Ndoa ya mzee "majuto" yavunjika

BashiriOnline

Senior Member
Nov 5, 2012
127
44
MWANAMKE anayedaiwa kufunga ndoa ya
siri na mchekeshaji mahiri Bongo, Amri
Athuman maarufu kama Mzee Majuto au
King Majuto, Rahma Abdallah (20), ameibuka
na kudai kutelekezwa na mumewe huyo.

Ndoa hiyo ambayo ilifungwa kwa siri jijini
Dar Julai 28, mwaka huu na kudumu siku
44, inaonekana imevunjika rasmi baada ya
Mzee Majuto kutoa talaka kupitia kwa msanii
wa filamu aitwaye Rehema Omary.

Akizungumza na mwandishi wetu, Septemba
9, mwaka huu, Rahma alidai kuwa alikutana
na Mzee Majuto jijini Tanga na kuanzisha
uhusiano wa kimapenzi kwa miezi sita kabla
ya kufunga ndoa Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani uliopita.

“Tulifahamiana Tanga, mimi ni mwenyeji wa
huko kama ilivyo kwa Mzee Majuto, wakati
tukiwa kwenye uhusiano, ulipofika Mwezi wa
Ramadhani akaona bora tufunge ndoa ili
tusiendelee kutenda dhambi, akaniambia
dhamira yake hiyo nami sikukataa,” alisema
Rahma.

Mke huyo ambaye ni kibinti cha umri wa
miaka 20 aliyepishana na Mzee Majuto kwa
umri wa miaka 40 alisema kuwa, mwigizaji
huyo alifuata taratibu zote za kufunga ndoa
kwa kupeleka barua ya posa nyumbani kwao.
“Alitoa mahari ndipo ilipopangwa siku ya
ndoa iliyofungwa nyumbani kwa mama
yangu, Mbagala-Zakhem, Dar,” alifafanua
Rahma.

Katika ndoa hiyo iliyofungwa katika Mtaa wa
Kibonde-Maji Julai 28, mwaka huu na Shehe
Abdurahman Kisoma na kufuatiwa na
sherehe nyumbani kwa bibi harusi, ulinzi
mkali uliwekwa ili siri ya Mzee Majuto kuoa
isivuje.

Mashahidi wa ndoa hiyo walikuwa ni
Suleiman Said ‘Barafu’ ambaye ni mwigizaji
aliyekuwa mpambe wa bwana harusi pamoja
na Mohammed Malila.

Cheti cha ndoa hiyo, kinaonesha kwamba
Mzee Majuto alimuoa mwanamke huyo kwa
mahari ya shilingi 20,000 aliyolipa yote.
“Baada ya ndoa, Mzee Majuto aliwaomba
wazazi wangu nikae nyumbani hadi Mwezi
wa Ramadhani utakapoisha ndipo
atakapokuja kunichukua, akaniachia shilingi
elfu sitini tu, mpaka leo hii sijamuona,”
alisikitika mke huyo ambaye alikuwa akijua
kama Mzee Majuto alikuwa na mke
mwingine.

Mke huyo wa Mzee Majuto alisema kuwa
kabla ya kufunga ndoa na gwiji huyo wa
uchekeshaji alikuwa akifanya kazi katika
saluni ya mwanamuziki Joseph Haule
‘Profesa Jay’ iliyopo Msasani, Dar.
“Nilikuwa nafanya kazi na kupata kipato
huku nikiwa nimepanga chumba lakini
Majuto aliniambia niache kazi na nirudishe
chumba, nami nikafanya hivyo nikijua naenda
kuishi kwa mume wangu, kumbe!...” alijuta
Rahma.

Baada ya Majuto kuondoka mke huyo alikuwa
akimpigia simu kutaka fedha za matumizi
lakini alikuwa akiambiwa awasiliane na Bi.
Rehema, mwanamke ambaye Mzee Majuto
huwa anaigiza naye katika filamu zake.
Rahma alilalamika kutumiwa ujumbe wa
matusi kwenye simu yake na mke mkubwa
wa Mzee Majuto.

“Kitendo hicho kinaniuma sana kwani wakati
mwingine huwa ananitukana na kunitishia
maisha, akidai eti atanifanyia kitu kibaya,
nikimpigia Majuto na kumweleza naye
ananijibu mbovu,” aliongeza.
Mke huyo mdogo wa Mzee Majuto alisema
kuwa anaumia kutokana na kuharibiwa
maisha kwa kuolewa na kuachishwa kazi
huku akiendelea kutukanwa na mke mkubwa.
Rahma ambaye aliliachia Amani nakala ya
cheti cha ndoa alisema msanii huyo
amemdhalilisha kwani kila akidai talaka yake
anamwambia ameshaituma kwa Bi. Rehema
na kumtaka aende akaichukue kitu ambacho
ni kinyume na makubaliano yao.

Rahma alisema kuwa amejipanga kwenda
kumshitaki Mzee Majuto katika Baraza Kuu la
Waislamu Tanzania (Bakwata) ili amlipe fidia
na kumtafutia kazi.
“Yeye ndiye aliyenioa lakini nikimdai talaka
ananimbia alimpa Bi.Rehema, wakati
mwanamke huyo siye aliyenioa, sasa
nampeleka Bakwata ili anikabidhi talaka na
kunilipa fidia,” alisema kwa hasira mke huyo.
Akijibu tuhuma hizo akiwa jijini Tanga, Mzee
Majuto alikiri kufunga ndoa na Rahma na
kusema kuwa alishamuacha kwa sababu
aligundua hajatulia.

“Huyo mwanamke nimeshaachana naye ila
kwa sasa anataka kunichafua, kama anahisi
ana haki kwa nini asiende mahakamani?
Nimemtuma mshenga ampe talaka hataki
kuipokea, anataka nije Dar. Kama huo siyo
uhuni ni nini? huyo mwanamke hajatulia,”
alisema.
 
Njaa zinaharibu utu'... sidhani kama alimpenda ulijua tu ndo ameshatoka kimaisha' then atatafuta kipoozeo mbele kwa mbele!! Mmh.. majuto nae
 
Wanawake jamani???mtoto mdogo ukawekwe ndani na jibabu lote hilo??au umaarufu ulimzingua?ndio akome hivyo kama alijua shida zake zitakwisha ameula wa chuya..Majanga!....
 
Wababu wengine wanajua kujifhalukudha kuoa binti mdogo maana yake nini? Au anataka kumfia kifuani???
 
Back
Top Bottom