Muda umefika sasa wa kumpata Undisputed Champion

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,415
21,110
Hii title ya Undisputed Champion kiuhalisia sidhani kama kuna bondia yeyote alishawahi kuipata.

Undisputed Champion ni yule bondia anayemiliki mikanda yote mikubwa zaidi kidunia ambayo kiidadi ipo minne ambayo ni WBC, WBA, WBO na IBF.

Mabondia wengi huishia kumiliki mikanda miwili au mitatu kati ya hiyo mikanda minne hivyo huishia kupata title ya Unified Champion.

Unified Champion ni yule bondia anayemiliki mikanda miwili au zaidi miongoni mwa mikanda hiyo minne (WBC, WBA, WBO na IBF) .

Mabondia wengi hushindwa kumiliki mikanda yote minne kwa sababu wengi hubadili uzito mara kwa mara (MF kutoka feather weight mpaka bantamweight,middle weight nk) .

Floyd isingekuwa kubadili uzito mara kwa mara ili apate mpinzani bora zaidi ili aingize pesa nyingi zaidi angekuwa tayari ameshapata hiyo Title ya Undisputed zamani sana kwa sababu title ya unified champion ameipata mara nyingi sana kwenye uzito tofauti tofauti ambao alikuwa anapigana (5 Weight Division), mpaka pambano lake na Manny Pacquiao ,Floyd alifanikiwa kumiliki mikanda mitatu (WBC,WBA na WBO )miongoni mwa hiyo minne hivyo alibakisha mmoja tu (IBF)ili kuwa Undisputed Champion ,


Sasa tukija upande wa heavyweight tunamuona bondia Anthony Oluwafemi Olaseni Joshua ukipenda muite Femi Boy au kwa kifupi AJ kama anavyojulikana na wengi, AJ anamiliki mikanda mitatu ambayo ni WBA,WBO na IBF hana mkanda mmoja tu ambao ni WBC ili akamilishe mikanda minne ili title ya Undisputed Champion.

Mkanda huo wa WBC unamilikiwa na Lineal Champion ambaye ni Tyson Fury ambaye amerudisha title hiyo ya U lineal baada ya kumtwanga bondia Deontay Wilder ,huku AJ yeye akiwa na title ya Unified Champion.

Kwa hiyo kitaalamu pambano tutasema Unified Champion vs Lineal Champion mshindi atakayepatikana atapata title ya Undisputed Champion.

Bondia AJ amekuwa akimkimbia Wilder mara kwa mara, alikuwa anasubiri tu Wilder apoteze pambano ili bondia atakayempiga Wilder apambane naye yeye na si yeye kumface Wilder moja kwa moja.

Hili limedhihirika baada ya pambano la pili kati ya Wilder na Tyson Furry ambapo Tyson aliibuka kidedea, team AJ wakiongozwa na promota wao Eddie Hearn walikuwa haraka sana kuhitaji pambano jambo ambalo halikuwa kawaida hapo mwanzoni.

Tyson Furry alituma kama ujumbe hivi kwenda team AJ baada ya kuonekana akitafuna Sticker yenye logo ya nchi ya Nigeria ambayo ndiyo asili ya Anthony Joshua kabla ya kubadili uraia.


Lakini mpaka sasa bado kuna sintofahamu katika pande zote mbili.

Kwa upande wa AJ, WBO waliagiza Alexander Usyka awe Mandatory Challenger dhidi yake baada ya Usyka ambaye ni bingwa wa WBO uzito wa Cruiserweight kuamua kupanda mpaka Heavyweight baada ya kumtwanga kwa Knockout swahiba wa Anthony Joshua ambaye ni Anthony Bellew.

Huyu bondia Anthony Bellew alishawahi kuwa trainer wa muda wa bondia Hassan Mwakinyo kwenye pambano lake lililofanyika Kenya chini ya udhamini wa Sportpesa.

Kwa upande wa Tyson Fury (Gypsy King) yeye mpaka sasa hajajulikana atapambana na nani maana kabla ya pambano ,WBC walitoa amri kwa bingwa atakayepatikana kwenye pambano lao atapambana na Mandatory Challenger ambaye ni Dillian Whyte.

Mbali na hilo, Deontay Wilder pia ameomba marudiano ya pambano la tatu (Trilogy Fight) jambo ambalo linauwezekano mkubwa kutokea kwa sababu promota wa Tyson Furry ambaye ni Bob Arum alifungua milango ya maombi kwa Team Wilder ndani ya siku 30 kama bado anahitaji
marudiano.

Bila kusahau huyu Bob Arum alishawahi kuwa promota wa Floyd Mayweather,Floyd alipomfukuza kazi na kuamua kusimamia mwenyewe mapambano yake,Bob Arum alienda kuwa promota wa Manny Pacquiao.

Floyd aliwahi kumshawishi Pacquiao amfukuze kazi Bob Arum kisha ajisimamie mwenyewe mapambano yake ili atengeneze pesa zaidi la sivyo ataendelea kunyonywa tu na Bob Arum.





usykaa_20200225_1.jpeg
dillianwhyte_20200225_3.jpeg
boxingwise_20200225_2.jpeg
1582408023971.jpeg
 
Mimi hiyo lineal tittle ndo huwa inanichanganyaga kabisa, unaweza nifafanulia kidogo? Maana Fury amekuwa akijimwambafy nayo mda mrefu

Sent using Jamii Forums mobile app
U lineal title unapatikana baada ya kumpiga mtu mwenye hiyo title.

Mwanzoni kabisa yule Lineal Champion huchaguliwa kwa kuangalia idadi ya titles ambazo anazo kisha mabondia wengine watakaofuata watakuwa nao ma lineal champions kwa kumpiga mwenye hiyo title.

Tuchukulie mfano, kwa heavyweight AJ ndiye mwenye titles nyingi hivyo kama kungekuwa hakuna title ya u lineal halafu tunataka kuanzisha tungempa Joshua,kisha mabondia wanaofuata wangekuwa ma lineal kwa kumpiga Joshua.

Labda bondia A akapigana na Joshua na akashinda huyu bondia tutampa title ya U lineal, baadaye akatokea bondia B na akamtandika bondia A then huyu bondia B ndiye atakayejulikana kama Lineal hali kadhalika angetokea bondia C akamtandika bondia B huyu C angekuwa Lineal.

Bondia atapoteza U lineal Champion kama tu atapigwa na bondia katika uzito huo huo alioupata hiyo title, mfano bondia akipata title ya U lineal kwenye U middle weight then akapanda mpaka heavyweight kisha akatandikwa, huyu bondia atabaki kuwa Lineal Champion kwenye middleweight division licha ya kwamba ametandikwa baada ya kupigana katika uzito tofauti.

Tuchukulie mfano Mikey Garcia alipanda uzito ili apigane na Errol Spence na alipigwa, kama ingekuwa ana title ya U lineal bado angetambulika kama Lineal Champion Katika uzito wake wa awali.

Bondia atapoteza title ya U lineal kama tu atashindwa kurudi uzito wake wa zamani ili atetee hiyo title, hivyo hiyo title itabaki kuwa Vacant na watachaguliwa mabondia wenye vigezo watambana kisha mshindi atapewa hiyo title.


Njia nyingine ni pale bondia atakapostafu masumbwi hali ya kuwa bado ni Lineal Champion ,mfano Rocky Marciano alistafu akiwa bado lineal champion hivyo wakachagua mabondia wengine waweze kuchukua hiyo title.


Tukija kwa upande wa Tyson Fury, yeye alitambulika kama Lineal Champion baada ya kumtandika Lineal Champion kwa kipindi hicho ambaye ni Wladmir Klistchko.


Tyson Fury bado aliendelea kuwa Lineal Champion maana hakuwahi kupigwa na yeyote tangu apate hiyo title ,pia hakustafu kupigana.

Kama ingetokea Deontay Wilder angempiga Tyson Fury, basi Deontay angetambulika kama New Lineal Champion.

Vile vile kama AJ atafanikiwa kumpiga Tyson Fury, basi atatambulika kama New Lineal Champion,pia atatambulika kama Undisputed Champion maana atakuwa amekamilisha mikanda yote minne.
 
Hance una uwezo mkubwa sana huku kwenye masumbwi, unaweza hata kuandaa document ukapata air time baadhi ya vituo vya radio,
Kiukweli wachambuzi wa masumbwi ni wachache mno sana sana tunamtegemea Yasin Abdallah, yule jamaa anajua sana
Usikalie kipaji Hance, achana na mambo ya udaku kaza huku kwenye masumbwi

Sent using Jamii Forums mobile app
Pamoja sana mkuu
 
Nice post

Kwanini AJ alikuwa anamkimbia wilder?
Not really sure but kuna reliable source niliwahi kuisoma inahusu boxing sana.. Na sababu kuu kwanini AJ anamkimbia Wilder ni masuala ya kibiashara zaid yaani kwamba, kambi ya team Wilder wanataka kukiwa na pambano wote wagawane 50% 50% kitu ambacho upande wa AJ hawaez kukubal na hawajah kukubal(rejea lile pambano la Aj vs Ruiz) uone upande wa AJ walvochukua percentage kubwa sana ya pesa
 
Bernard Hopkins Vipi?
Lennox Lewis alikaribia na kuitwa undisputed wakati ulee

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Asante nimekupata vyema kuhusu Lineal Champion, ila nachoshangaa Fury alikaa nje ya ulingo kwa takribani miaka mitatu, sasa ilikuwaje hawakumvua hiyo status, mbona mikanda walimpokonya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..I predicted Tyson in 6 cos he's the bigger man and a better boxer..but in losing I saw that wilder is a much better boxer than many think.. anyone who knows an athlete could see that by round 4 he was going back to corner cussing himself cos something in his arsenal wasn't working..speed reflexes balance .his own body was letting him down..fury saw that. but he..an empathy..didn't want to kill the guy..they love each other..wilder the warrior would have.ike he said..gone out on his shield!!..would love to see it again..may be very different from the first 2 I think!!!..imho..


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom