Ndoa zimekuwa sio za mvuto tena

chongoe

JF-Expert Member
Mar 22, 2019
1,128
2,717
Habari zenu waungwana siku hizi ndoa imekuwa sio kitu cha mvuto sana sababu wazazi wa muolewa wanafanya mtaji binti yao utakuta anaenda kuposa sehem mahari anayotozwa ukitoa atachopewa bi harusi pesa iliobaki ndio inayofanya shughuli kama chakula na mengineyo.

Utakuta binti baada ya kupata mahari na kununua kitanda na godoro anaanza dharau ndani ya nyumba kwakuwa anajua akiachwa kwakuwa ana kitanda na godoro anajua ataweza maisha ndio maana siku hizi kuachana imekuwa kawaida kwakuwa hata wazazi hawana uchungu na ndoa iliofanyika ya binti yao wanajua gharama zote zimetokana na mahari.

Mwisho namalizi natoa angalizo kwa wanaume wenzangu:

HAKUNA SHIMO LINALOJICHIMBA WENYEWE KILA SHIMO LINA MCHIMBAJI WAKE SASA WEWE JIFANYE MJUZI KULETA UREMBO KWENYE SHIMO HATA MCHIMBAJI HUMJUI KUWA MUANGALIFU
 
Wazazi wanakamua na kutaka kumaliza shida zao zote kupitia Bride Price, wanasahau kabisa kuwa kuna maisha mengine baada ya ndoa.
 
mahari milioni moja, halafu ndoa haidumu,si bora kubeba bure maisha yaendelee, ya nini kumtia hasara kijana wa watu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom