Ndoa ya bomani inatambulika kisheria

Ndoa ya bomani inatambulika kisheria

teenwolf

Senior Member
Joined
Feb 12, 2017
Posts
122
Reaction score
76
nauliza,ndoa ya bomani inatambulika kisheria?

vipi ikitokea migogoro ndani ya ndoa?

kuna migogoro ambayo ni LAZIMA kusuluhishwa kiimani zaidi???
 
Kuna kitu ambacho unafanya kiserikali ambacho hakitambuliki kisheria?!...nenda ofisi za mkuu wa wilaya ukaulize
 
Ni ndoa kama zilivyo ndoa zingine!
Tofauti ni imani ya dini tu, haitambuliki kanisani
 
Kazi ya kufungisha ndoa ni ya serikali sio dini! Kama ilivyo kuhesabu watu, kuandikisha wapiga kura,nk Dini zinapofungisha ndoa zinafanya hivyo kwa idhini na kwa niaba ya serikali! Ndio maana wanaofungisha ndoa katika dini ni lazima waidhinishwe kufanya kazi hiyo na serikali yaani maombi hupelekwa serikalini kisha serikali hutoa kibali cha kufungisha ndoa. Vyeti vinatolewa na serikali sio dini na vimefanana bila kujali ni dini gani inafungisha ndoa. Ndio maana mfungishaji ndoa katika hatua ya kufungisha baada ya viapo huwa anasema "kwa mamlaka nilitopewa na jamhuri namtangaza John na Eddah kuwa mme na mke"
Kwa hiyo Mkuu wa wilaya ndiye hasa mwenye jukumu la kufungisha ndoa, hao wengine wanafanya hivyo kwa niaba yake
 
Tena ndoa ya bomani naona ni nzuri zaidi kwa wale ambao wangependa kuoa mke zaidi ya mmoja.

Pale bomani wanamuuliza kabisa mwanaume kama ndoa yake itakuwa ya mke mmoja au wengi, na kuna sehemu kabisa wanatick.
 
Kuna dada mmoja alipata mchumba wa dini tofauti, wenyewe walikubaliana wafunge ndoa bomani, baada ya hapo wazazi wa mke walikuja juu, lazima kijana abatatizwe, kwakua walipendana alibatizwa ndoa ikafungwa kanisani.

Kwa mume wamekuja juu, mwisho wa yote wote walislim ndoa ikafungwa tena kwa ubani, nikikaa ninawaambia nyinyi kuachana kwenu itakuwa shida, si kwa ndoa tatu.
 
kisheria hiyo ndio ndoa hasa ya kisheria!ni sheria zinazotambulika na mahakama mwanzo mwisho!!
 
Back
Top Bottom