MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,588
...asante mwj1....
...unapozungumzia changes una maanisha nini? kwa muono wako, wadhani mabadiliko haya yameanza lini kiasi cha kulinganisha uzamani wa wazazi wetu na huu usasa wa kikwetu?
...mtazamo wangu wa ndoa za kisasa nalinganisha waliooana 1980's kuja mpaka leo hii 2011....kasi ya watu kuoana na kuachana imekuwa kubwa kulikoni wazee wetu waliokuwa wameoana miaka ya 60's na kurudi nyuma...au?
Kuhusu Upendo:
Kwa mtazamo wangu mie haya mapenzi ya "Egoli" tuliyoyaiga toka kwa wazungu yamechangia kwa kiasi kikubwa udhaifu katika ndoa nyingi za siku hizi. Hii kujidai unataka kufall in love ndo uoe/olewe imetupelekea kuiumbia na kuikubali counterprt ya falling in love ambayo ni falling out of love. Siku hizi si jambo la kushangaza kujikuta unaitwa kwenye kusuluhoisha ndoa ambayo mmoja wa wanandoa hao alilala tu usiku na kuamka asubuhi akiwa ameshafall out of love na sasa anadai talaka au anataka kuvunja ndoa. Na ajabu sana kuna kila aina ya justification ya hii falling out of love ambayo mwisho wa siku tunalazimika kukubaliana na muota ndoto huyo.
Wazee wetu wa zamani hawakuwaga na falling in love bali walikuwa na Growing in love...it just keep on growing hakuna kufall out na ndio maana walikuwa wavumilivu. Kwa kuwa unaishi kwenye ndoa ambayo kadri siku ziendavyo love inajijenga, kukua na kukomaa hata ukifanyiwa kosa gani wewe unajihisi kumpenda zaidi ingawa kwa manung'uniko kwa ndani! Ndoa za siku hizi kwa kadri unavyokosea mwenzio ndivyo anavyoendelea kuizungusha door knob ya love na mwisho anaufunguua na baaam amefall out.
Samahani imekuwa ndefu.
Mbu tatizo ni kwamba watu tu hodari waku-exaggerate mambo. Haki za wanawake hazisimami kupingana na majadiliano ndani ya ndoa. Huo ukandamizaji unaoongelea unatokana na mwanaume kutaka kuwa mwamuzi juu ya maisha ya mwanamke badala ya kumfanya rafiki/partner wake, mtu wa kushauriana na kujadiliana mpaka kufikia muafaka kwenye kila jambo.
Hata kumtaka mtu abadili alichovaa kunaweza kuwa ukandamizaji iwapo unamuORDER kama mtoto, badala ya kumshawishi kwa kumueleza na kumuelewesha sababu ya wewe kutaka afanye hivyo. Ndoa/mahusiano yoyote ambayo mmoja (mke au mume) anataka awe mtu wa kusema tu "FANYA HIVI, FANYA VILE" na kutegemea "NDIO MZEE" toka kwa mwenzake lazima yawe na matatizo.Na hapa ndipo nnapokubaliana na FF kwamba haitakiwi mmoja amuoe mwenzake bali inatakiwa muoane. Muwe marafiki na wapenzi, sio mmoja awe boss wa mwenzake.
Sasa mkwe kama zamani kupendana kulikua kunakuja baadae huo upendo wa dhati walikua wanaangalia vipi kabla ya kukubali/amua kuoana?ndoa za zamani walikuwa hawafahamiani wala kujuana lakini walijifunza kupendana na waliweza kuhimili lolote katika ndoa kwa uvumilivu na upendo wa dhati....za sasa imekuwa kama fasheni mtu anaolewa kuondoa aibu kwenye familia...unaweza kuta msichana anampenda mvulana lakini mvulana sio sana inabidi kuoa kwa huruma fulani vivyo hivyo kwa mvulana anapenda sana bi dada anakubali kwa vile asionekana mbaya au baada kukosa wa kumwoa.... pia wengine wanaoana umri unakwenda bora lolote au jamaa maisha yanalipa. kwa jumla maisha ya ndoa za sasa yanaangalia vitu na sio upendo wa dhati
Ndoa za kisasa hazidumu kwa sababu watu wanaoana kwasababu zingine ukiacha sababu za kidini na upendo baina yao. Wanandoa wengi wa sasa hawana hofu ya mungu wala hawafati mila na desturi zao ambazo kwa namna moja au nyingine zingewasaidia kuwaweka pamoja.
weman right = women rights
ndoa za zamani walikuwa hawafahamiani wala kujuana lakini walijifunza kupendana na waliweza kuhimili lolote katika ndoa kwa uvumilivu na upendo wa dhati....za sasa imekuwa kama fasheni mtu anaolewa kuondoa aibu kwenye familia...unaweza kuta msichana anampenda mvulana lakini mvulana sio sana inabidi kuoa kwa huruma fulani vivyo hivyo kwa mvulana anapenda sana bi dada anakubali kwa vile asionekana mbaya au baada kukosa wa kumwoa.... pia wengine wanaoana umri unakwenda bora lolote au jamaa maisha yanalipa. kwa jumla maisha ya ndoa za sasa yanaangalia vitu na sio upendo wa dhati
Samahani Lizzy,
Ndoa ni ya watu wawili kwa hiyo hatuwezi kusema kuwa matatizo ya ndoa yanasababishwa na wanaume peke yao.
Labda kama nimekuelewa vibaya!!
Inabidi na walimu wote wa kike mashuleni WAFUKUZWE.Nionavyo mimi.......Haki za wanawake ni tatizo,ni tatizo coz wanawake wanachohitaji ni kuwa SAWA na wanaume.Mwanaume anaweza kuwa ana makosa lakini haya makosa yaangaliwe kimtazamo wa kimaandiko zaidi,na hayo makosa ya mwanaume yatazamwe kimaandiko!Mfano maandiko yamekataza mwanamke KUMTAWALA mwanaume,pia yamekataza KUMFUMDISHA mwanaume na hizi ni moja ya "haki" anazozipigania mwanamke,kwenye ndoa haiwezekani kila kitu kikafanywa na kila mwanandoa,yapo ya mwanamke yapo ya mwanaume,vurugu za usawa ndo chanzo cha talaka nyingi,matokeo yake watoto wanakosa malezi tunapata matokeo ya tabia nyingine za kijinga na za ajabu!
Sasa mkwe kama zamani kupendana kulikua kunakuja baadae huo upendo wa dhati walikua wanaangalia vipi kabla ya kukubali/amua kuoana?
Sasa mkwe kama zamani kupendana kulikua kunakuja baadae huo upendo wa dhati walikua wanaangalia vipi kabla ya kukubali/amua kuoana?
Inabidi na walimu wote wa kike mashuleni WAFUKUZWE.
Sasa kama inaweza kuanzia popote kwanini unaona kwamba wanaoanza kwa kupendana wanakosea/ndio sababu ya ndoa kutokudumu?Niliwahi kuelezea kitabu kimoja ambacho kinajadili haya mambo ya muhimu kwenye ndoa (marriage triangle...love, sex and living together) wapi pa kuanzia...Which to me, nakubaliana na mwandishi kwamba unaweza kuanza na lolote. Kama unajitambua, hakuna shaka kwamba ndoa yako itakuwa imara!!
Hebu chungulia hapa,
http://www.amazon.com/I-Married-You-Walter-Trobisch/dp/0966396669
Upendo unafundishwa kwenye familia,ndoa ni uamuzi sio upendo,ukijua kupenda haitakua kazi kuanzisha familia na YOYOTE kwani unakua umempenda tayari!Umempenda coz kigezo cha kupenda ni huyo awe binadam na sio awe na hela au mrefu au miguu ya bia au mtanashati!