Ndomba kumrithi Hosea very soon | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndomba kumrithi Hosea very soon

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NgomaNzito, Sep 9, 2008.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2008
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Heshima mbele wakuu

  Taarifa zilizotoka hivi punde kutoka kwenye mitambo na nzi wetu wamekamata kwenye antena zao zinasema muda si mrefu mkulu atampiga chini Bw.Hosea wa takukuru na kumweka Mjeshi Ndomba aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha na baadae Mkulu kumrudisha jeshini ili kuweka nidhamu ya jeshi juu. Hapa tutaambiwa Hosea anastaafu lakini umri bado Mhh!!!!. Pia wale tunaowapigia kelele sana hapa Jf kama Mwanyika na mwenzie Mgonjwa watapigwa chini tukipata dodoso tutaziwasilisha

  Nzito
   
 2. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mkuu wa Utumishi wa JWTZ, Brigedia Jenerali Samwel Ndomba, alipokua Mkuu wa Mkoa alikuwa Kanali na akarudishwa jeshini na kupandishwa cheo. Amekuwa akitajwa sana kumrithi Hosea.

  pamoja naye wametajwa pia kina Ali Siwa aliyekuwa TIS chini ya Cornel Apson na pia amekuwa akitajwa mama Lilian Mashaka, ambaye ametumia muda mwingi kumpiga vita bosi wake Hosea.

  JK na Lowassa ndio waliomponza Hosea na wakimuondoa bila kuwashughulikia mafisadi itakuwa hawajafanya kitu kwani kutatokea kina Lowassa wengine kina Hosea wengine wakafanya mambo yale yale.

  lakini kuna utetezi mmoja kwamba, wakati wa kuchunguza Richmond, Hosea na wenzake walitumia sheria ya zamani ya PCB ambayo ilikuwa na makosa manne tu ya rushwa na ilikuwa na vikwazo kibao.

  Kwa sheria hiyo ya mwaka 76 wasingeweza kushinda kesi dhidi ya wahusika wa Richmond. Kosa walilofanya ni kulazimishwa na kukubali kutangaza kwamba hakuna kesi kwa shinikizo la wanasiasa wakati kwa kawaida hata kama kesi ikiwa hakuna ushahidi kwa wakati huo, unaweza kufunga jalada na kulifufua pale ushahidi ama sheria zinapobadilika kuruhusu uchunguzi na uchukuaji hatua. Hosea na wenzake walijua sheria inabadilishwa lakini kwa kuwa wanasiasa na zaidi Lowassa alikuwa ni zaidi ya YEYOTE serikalini, Hosea alihitaji ujasiri wa pekee kuweza kumkatalia.
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Sep 9, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,098
  Trophy Points: 280
  ngoma-nzito,

  ..Brig.Gen.Ndomba kuleta mabadiliko ya maana kwasababu mafisadi karibu wote anaopaswa kuwashughulikia ni wateule wa Raisi Kikwete.

  ..zaidi, huko Jeshini Brig.Gen.Ndomba ameleta mabadiliko gani? maanake ni open-secret kwamba Jeshini nako kuna uchafu wa kila aina haswa ktk matumizi ya fedha na manunuzi.

  ..Col.Maftaha na Maj.Gen.Kamazima wametangulia huko PCCB kama Ma-Director. pamoja na "UJESHI" wao rushwa na ufisadi vilishamiri. now, what is so special na huyo Brig.Gen.Ndomba?

  ..RAISI WETU LT.COL.KIKWETE NI MJESHI VILEVILE. SASA NINI KIMEMZUIA KUPAMBANA NA RUSHWA? KWANINI TUMSUBIRI BRIG.GEN.NDOMBA KUPAMBANA NA RUSHWA?
   
 4. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Halisi nipenyezee jina langu huko. Nipo serious nitapambana nao hao jamaa kama yule mkurugenzi wa bandari ..nani vile.Samsoni mahiga au?
   
 5. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2008
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  JK tusimsifu sana na ujeshi wake. Jamaa kaakulia mtaani, jeshi halijui sawasawa. Alienda jeshi kisiasa tu.
   
 6. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ....Kwani wakuu hivi lazima mnene wa PCCB lazima awe mjeshi??? Mi kwa mtazamo wangu naona hawa wajeshi sijui wagambo wamechemsha kufanya kazi utadhani taasisi haiongozwi na mjeshi.....Na huyo Ndomba sijui kama atakuja na jipya...Tusubiri tuone!!!
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Sep 9, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,098
  Trophy Points: 280
  Kipanga,NgomaNzito,

  ..Raisi mwenye ni "Mjeshi" sasa ni nini kinachomshinda kupambana na Rushwa?

  ..kwanini tumtegee Brig.Gen.Ndomba kupambana na rushwa wakati tayari imemshinda Mjeshi mwenzake Amiri Jeshi Mkuu Lt.Col.Kikwete?

  Zero,

  ..wakati wa kampeni tuliambiwa kwamba Kikwete ni Mjeshi aliyebobea ktk masuala ya Uchumi.

  ..tukasubiri kwa hamu sana kuona matokeo ya utumishi wake kama Raisi.

  ..inaelekea aliomba kazi kwa kutumia sifa za uongo na kugushi.
   
 8. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2008
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Heshima yako NN.
  Hivi huyo Br.Gen. Ndomba karudisha nidhamu gani huko jeshini?
  Sababu tunajua rais wetu nae ni mjeshi(tena kanali) na hicho sio cheo kidogo!
  lakini tujiulize Rais amefanya nini kupambana na mafisadi na ufisadi?
  mimi naona hapa kinachofanyika ni kueana vyeo tu ili kuwafanya wadanganyika waamini kuwa serikali inatekeleza mapendekezo ya bunge.
  Suala la msingi hapa ni ateuliwe mtu muadilifu, jasiri na shupavu atakayeweza kupambana na ufisadi na mafisadi.
  Vinginevyo tutaendelea kuumizwa na ufisadi kwa mabadiliko ya safu ya PCCB yanayolenga kutupumbaza kumbe wanaendelea kupunga upepo.
  Hata hivyo kama kuna mtu anamfahamu vizuri Br.Gen. huyu, kama anaweza kweli kuudhibiti ufisadi basi tunaomba atutoe wasiwasi kwa kutuwekea hapa wasifu wake ili tujue PCCB sasa inakabidhiwa kwa Gen. wa ukweli au Gen. mwanasiasa.
   
 9. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2008
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Joka Kuu,

  Mchumi wa wapi? Tatizo uliukalia ukatibu wa wilaya wa chama kwa muda murefu mno tena akiwa wilaya za vijijini. Nafikiri uchumi ulishamtoka siku nyingi sana. Sasa anatumia umaarufu sijui hata alikoupatia. May be Baby Face!!!!!!!!!!
   
 10. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ...Kwiiii kwi kwiiiiiii..Mnatafuta warembo???
   
 11. M

  Masatu JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  FairPlayer I think u mean Samson Luhigo. He was the most corrupt DG THA now (TPA) ever had.

  Dredging Dar channel, ununuzi wa cranes mbovu, mkataba wa upanuzi wa bandari za Mtwara na Tanga, the list is endless....
   
 12. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2008
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na wewe kabisa wanajeshi ni wengi kwenye system ukiawaacha akina makamba na wengine kuna wanajeshi wengine wenye uchungu na nchi hii kama tulivyo sisi hao wanatakiwa (wajitokeze) labda kupigania nchi yetu
   
 13. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #13
  Sep 9, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280

  ..huyu ndomba hana lolote zaidi ya urafiki na jk...na hata huko jeshini hana jipya ...zaidi wanamuona raia tu!!!....kwani jk haoni nje ya marafiki zake..???

  .....ndomba huyu huyu ndie alitaka kumrusha awe CDF....next...kila kitu yeye...
   
 14. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #14
  Sep 9, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280

  ..hadi kuja kuibuliwa mwaka 1990...jk alikuwa akipanda baiskeli tu kama katibu wa chama wilaya newala...akitumia muda mrefu kufukuzia kinamama kwenye ma tembe ya udongo....offcourse ndiko alipompta mwalimu wa UPE ..salma...huo uchumi ka practice lini????

  ...hiyo ndoto ya urais ilimpata ghafla....pamoja na kujifanya ni moja ya watu waliokuwa karibu na mwalimu ...si kweli..kwani mwalimu asingemuacha kwenye cheo kidogo kwa miaka yote hiyo..hadi warioba alipomleta mjini kwa mwinyi..baada ya kumkuta kule kwenye mafuriko ya elnino....sana sana ukaribu na mwalimu ni kipindi akiwa foregn wakati wa burundi peace...ukweli jamaa ni smart kwenye kutumia opportunity....
   
 15. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #15
  Sep 9, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Huwa kuna wakati Wakenya wanamsema JK kuwa ni Opportunist.Mimihuwa nawapinga sana hadi natokajasho lakini mimi kwa kweli najua huyu mkuu ni opportunist aliyeshindikana,yaani we acha tu.


  Huo Uchumi wake hata yeye mbona hauamini? Active foreign minister.Kwi kwi kwi
   
 16. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #16
  Sep 9, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Presidential dream inatokea kama uyoga,it's pathetic.
   
 17. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #17
  Sep 9, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Lakini nadhani kabla ya kuwa Waziri mdogo, Kikwete alishashika nafasi muhimu za uongozi kwenye Chama na Jeshi. Kwa kuteuliwa kuwa Waziri mdogo hilo kwa kweli sina tatizo nalo.

  More from Wikipedia:

   
  Last edited: Jan 6, 2009
 18. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #18
  Sep 9, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Kama uwezo wake wa sasa ndio huo pamoja na improvement alizofanya,sijui kwenye vyeo hivyo vya chini ilikuwaje?
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Sep 9, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,098
  Trophy Points: 280
  Kuhani,

  ..katika kazi zote alizofanya kabla ha-serve kwa muda mfupi pale Wizara ya Fedha sioni yoyote ile inayohusiana na uchumi.

  ..alipokuwa wizara za fedha na mambo ya nchi minongono ilikuwa haiishi kwamba alikuwa kama kivuli tu, lakini defacto Ministers walikuwa wengine ambao sitaki kuwataja hapa.

  ..sasa huyu Kikwete tukimuita Mjeshi, Brig.Gen.Hassani Ngwilizi tutamuita nani?
   
 20. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #20
  Sep 9, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  I doubt kuhusu Ali siwa bcoz tetesi ni kwamba huyu jamaa na JK picha hazipandi kabisa,kisa mchakato wa mgombea urais wa ccm 2005
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...