilia mkanda wa WBA (welterweight) kutoka Marekani Keith 'OneTime' Thurman ambaye hajawahi kupigwa. Keith Thurman katika press conference alinukuliwa akisema anamuheshimu sana Pac kama legend na amefurahi kupata nafasi ya kushea naye ulingo though "don't be surprised if Man Pacquiao goes nite nite", akimaanisha tusishngae kumuona Pac akilamba sakafu. Pambano hilo litafanyika Marekani MGM Grand kesho alfajiri.

Vilevile siku ya kesho dunia itashuhudia pambano jingine la kuvutia la uzito wa juu kati ya Dillian Whyte kutoka Uingereza dhidi ya Oscar Rivaz kutoka Columbia. Pambano hilo linatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na mabondia wote kuwa na rekodi nzuri, Wote wamecheza mapambano 26, Whyte akipoteza moja dhidi ya AJ, kwa upande wa Rivaz hajawahi kupoteza. Pambano hilo ni la muhimu sana kwa Dillian Whyte kwani akishinda litampatia tiketi moja kwa moja ya kupigania mkanda wa WBC , ambapo atasubiria mshindi wa pambano la Wilder vs Fury litakalofanyika February mwakani. Pambano hili litafanyika London Uingereza usiku wa kuamkia kesho.
Screenshot_20190720-084039_1563604139552.jpeg
Screenshot_20190720-084822_1563604110040.jpeg
Screenshot_20190720-085208_1563604051183.jpeg
Screenshot_20190720-085245_1563603989010.jpeg
 
screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
9,726
2,000
Kwenye pambano la WHYTE vs RIVAZ kutakuwa na pambano jingine la kusisimua 'undercard' la uzito wa juu kati ya CHISORA na SZPILKA
Screenshot_20190720-085228_1563604018431.jpeg
 
screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
9,726
2,000
Mnigeria mwenye ngumi za kutisha ambaye mapambano yake yote anayamaliza ndani ya Round 2 'EFE AJAGBA' atapigana na Mturuki 'undercard' kwenye pambano la Pacquiao vs Thurman. This man is the next big thing, kina Wilder wamuangalie sana huyu atakuja kuwasumbua miaka2-3 ijayo
Screenshot_20190720-085032_1563604181536.jpeg
 
screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
9,726
2,000
Oscar Rivaz, this man is tough. Dillian Whyte inabidi awe very careful, lasivyo anaweza akazimishwa ndoto yake ya kupigania mkanda wa WBC
Screenshot_20190720-085440_1563603930855.jpeg
 
mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
5,781
2,000
Unajua katika michezo ambayo sielewi mpangilio wake Ni hii ya ndondi.
Sijajua huwa wanapangaje viwango vyao maana naona wote wanasifiwa kwa kuitwa heavy weight.
Kwa mfano bondia wetu Hassan Mwakinyo yupo kwenye viwango gani?
Je anaweza kupigana na bondia yeyote wa heavy weight duniani?
 
Heavyweight ni just weight class, haina mahusiano yoyote na ubora wa mpiganaji. Kama hao kina Man Pacquiao ni uzito mdogo 'welterweight' kama kilo sabini kasoro hivi, hao heavyweight wanaanzia kwenye kilo 95 hivi na kuendelea. Uzito una màana kubwa sana kwenye any combat sport, huwezi mpambanisha mtu mwenye kilo 60 na kilo 100, it's unfair na wangeruhusu hilo tungeshuhudia vifo vingi ulingoni. Mwakinyo wetu nadhani anapigana uzito wa super welterweight, karibu uzito sawa na kina Pacquiao
 
Kwa hyo kwa Sasa hivi ni mabondia gani wameshikilia nafasi za heavyweight duniani,maana Mimi kwa kutoelewa kwangu nilifikir kwamba kina Man Pacquiao ndio wapo viwango vya mwisho.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom