Ndoa za watu ziheshimiwe

JOMAM

JF-Expert Member
Aug 6, 2012
330
139
Naamini mko poa,

Watu wengi tunapata matatizo na hatujui sababu ya matatizo tunayoyapata.

Mara nyingi zinaweza kuwepo sababu mbalimbali ila kuna jambo naona liko sana humu na nahisi ni laana tunayoitengeneza au tuliokwisha itengeneza.

Kwanini tunaona sifa kutembea na wake za watu au waume za watu? Naona thread nyingi hapa watu wanajisifu kwa kuvunja nyumba za watu.

Pamekuwepo mikasa mingi ya vifo vinavyotokana na wivu wa mapenzi. Hivi hii damu mbona tunaiona kawaida? Sisemi msizini nitakuwa napoteza muda hapa, ila heshimuni ndoa za watu.

Ndoa ni zaidi ya mahusiano ya sex, kuna malezi ya watoto pale na makuzi mengine.

Hivi unajisikia vipi mtu anapokuja anakwambia huyu si baba yako, na anakuonyesha jamaa uliyekuwa unamchukia ndio baba?

Mwisho, siwazuii msizini ila epukeni kutembea na wake za watu, watoto wa shule na kuandika thread zinazovunja maadili ya jamii.

Muwe na uzinzi mwema. Msisahau ni jukumu letu kuilinda au kuibomoa jamii yetu.
 
Umeongea ukweli mkuu.

Lakini wanandoa ndio wanahaki ya kulinda ndoa zao kwanza kabla ya watu wengine.

Wao wajitahid wajiheshimu, wamalize matatizo yao ndani kabla hawajatoa nje na wapunguze kusema udhaifu wa ndoa zao kwa watu wa nje.

Wao wakiheshimu ndoa zao hakuna ambae atavunja ndoa ya mtu.
 
Keshatendwa huyu.

Wake za watu wengine wanataka wao,anakufanyia majaribu unakosa namna unamnaniliu!!😎
Pia waambie na wenye wake zao wawale vizuri.
 
Umeongea ukweli mkuu.

Lakini wanandoa ndio wanahaki ya kulinda ndoa zao kwanza kabla ya watu wengine.

Wao wajitahid wajiheshimu, wamalize matatizo yao ndani kabla hawajatoa nje na wapunguze kusema udhaifu wa ndoa zao kwa watu wa nje.

Wao wakiheshimu ndoa zao hakuna ambae atavunja ndoa ya mtu.
Ni kweli usemalo ila me nachopinga ni swala la mtu kuja kujivunia hapa kama ni jambo jema, hapa wanaingia mpaka wadogo zetu sana kiumri wanajifunza nini?
Watafikiri ni sifa kukaa unatembea na waume na wake za watu mpaka siku vinamtokea puani!
 
Keshatendwa huyu..
Wake za watu wengine wanataka wao,anakufanyia majaribu unakosa namna unamnaniliu!!😎
Pia waambie na wenye wake zao wawale vizuri.
Sina shaka na uaminifu wa mke wangu! Walau sijaona tatizo wala hajanionyesha usaliti wowote, ila naamini watu wanaokumbwa na fedhea hii hupitia maumivu sana, niliona mwaka Fulani moja ya balozi kwenye mtaa mmoja alikatwa na shoka kwa wivu wa mapenzi! Watu wamepigana risasi,wamepeana sumu na mikasa mingi. Kwakua hii jamii ni yetu sote tunapaswa kukemea uvunjifu wa ndoa,usaliti,mapenzi ya jinsia moja, na mapenzi ya kinyume na maumbile kwa manufaa ya jamii yetu
 
Back
Top Bottom