'Ndoa' ya Hosea, Richmond na Serikali ni batili, ivunjwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Ndoa' ya Hosea, Richmond na Serikali ni batili, ivunjwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Watanzania, Nov 4, 2009.

 1. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sote tunaelewa kuwa tangu mwanzo Hosea na TAKUKURU yake waliisafisha Richmond. Serikali nayo imekuwa inamshupalia kila anayehoji Richmond. Serikali iliweza hata kuficha kumbukumbu kuhusu Richmond, hadi leo hazijulikani zilipelekwa wapi na hakuna hata mtumishi mmoja aliyeulizwa na Serikali kuhusu upotevu huu wa nyaraka ambazo zilikuwa muhimu katika uchunguzi wa mkataba wa kitapeli wa Richmond.

  Hosea anachofanya sasa ni kuendeleza ‘mapenzi’ yake kwa Richmond. Na serikali inashirikiana na TAKUKURU ili mrembo huyu Richmond kipenzi chao aendelee kuwa salama. Kwetu sisi wananchi tunawataka wabunge katika bunge hili linaloendelea wamalize suala la Richmond kwa kupata taarifa za utekelezaji wa maamuzi ya Bunge letu kuhusu Richmond. Na kama taarifa hazitaridhisha basi tunawaagiza wabunge wetu wamtake Rais avunje bunge ili waje kutuomba kura upya.

  Suala la Posho analoshikia bango Hosea na Serikali katika kulinda ndoa yao na Richmond kwa sasa siyo kipaumbele cha wananchi. Watanzania tunataka kwanza suala la Richmond liishe halafu habari ya posho ije baadaye kama serikali na Hosea wanaubavu wa kutosha kushughulikia suala hili. Hatutaki kwa sasa mjadala uhame kutoka kumaliza suala la Richmond kwenda kujadili masuala ya posho. Hapa hata vyombo vya habari vimeshatekwa

  Miezi michache iliyopita katika wilaya moja hapa nchini, kaimu mkurugenzi alikataa kulipia gharama za malazi za msafara wa makamu wa Rais Mh. Shein. Wanasiasa katika wilaya hiyo walimshupalia Mkurugenzi huyo kulipa gharama hizo yeye akakataa akisema kuwa hakukuwa na bajeti yake. Ilibidi waziri Kombani amtetee kuwa hajatenda kosa lolote kutoa malipo hayo. Lakini ni wakurugenzi wangapi ambao huko nyuma wameza kukataa kutoa malipo kama hayo? Ni wazi makamu wa Rais na Rais pia pamoja na mawaziri na watendaji wengine wa serikali kama makatibu wakuu wamepewa malipo mara mbili. Hosea na Serikali wakitaka washughulikie suala la posho mara mbili hawana budi kupanua wigo, siyo kwa wabunge tu.

  Suala muhimu hapa ni kuwa Hosea asiwang’ang’anie wabunge pekee kuhusu posho na hasa katika kikao nyeti cha kumaliza suala la Richmond. Hosea na Serikali wasivuruge mchakato wa bunge kwa maslahi ya kulinda ndoa yao na Richmond ambayo ni Batili.
   
Loading...