jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,989
- 22,521
Kwahiyo mkulu cheo alipewa na Mwinyi kwasababu ya dini?maana alimteuwa kwenye madini na nishati na wakati hajasomea fani hiyo!Same way huko chadema kuna wanaopiga kelele hizo za watu kupewa madaraka kwasababu ya dini,JK style.Mwinyi akiwa rais, siku moja alimuaigiza malecela kuwa anataka kuona viongozi wapya wenye asili ya kiisilamu wakipewa nafasi za uongozi, muungwana wakati huu alikuwa Tunduru, ambako alikuwa amepewa adhabu ya kwenda huko na bosi wake CCM Dododma, Mwakawago aliyekuwa akimchukia sana,
katika uho mkumbo malecela aliwapromote, Dr. Mtulia, Makamba, na muungwana kuja kuwa waziri mdogo.
Alizaliwa Oktoba 7, mwaka 1950 katika kijiji cha Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Elimu.
1958-1961 - Shule ya Msingi Msoga
1962-1965 - Shule ya Msingi ya Kati ya Lugoba
1966-1969 - Shule Sekondari Kibaha
1970-1971 - Shule ya Sekondari Tanga
1972-1975 - Chuo Kiku cha Dar es Salaam, Shahada ya kwanza ya Uchumi
1976-1977 - Mafunzo ya Afisa wa Jeshi / Uongozi wa Jeshi, Monduli
1983-1984 - Mafunzo ya Makamanda wa Jeshi
Nafasi alizowahi kushika
1975-1977 - Katibu msaidizi wa TANU wa Mkoa
1977-1980 - Katibu Msaidizi wa CCM, Kisiwani Zanzibar
1980-1981 - Afisa Utumishi wa CCM makao makuu
1981-1983 - Katibu wa CCM Mkoa Tabora
1983-1986 - Mkufunzi wa Siasa katika Chuo cha uongozi wa Jeshi Monduli
1986-1988 - Katibu wa CCM Wilaya ya Nachingwea na baadaye Masasi
1988-1990 - Naibu Waziri wa Nishati na Madini
1990-1994 - Waziri wa Nishati, Madini na Maendeleo ya Maji