screpa
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 10,792
- 15,693
Kesho ni siku nzuri kwa wapenzi wa ndondi, dunia itashuhudia mapambano ya kuvutia kati na 'Legend' aliyegoma kustaafu Senator Man Pacquiao kutoka ufilipino dhidi ya bingwa anayeshikilia mkanda wa WBA (welterweight) kutoka Marekani Keith 'OneTime' Thurman ambaye hajawahi kupigwa. Keith Thurman katika press conference alinukuliwa akisema anamuheshimu sana Pac kama legend na amefurahi kupata nafasi ya kushea naye ulingo though "don't be surprised if Man Pacquiao goes nite nite", akimaanisha tusishngae kumuona Pac akilamba sakafu. Pambano hilo litafanyika Marekani MGM Grand kesho alfajiri.
Vilevile siku ya kesho dunia itashuhudia pambano jingine la kuvutia la uzito wa juu kati ya Dillian Whyte kutoka Uingereza dhidi ya Oscar Rivaz kutoka Columbia. Pambano hilo linatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na mabondia wote kuwa na rekodi nzuri, Wote wamecheza mapambano 26, Whyte akipoteza moja dhidi ya AJ, kwa upande wa Rivaz hajawahi kupoteza. Pambano hilo ni la muhimu sana kwa Dillian Whyte kwani akishinda litampatia tiketi moja kwa moja ya kupigania mkanda wa WBC , ambapo atasubiria mshindi wa pambano la Wilder vs Fury litakalofanyika February mwakani. Pambano hili litafanyika London Uingereza usiku wa kuamkia kesho.