Ndoa ya CCM na CUF ilifanyika lini?

Hii ndio JF, ndani ya muelekeo mpya na MODs ni kama wamelala. Hivi hii picha si inajulikana ilipigwa kwa tukio gani. Sasa yamekuwa makubaliano ya SIRI. Kazi kweli kweli.
 
Ndoa ni ndoana!! Ndoa hii mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh? Hata hivyo vibaraka ni wengi?
 
:smile-big: Alaaaaaah, kumbe!!!! Kelele zote za kumuunga mkono Slaa awe next Prezidaa ni suala la ukatoliki. Basi mimi nasema KESHA SHINDWA. Udini wa aina hii haukubaliki TZ. Udini, rangi, ukabila, jinsia nk. visituongoze katika kupata viongozi. Kwa wale wenye itikadi hii, bora mkae kimya kabisa.

Sasa mimi nasema HATUDANGANYIKI kwa ajili ya UKATOLIKI wake. Atapata 32% tu ya kura zote, niko hapa na mtaniambia.
 

Kwa hiyo mwaka huu mmepanga kuiba 68% ya kula (sorry, kura)?
 
Mi nadhani mmechanganyikiwa! Ukisha changanya hisisa za dini na siasa unakuwa umejimaliza, huwezi kumridhisha mtu. Hebu toeni story nzuri zenye kuleta maelewano na si kuleta mkorogano bana!
 
Je yanahusu:

1. Mahakama ya kadhi?
2. Kuingiza Tanzania kwenye nchi za kiislam?

Kwa mwanaCHADEMA aliyekubuhu kama wewe kuanzisha propaganda ya aina hii inaonyesha wazi wapi tunaelekea......

Nawakilisha

omarilyas
 
Mkuu si suala la udini na sisi hatuko huko (simsemaji wa Mwafrika) hii issue ni kubwa si nyepesi kwa ustawi na maendeleo ya nchi yetu. Tutaweka hapa hold on wakati muafaka. Soma maneno yangu

Ni fikira za UDINI tu ndio zinazodetect mitazamo yenu katika hili.....hakuna kingine
 
Mzee Kibiongo! Umezeeka lakini akili zako ni za mtoto wa miaka miwili!!!!
 

Sizitaki mbichi hizi.....Hivi mnajua kama hao wapiganaji wenu huko kwengine mpaka dakika ya mwisho walikuwa wanalobby angalao kuteuliwa ubunge na rais....Hivi mnajua kuwa baadhi ya hao wapiganaji wenu waliwahi kuwa tayari kuhama chama ili wateuliwe Ukuu wa Wilaya na wazee wa chama wakakubaliana nalo....

Acheni huu ujinga wa kukimbilia kuita watu wasaliti mradi tu wameweza kuwalazimu wapinzani wao kukaa chini na kushirikiana katika level sawa. Mtu yeyote anayeona serikali ya mseto Zanzibar ni usaliti wa CUF ni ama hana mapenzi na watu wa Zanzibar ama kwake yeye damu za watu wa Zanzibar kuelendelea kumwagika ndio furaha yake kwa muono kuwa inasaidia maslahi ya "upande" wake.

Walichofanya CUF ni UTHUBUTU WA KIUONGOZI (COURAGE OF LEADERSHIP) wa hali ya juu ambao wale walioamua kukumbatia siasa za ujanjaujanja kama wafanyavyo baadhi yenu hivi sasa kamwe hawawezi kuelewa.
 
Kuna habari ambazo nina wasiwasi nazo ,habari zenyewe ni kuwa Chadema imetumika katika kuiletea ushundi CCM na ni pale Slaa alipopiga U-TURN na kujiingiza katika kinyang'anyiro cha Uraisi ,ikumbukwe kuwa wengi wa wagombea wa vyama vya upinzani walikuwa wameshaamua kutogombea nafasi hiyo ,na wote kuelekeza nguvu zao katika kugombea ubunge.

Hapa tayari Watanzania walikuwa wameshalenga shabaha ya kuiangusha CCM kwa kupeleka nguvu zao kwa Mgombea mmoja tu wa CUF ,Lipumba ,mgombea ambae angeweza kabisa kuilaza CCM kutokana na kura zitakazo miminika kutoka vyama pinzani.

Ingawa wengi hawafahamu kilichomsukuma Slaa kugombea nafasi hiyo ,wenyewe ndani ya Chadema wanadai au yeye mwenyewe Slaa anadai kuwa wamempendekeza, ingawa yeye mwenyewe alikuwa hataki kuingia katika ugombea huo,hizi ni mbinu za kuwateka waTanzania na kuwalaghai kuwa ni mapendekezo ya Chama. Hapa mkae mkielewa kuwa pamechezwa mchezo mkubwa sana na kuwafanya hata wale waliokuwa na msimamo mkali wabaki wakiamini kuwa Chama ndio kimependekeza ,nawaomba mjaribu kuchunguza kwa kina kabisa mtauona ukweli kuwa hapa CCM wametumia karata yao ya kuwa na chama risavu ambacho ni Chadema,huwezi kuamini kirahisi lakini siasa ndivyo zilivyo wanaofahamu ni wachache sana.

Wengi tulishangaa sana na kutaka kujua kilichomsukuma Slaa na sasa imeeleweka kuwa CCM wamemtumia na wameshafanikiwa katika kuwagawa WaTz kwa mara ingine,you must think hard to get the inner core of the Slaa turning factors.

:A S-danger:
 
mkuu signature yako naona unaitekeleza kwa vitendo
 
Mhhh another conspiracies! I beg you to communicate with ur brain before posting rubbishes and worms in the forum!
 
Mhhh another conspiracies! I beg you to communicate with ur brain before posting rubbishes and worms in the forum!
M

Mbona unakuwa mkali, jibu hoja kwa hoja Pastor, unapoteza uelekeo au ndiyo dalili ya kulemewa
 
M

Mbona unakuwa mkali, jibu hoja kwa hoja Pastor, unapoteza uelekeo au ndiyo dalili ya kulemewa
mkuu tatizo la upinzani kushindwa haliletwo na slaa pekee... in actual facts, linaletwa na existing system ambayo role inayokuwa played na upinzani ni ndogo mno... kwahiyo kusema ni slaa its a mistake, ni kama kutafuta mchawi tu!!!

one needs to ask, hivi kweli mtu unagombea mpaka watu wanaacha hata kuuliza utatufanyia nini, lakini hukati tamaa?? chadema left z'bar for cuf, but there is not mutual feeling for them in the mainland where prof is getting weaker and weaker

that being said, i still believe hata waungane, with the current set up, ushindi ni ndoto

wajifunze kenya jinsi taifa lilivyopata moto wa maendeleo bada ya kupitisha katiba mpya

hata wachina wa kenya wanamaliza kazi kabla ya muda
 
Kuna habari ambazo nina wasiwasi nazo
Wengi tulishangaa sana na kutaka kujua kilichomsukuma Slaa
Habari za kutunga mwenyewe kwa nini uwe na wasiwasi nazo au wasiwasi kuwa zitagundulika kuwa ni za uongo. Kama ulivyoseama wengi mlishangaa kwa ujio wa Dr. Slaa na bado mtazidi kushangaa atakapoanza kampeni stay tuned.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…