Ndoa ya Denti Shule ya Salma Kikwete Aibu!

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,446
Aibu! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya ndoa ya denti wa kidato cha pili wa Shule ya Sekondari ya Salma Kikwete, Tunu (16) kushindwa kufungwa baada ya polisi kuvamia kwa madai kuwa bibi yake aitwaye Zainabu na babu yake walitaka kumfungisha ndoa bila ridhaa ya binti huyo.
Sakata zima lilitokea hivi karibuni, maeneo ya Mwanayamala Kisiwani jijini Dar, anapoishi denti huyo na bibi yake pamoja na babu yake ambapo wazazi wake walishafariki dunia.

qq.jpg

Akisimulia mkasa mzima, mama mdogo wa binti huyo aliyefahamika kwa jina moja la Veronica, aliyesaidia kutoa taarifa polisi ili binti huyo asiolewa, alisema kuwa yeye na denti huyo wanafahamiana kwa sababu walikuwa wanakaa majirani ambapo alikuwa akimsaidia baada ya wazazi wake kufariki na ndiyo maana anamuita mama mdogo.

“Unajua wazazi wa Tunu walipofariki nilikuwa nikimsaidia saidia mpaka akaingia kidato cha kwanza lakini nilipata matatizo nikaenda nyumbani ambapo nami nilifiwa na wazazi wangu, niliporudi nilihama huko Mwananyamala lakini hivi karibuni nilikwenda kumfuatilia kule shule alipokuwa anasoma nikaambiwa kuwa hayupo alisimamishwa kutokana na ada,”alisema mama mdogo huyo.
Aidha, mama huyo alisema kuwa juzi alipokuwa nyumbani simu yake iliita ndipo akapokea na kusikia sauti ya dada yake na Tunu ambaye alimuomba amsaidie kwani Tunu anataka kuozeshwa na bibi na babu yake siku hiyo ya Jumapili (wiki iliyopita).

“Nilitafuta msaada wa serikali ya mtaa, polisi, ustawi wa jamii pamoja na vyombo vya habari ndipo tukaenda kuvamia hapo nyumbani ambapo tulimkuta Tunu akiwa kwenye maandalizi ya kuolewa huku bwana harusi naye akiwa amekwenda msikitini kufunga ndoa kisha ndiyo aje nyumbani kumchukua mwari wake,” alisema mama huyo.

TUNU AELEZA ILIVYOKUWA
Baada ya kuongea na mama huyo, mwandishi wetu alimsaka Tunu ambaye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa bibi yake alitaka kumuozesha kwa mwanaume ambaye yeye hakumfahamu hapo awali na kwamba yeye alikuwa bado anahitaji kusoma kwani alisimama baada ya kukosa ada.
“Baada ya kukosa ada na kushindwa kufanya mtihani wa kidato cha pili bibi aliniweka ndani na aliniandalia mwanaume wa kunioa lakini nashukuru Mungu nimeokolewa,” alisema Tunu.

BIBI AJITETEA

Ili kuupata ukweli wa denti kutaka kuolewa, polisi na ustawi wa jamii waliingia nyumbani kwa bibi na kujifanya wao ni wageni wa upande wa muoaji ambapo bibi alifurahia na kuwaomba wasubiri mpaka bwana harusi atakapotoka msikitini ndiyo watamuona mwari wao.
Baada ya bibi kuwaeleza hivyo, polisi na watu wa ustawi walimbana na kuanza kumhoji sababu ya kumuozesha denti ambapo alibadilika na kuanza kujiumauma kisha kusema kuwa anachojua mjukuu wake ni mwari na wala si bi harusi na siku hiyo aliiandaa kwa ajili ya kumtoa.

MSHENGA NAYE ATOA NENO
Mshenga ambaye jina lake halikufahamika alijitetea na kudai kuwa yeye anachojua ni kwamba binti na bwana harusi walikubaliana na kabla hajawakutanisha alikwenda kuongea na bibi harusi ambaye hakumweleza chochote bali alikubali kuwa ataolewa.

“Mimi nashangaa kuona nakamatwa wakati bi harusi alinikubali, niliongea naye kabla ya harusi na nina hata picha zake kwenye simu yangu siku hiyo nilipokuja kuongea naye, mambo ya kuwa ni mwanafunzi sikuyajua na wala sikujua kama haitaki ndoa,” alisema Mshenga.

BWANAHARUSI APATA KIGUGUMIZI

mwanafunzi.jpg

Bwana harusi, Sefu, alipoulizwa kama alikuwa akifahamiana na bi harusi alishikwa na kigugumizi na kudai kuwa hakumjua bi harusi kabla na wala hakujua kama ni mwanafunzi.
“Nilimtahadharisha mshenga kama bi harusi atakuwa hataki asimlazimishe kwani hata dini haitaki hivyo lakini hakuniambia kama alikataa labda tumuulize yeye,” alisema bwana harusi.

MWENYEKITI ATHIBITISHA
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwananyamala- Kisiwani, Haji Makame alithibitisha kuwa yeye ndiye alivunja ndoa hiyo ambayo ilikuwa imeshaanza kufungwa ambapo alimkuta babu wa denti akimsimamia mjukuu wake kuolewa kama mtoa idhini na kuamuru ndoa isifungwe achukuliwe babu, bwana harusi na bibi harusi waende kwenye mikono ya sheria.
“Mimi na mwenyekiti mwenzangu wa mtaa husika tulipofika msikitini tulikuta ndoa ishaanza kufungwa, nikataka kujua binti anayefunga ndoa akaitika babu yeye ndiye anahusika, nikamuuliza unafunga ndoa na mwanaume mwenzako akakataa na kusema kuwa yeye ndiye anatoa idhini na yupo pale kwa ajili hiyo na hapohapo ndipo niliamuru babu na bwana harusi tuongozane tukaonane na mkono wa sheria,” alisema mwenyekiti.

BIBI, MSHENGA NA BWANA HARUSI POLISI
Baada ya maongezi hayo polisi walimchukua bibi na mshenga pamoja na bwana harusi na kuwapakiza kwenye difenda na kuwapeleka Kituo cha Polisi Osterbay kwa ajili ya hatua za kisheria.

Chanzo:Globals Publishers
 
Ikishafikia hatua hiyo kuzuia kuolewa ni jazi bure....
 
Sasa hapo tatizo ni lipi make huyu si mwanafunzi tena kwa kuwa hata mtihani wa kidato cha pili hakufanya na hakuwa anaendelea na masomo.!!! Jamaa kabaniwa hivi hivi asee
 
Uzuri huyu jamaa hajambanjua huyu demu.

Mwananyamala pale msisiri Primary wanafunzi wanafanya mapenzi madarasani, hii inatokana na shule kuwa kwenye makazi ya Watu, imezungukwa na Baa na Gesti house na kijiwe cha Rama-Deta cha kuuzia unga na bangi.

Ukipita kuanzia saa moja usiku unakuta wanafunzi wameshikishwa ukuta na miguno kwa mbali tu, hao hawajafika lasaba.
 
bwana harusi aliambiwa bibi harus kamaliza 4m 4 hakufaulu na yupo 16yrs age kwa mujibu wa sheria anaruhusiwa kuolewa kwa ruksa ya wazazi, kosa lake nn????????

Acha uzandiki unatetea uasherati, Miaka 16 hata Uke haujakomaa, Ni kumharibu na kumsababishia fistula na kansa ya mlango wa uzazi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom