Ndoa’ ya Sumatra, majembe yavunjika rasmi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
SIKU chache baada ya serikali kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kuvunja mkataba na Kampuni ya udalali ya Majembe Auction Mart ya Dar es Salaam, mamlaka hiyo imeanza kufanya kazi zilizokuwa zikifanywa na Majembe.
Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, aliagiza mkataba huo kuvunjwa ifikapo Desemba 31 mwaka jana na katika kutimiza agizo hilo, jana Tanzania Daima liliwashuhudia maofisa wa Sumatra na askari wa Usalama Barabarani wakiyadhibiti magari hasa daladala.

Kazi hiyo ilionekana ikifanywa kwa nguvu na Sumatra baada ya maofisa wake kutanda katika maeneo mbalimbali ikiwamo Mtoni Mtongani, Kariakoo na Ubungo, hali iliyowafanya madereva wa daladala kuwahofia hivyo kuongeza umakini.

Kampuni ya Majembe ilipewa na Sumatra mkataba wa uwakala wa kusimamia shughuli za daladala jijini kwa miaka miwili kuanzia mapema mwaka jana.

Pamoja na mambo mengine, Nundu alisema kuvunjwa kwa mkataba huo kutasaidia kupunguza kero zinazosababishwa na Majembe.

Waziri huyo alisema wameamua kuuvunja mkataba huo kutokana na Majembe kuendelea kukiuka sheria na kanuni walizopewa kabla ya kuanza kazi za uwakala.

Kwa mujibu wa waziri huyo, Majembe ilianza kufanya kazi zisizowahusu ikiwemo za usalama barabarani na kubainisha kwamba hizo ni baadhi ya kazi zinazotakiwa kufanywa na askari wa kikosi cha Usalama Barabarani.
 
Back
Top Bottom