Mapenzi mara zote huwa yanaisha au kufifia baada ya muda fulani na yanapoisha ndipo wanandoa wanaanza kukwaruzana sana na hatimaye kuachana. Kwa hiyo kufikiria kuishi na mtu maisha yako yote na ambaye mtaboana tu ni changamoto. Hii inaweza kuwa moja ya argument za ku-support ndoa za mikataba. Hata hivyo ndoa za mikataba zina madhara ambayo yatahitaji miaka zaidi ya hamsini kuyashughulikia. Nchi za Scandinavia ni mashahidi wa hili. Nusu ya wakazi wa Sweden, kwa mfano, ni wahamiaji. Sasa niliongea na rafiki yangu Mswidi akasema imebidi nchi iangalie upya sera ya ajira na uraia kwa sababu ilifika mahali ikajikuta haina nguvu kazi. Wazee walikuwa wengi kuliko vijana na watu wa kufanya kazi viwandani wakawa hakuna, ikabidi iwe inapokea wahamiaji na wakimbizi wengi ambao wangeziba gap hilo (ukienda maeneo kama ya Tensta ni kama upo Somalia vile). Hii inatokana na ukweli kwamba walichezea hii taasisi ya ndoa. Kuna haja gani ya kuzaa na mtu ambaye una uhakika mtaachana baada ya miezi 6 au mwaka mmoja? Waswidi waliendelea kuoana na kuachana bila kuzaana kwa kipindi kirefu toka waliporuhusu flexibility kubwa kwenye ndoa (Si unajua kule wamama wapo juu na hawataki kubanwa???), sasa mpaka kufikia mwaka 2007 kulikuwa na watu milioni 9 huku milioni 4.5 wakiwa wahamiaji na wengi wa waswidi original wakiwa wazee. Sasa hivi kule ukizaa mtoto serikali inalea mpaka university, kila kitu bure. Kwa maana nyingine mtoto ni wa serikali wewe ni chombo kilichotumika kumleta hapa duniani. Na wanasera za chinichini za kulazimisha wanandoa kukaa pamoja muda mrefu na kuwashawishi wazae watoto wengi (Watoto wengi unapata hela nyingi za malezi toka serikalini). Labda tupitishe ndoa za mikataba ili kupunguza idadi ya watu wanaotokana na kuzaliana. Tujifunze kwa wenzetu, tusichezee ndoa. Tuache sheria zetu za ndoa kama zilivyo kwa sasa.