Ndoa yangu iko hatarini, Ushauri unahitajika.

Ndoa yangu iko hatarini, Ushauri unahitajika.

MotoYaMbongo

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2008
Posts
2,146
Reaction score
887
Nimeoa mwaka huu. Ndugu wa mke wananjaa sana halafu uelewa wao katika maisha mdogo sana, kila tatizo wakipata kimbilio kwangu, na mimi maisha yamenibana sana siwezi kuwalea. Mke wangu hadi amechoka na anaogopa kuwaambia ukweli, jamani naombeni ushauri nifanyeje. Hali sio nzuri.
 
ndoa haiko hatarini maana bado wewe na mkeo mu wamoja... hatari sababu ya ndugu???mngetofautiana khs hilo sawa.... wewe waambie ukweli,bora lawama kuliko fedheha...
 
kwani umeoa familia/ukoo au binti?
na usingemuoa huyo binti wangekua ombaomba kwa nani?
-----
-----
wasaidie penye ulazima kulingana na uwezo wako.
 
Hapo rahic kaka!!!!!! Mficha uchi hapati mwana! Wafungukie mbele ya mtoto wao (mkeo) maana asipokuwepo watasema ni agenda yako tu. Liwekeni wazi mkiwa familia kuonesha ni kero ya kifamilia, hapo vp kaka!
 
Nimeoa mwaka huu. Ndugu wa mke wananjaa sana halafu uelewa wao katika maisha mdogo sana, kila tatizo wakipata kimbilio kwangu, na mimi maisha yamenibana sana siwezi kuwalea. Mke wangu hadi amechoka na anaogopa kuwaambia ukweli, jamani naombeni ushauri nifanyeje. Hali sio nzuri.

nahisi familia nyingi zinafanana. msiogope kuwaambia ukweli kuwa hamuwezi kuwasaidia kama watakavyo, eti labda watakusemeni vibaya. ubinafsi unawasumbua hao ndugu. lawama sio gunia la misumari, zinabebeka. vinginevyo mtapata maradhi ya moyo. safari njema ya ndoa.
 
Hilo mbona ni tatizo dogo ila kama mnaelewana na mkeo na yeye ameona hao ndugu zake wamezidi.Waambie hali zenu ni mbaya ila chochote kidogo mtakachopata mtawasaidia! Kwani pesa zinaongea mfukoni? Ila ukijionyesha unazo usumbufu lazima.
 
kwahiyo unataka vunja ndoa kisa ndugu wa mke...?!!
 
waambie ukweli ila chagua na chambua maneno ya kuyatoa....
 
Kuna vitu vingine unatakiwa mtu kuwa na hekima katika kufanya maamuzi. Mkeo ndiye wa kuongea na ndugu zake kuhusu suala hilo kama mkeo ataentertain hicho kitu basi tatizo litakuwa kwa mkeo. Furaha ya mkeo ni kuona ndugu zake wanapata ahueni baada ya kuolewa na wewe
 
Mbona rahisi sana wewe kunja ndita tu, muda wote ukiwa nao ucheshi weka pembeni.
 
Haya mambo magumu. Ongea na mkeo mueleweshe tuu kwamba kulinda heshima ya ndugu zake awaambie ukweli hali yenu. Ikishindikana funguja mwenyewe
 
Be real. Fanya unachoweza, na usichoweza unaacha. Wote ndo tunaishi hivyo. Tatueni shida zenu kwanza na then kama kuna ziada saidieni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom