Ndoa yangu haina amani

Inategemea na aina ya mke, niliwahi kufulia japo mke wangu hakuwa na kipato kikubwa sana lakini alisimama imara mpaka hapa nilipo na sikusikia jambo lolote la kudhalilisha utu wangu.
Kwa wewe ulioa mke kweli na ulibahatika! Kwa hawa waliooa wanawake chuma ulete huwezi kueleweka siku mishe zikibuma!
 
Hapo ulikaza balaa mzee baba😀 kilume ndago!
 
Story kama hii sikia tu kwa mwenzio,pole sana mkuu kwa unayopitia,sio kwa nia mbaya lakini inaonesha wife ana mchepuko wake tayari anakutafutia sababu tu ya kuachana..
My Take:Achana nae kabla hajakuletea vituko vya wazi wazi
Natafuta pa kuanzia maisha mkuu ndio jambo kubwa kwangu kwa sasa
 
Liverpool VPN njoo utoe ushauri huku

hawa viumbe hawasikii, wanazidi kuoa
Mkuu Liverpool VPN njoo umshauri jamaa

BTW anayewadanganyaga eti mke anaweza mlea mume ni nani?

Yaan kweli unaomba hela kwa mke ukaangalie mpira .....yaan bila aibu kabisa unaomba
Hawa watu wanachosha sasa...

Umefika muda tuwapige makonzi tu ili kubust akili zao.

Washaambiwa WASIOEEEE ila HAWASIKII.

Haloo brothers NDOA MAJANGA Msioeeee.

#YNWA
 
Amekusikia na tumekusikia Mkuu, nini kifanyike?
Mwanamke keshazaa naye watoto wawili.

Huyu ni Mke wake kabisaa halali ( ukishazaa na mwanamke watoto wawili watatu wala usiumize kichwa tena juu yake ).

Kwa sasa Jamaa, Ajikite kurudisha Thamani yake .

( kihalisia na kama mwanamke angekua Muumini wa Utu, kwa sasa ndio ulikua wakati sahihi wa kusimama na Jamaa, kumpa moyo, kumuombea na KUMFICHIA AIBU JAMAA MBELE ZA WATU)

sisi wanaume kuna ule wakat unataka utoke kidogo, ukae na masela ,n.k, ni wakat wa mwanamke kumwambia " Hubby leo kachamke na wenzako, pesa hii hapa "..

Badala yake mwanamke anazidi kumnyonga jamaaa, Huyu jamaa muda mfupi ujao, ataanza kuona giza, yaan hata kichwa kufunguka ,kitashindwa ..nandio mawazo mabaya mabaya yataanza kumuijiaa...Mke ana mtu .mke amanisaliti..kisa sina hela..kisa hiki....


Lkn niseme ,Toka awali kuna kitu alishakikosea kukitengeza nacho ni HESHIMA.


NDUGU ZANGU, LAZIMA IFIKE MAHALI MWANAMKE AKUHESHIMU PASIPO KUJALI KIPATO CHAKO.


PESA HUJA NA KUONDOKA..LKN UTI WA MTU UTAISHI MILELE NAMILELE MPAKA KUFA KWAKO.


hii inamaana ,Mwanamke mke wako. Lazima auheshimu UTU WAKO wakati wote wa Pesa au kutokua na Pesa.



Tuachane na hayo

Nini Jamaa afanye ???


Jamaa ni mjuzi wa biashara nandio sehem ya maisha yake, watu biashara hkua na kushuka lkn husimama nakuendelea ( niliwah kufungua kabishara nikamuweka Ndugu yangu, alikula mpaka mtaji ,kakafa kote)
Ila sikuacha..


kwakua ana nyumba, na mjuzi wa biashara , Akakope Pesa anayojua inatosha kabisa kuanzisha bishara

Ni vema pia asikae kimya, awashirikishe wazazi, na ndugu zake wa damu, mawazo yao nayake ,ataondoka na kitu ( shida ya wengi ni kukaa na mambo moyoni)

Jamaa asikaee kumfatilia mwanamke, asikae kumuomba kitu kwa mwanamke.

Aanze mapambano , yaan huyo Mwanamke , Dawa yake ni sio kumkimbia, sio kumfukuza sio kuachana naye sababu HAMNA BAYA LA KUFANYA IVO ....LABDA KAMA KUNA USALITI ATAUFANYA KWA JAMAA , SABABU TU YA MAISHA YA JAMAA YA SASA.


Kuomba Mungu, kwa uwezo wetu ,kutoboa maisha ni kazi , unamuomba Mungu akupe njia na kubariki mikono yako.
 
Usioe mke wa Pili ,,Kaka.

Unayo nafasi kubwa sanaaaa ya kurekebisha na maisha yakaendelea kua sawa.


Mimi kwenye kutengana, huwa nashaur mtu aachane na mwanamke km amesalitiwa na amejua.
 
Inategemea na aina ya mke, niliwahi kufulia japo mke wangu hakuwa na kipato kikubwa sana lakini alisimama imara mpaka hapa nilipo na sikusikia jambo lolote la kudhalilisha utu wangu.
Hili ndio mimi nalisemea .


HONGERA SANA MKUU, WEE UNA MKE ALIYETOKA MBINGUNI KWA BABA MUNGU.
 
Nimejiuliza maswali kama yako mkuu, nikaaandika aa weeeee afu nikafuta, yaani
 
Pole sana
Nyakati zingine sie wanawake kweli mtihani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…