pwilo
JF-Expert Member
- May 27, 2015
- 10,098
- 12,473
Ikiwa imebaki siku moja kabla ya kuingia mwaka 2024 na kuuaga mwaka 2023 kwangu mimi naweza kusema mwaka 2023 ulikuwa mzuri na ulikuwa na maumivu pia ndani yake.
UZURI.
mwaka 2023 nilibahatika kuoa baada ya kusua kusua na familia kupiga kelele kwa mda mrefu nikaamua kuo siwezi sema nilishinikizwa ila nilikuwa nishajipanga sema kuna mambo tu hayakukaa sawa ya kikazi ndio ilikuwa kikwazo.
Niliamua kuanza maisha mapya na mpaka sasa tunaendelea vizuri na mke wangu na mungu akijalia mwakani tunatarajia mtoto. Ilikuwa furaha kwa familia ndugu na marafiki lakini hasa wazazi wangu akiwemo mama yangu mzazi baba yangu mzazi pamoja na bibi na babu yanga na ndugu zangu wakizaliwa tumbo moja.
Sikutaka harusi ya gharama na niliwaambiwa nyumbani wafanye sherehe ya kawaida na hata michango sikuchangisha kwasababu nilikuwa sitaki harusi ya show off lakini familia na ndugu walikataa wakasema mimi nitulie niwaachie wao swala hilo mimi nisubirie kuchukua mke tu hakika harusi ilifanya licha ya kutotaka michango na kuchangisha hela ila marafiki zangu na ndugu walipopata taarifa walinipigia simu wakilalamika kwa nini sijawaambia mapema na wengine kuahidi kunichangia kidogo walichojaaliwa na kweli walifanya hvyo.
Harusi ilifanyika kwa siku tatu siku ya kwanza ilikuwa maulidi siku ya pili ilikuwa mziki siku ya tatu ilikuwa after party kwa kweli ndugu na familia walifurahi sana na hata mimi nilifurahi sana hasa baada ya marafiki zangu ambao tulikuwa na kusoma pamoja kujitokeza licha ya kutowasiliana kwa mda mrefu nilifurahi sana nikikumbuka ile misafara ya boda boda na magari kwakweli ilikuwa siku ya furaha sana.
HUZUNI.
Mzee wangu alikuwa anaumwa mda mrefu sana alikuwa anasumbuliwa na sukari na moja kati ya kauli zake ilikuwa ananiambia mwanangu fanya uoe au unataka mpaka wazazi wako tufariki ni moja kati ya kauli ambayo naikumbuka mpaka leo hii. Mimi naishi mbali na familia hivyo baada ya harusi tukaagana na kupeana mikono kumbe ilikuwa ndio tunaagana.
Ni miezi miwili sasa baada ya mzee kutangulia mbele ya haki mungu amlaze mahala pema maana alichokitaka kwa mda mrefu alikishuhudia.
Pumzika kwa amani mzee wangu.