Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Mastaa wa Filamu Bongo waliokuwa wanandoa, Mike Sangu na Salome Urassa ‘Thea’ wamepelekana kwa padri wa Kanisa la Katoliki Parokia ya Mwananyamala jijini Dar kwa ajili ya hatua ya kutalikiana.
Chanzo kilicho karibu na mastaa hao kilidai kuwa, Thea ndiye aliyekusanya picha anazoposti Mike kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa na mpenzi wake wa sasa aitwaye Eliza na kuzipeleka kwa Padri ili kushawishi apewe talaka yake.
Ili kujua ukweli wa habari hiyo, mwandishi wetu alimtafuta Mike, alipopatikana alisema:
“Ni kweli niliitwa nikajieleza ingawa habari hizi nisingependa ziandikwe magazetini kwa sababu bado ziko ngazi ya kanisani,” alisema Mike huku Thea akigoma kuongea chochote akidai ni mambo yake binafsi”.
Source: Bongo Movie