Nimeoa mwaka huu. Ndugu wa mke wananjaa sana halafu uelewa wao katika maisha mdogo sana, kila tatizo wakipata kimbilio kwangu, na mimi maisha yamenibana sana siwezi kuwalea. Mke wangu hadi amechoka na anaogopa kuwaambia ukweli, jamani naombeni ushauri nifanyeje. Hali sio nzuri.
Umeoa Kigoma nini?
Maana hao jamaa hawakupi mke mpaka wahakikishe choo unachotumia kimejaa wanajua lishe ipo.
Hahaaaaa...bora angeoa mzunguTatizo la kuoa waswahili
Wekeni bango mlangoni HIKI SIO KITUO CHA MISAADA
Heee vunja ukimya kaka eh uzungumze nao! Heri lawama ya wazi,Kuliko UPENDo uliositirika
Tatizo la kuoa waswahili
Mradi mkeo nae ameliona hilo basi yeye ndio akawaeleze ndugu zake kwanza,mkiona hamna mabadiliko mtaongea pamoja as a family sasa kama wataendelea watakuwa wanawatafuta undani sasa!!!!
Mkewe atakuwa mnafiki...sidhani kama ndugu zangu wanakuwa kero nitashirikiana na mume wangu kuwashangaa badala ya kuchukua hatua...naye ni mule mule...Hiyo ni tabia ya familia.