Sababu za uvunjifu wa ndoa na muarubaini wake

Jul 20, 2021
5
13
CHANZO CHA UVUNJIFU WA NDOA NA MUARUBAINI WAKE.

Katika mambo yanayowadumbua watafiti mpaka leo hii ni suala la kuvunjika kwa ndoa makundi kwa makundi.

Kipindi Cha nyuma enzi za mababu zetu ilukuwa jambo la kustaajabisha kumuona mtu kamtaliki mkewe na kuibua maswali mengi bila majibu, lakini katika jamii yetu leo imekuwa kama fahari wanandoa kuachana.

Watafiti mbalimbali wamejaribu kuchunguza suala hili lakini bado wameshindwa kupata jibu kamili haswa ni kwanini siku hizi talaka imekuwa kama 'fashion'.

Sababu nyingi zimekuwa zikihusishwa na mkasa huu lakini sababu kuu haswa bado haijajulikana. Wapo wanaosema mmonyoko wa maadili, au maendeleo ya sayansi na teknolojia au ukosefu wa elimu ya ndoa nakadhalka. Yote haya yanachangia kuvunjika kwa ndoa lakini ipi haswa ndiyo chanzo kikubwa bado ni kitendawili.

Tukianza na hoja kuwa uvunjifu wa ndoa ni matokeo ya mmomonyoko wa maadili suali litakuja ni nini kimepelekea mmomonyoko huo? lini ulitokea na kivipi? Hapa unaweza kujiuliza msururu wa maswali bila majibu.

Tukija kwenye hoja ya ukosefu wa elimu ya ndoa swali litakuja kwani zamani kulikuwa na vyuo vya ndoa na sasa hivi havipo? Kwanini siku hizi tunashuhudia talaka hata kwa makungwi wenyewe wanaotoa hiyo elimu kuhusu ndoa?. Kiufupi hoja hii bado haina mashiko katika muktadha huu.

Sababu zinazotajwa kuhusu kuvunjika kwa ndoa ni nyingi sana ila tunachokitaka hasa ni ile kubwa, kwa mfano unapozungumzia sababu za kuja kwa wakoloni Afrika unaweza kutaja sababu nyingi sana lakini kubwa kabisa ni "Industrial Revolution", kwahiyo hizo nyingine ni 'minor causes'.

Tuje kwenye hoja ya msingi, kwanza kwakuwa lengo letu ni kupata chanzo kikuu cha kuvunjika kwa ndoa inatubidi tupige picha maisha ya Babu zetu kisha picha hiyohiyo tuilete katika jamii yetu ya sasa af tulinganishe.

Tuanze kwenye lengo la ndoa na maana yake enzi hizo, mababu zetu waliifasiri ndoa kama hatua muhimu katika maisha ya mwanadamu na sehemu ya kuunganisha undugu. Aidha lengo kuu la ndoa kwa wakati ule ilikuwa kukuza familia na kusaidiana katika shughuli mbalimbali.

Tukija katika jamii yetu ya leo ndoa hufasiriwa kwa namna mbili, kwa upande wa mwanamke huhisi ndoa ni sehemu ya kujinufaisha kiuchumi na kuleta maendeleo katika familia yake ndiyo maana hata kwenye mahari wazazi hutaja kubwa wakihisi hiyo ni sehemu ya kujipatia kipato, aidha kwa upande wa mwanaume huiona ndoa kama sehemu ya kujitosheleza matamanio yake tu basi hivyo akipata alichokusudia basi si muhali kwake kumuacha aliyemuoa.

Tukija kwenye maisha ya ndoa, mababu zetu waliishi kwa mapenzi makubwa na kustahamiliana katika shida kwani waliamini ni sehemu ya maisha. Katika ndoa nyingi za siku hizi wanandoa huhisi kuwa siku zote za ndoa ni furaha na amani ndiyo maana shida zikianza kidogoa aidha mwanaume atatelekeza mwanamke au mke ataanza kudai talaka.

Muarubaini wa yote haya upo katika njia tofauti tofauti mfano wanandoa kuwa wavumilivu, kuishi katika uhalisia, kufumbia macho baadhi ya madhaifu na kufuata misingi ya dini kwani ndiyo nguzo kuu ya maadili
 
Back
Top Bottom