Wont be the same
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,564
- 2,483
Waziri kivuli wa ofisi ya waziri mkuu- bunge, Sera, vijana, kazi na ajira, Kutokea ACT Wazalendo, Ndolezi Petro kupitia ukurasa wake wa X ameandika kuwa uamuzi uliotolewa na Mwenyekiti wa Chadema Ubungo wa kuwazuia wananchi kujiandikikisha kwenye daftari la uchaguzi kuwa ni kampeni ya hovyo ya CDM kuwahi kutokea.
===
Taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa kichama Ubungo
“Nape yalimtoka yaliyokuwa moyoni akizungumza kwamba kushinda inategemea nani anayetangaza yule ni kijana wa kwenye chama kile kwa muda mwingi sana kwa hiyo kwa vyovyote ni vyema tukamsikiliza. Ikiwa hivyo kwamba mapenzi ya yule anayetanganza ndiyo uamuzi, wananchi wana haja gani ya kuja kujiandikisha na sasa tunawaambia kwamba zoezi la kujiandikisha kupiga kura kwa mkoa wa Dar Es Salaam wanatakiwa waanze kesho ili iweje wajiandikishe waende kwenye zoezi ambalo kwa hakika kura zao hazitaheshimiwa. Na ndiyo maana katika vikao vyetu tulivyofanya kwa siku za karibuni tumedhamiria dhahiri kwamba hatutatoa ushirikiano kwenye suala hili la uandikishaji wa wapiga kura, wanachama wetu na ndugu zetu hatuna sababu ya kupoteza muda kwenda kwenye daftari ambalo hilo daftari lenyewe tunataka hilo daftari lenyewe lifanyiwe mabadiliko.
“Tunaposema Reforms ni pamoja na hilo daftari uchaguzi liweze kufumuliwa liweze kuandikishwa upya. Msimamo wa chama chetu ni kuhakikisha kwamba lile daftari la wapiga kura watu sahihi waliopo kule ndani waandikishwe lakini pili tuwe na uwezo wa kulifikia daftari hilo bila mizengwe.” Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Mkoa wa Kichama wa Ubungo Amos Maziku.
Source: Jambo TV
Soma pia: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze