Ndoa nzuri ni suala la bahati acha ujuaji

Ndoa nzuri ni suala la bahati acha ujuaji

Mjanja M1

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2018
Posts
4,197
Reaction score
14,902
Habari zenu Wakuu,

Nimekuwa nikisoma Threads tofauti za wanaume wenzangu wakilalamika kuhusu ndoa na kujiapiza kuwa hawatokuja kuingia kwenye taasisi hii adhimu ya Ndoa.

Ngoja niwaambie ukweli tu ambao nahisi wengi hamuujui au hamtaki kuujua kwa ubishi wenu...

Wakuu! Ndoa njema ni Bahati na sio ujanja wako binafsi na Upendo wa kweli kuupata ni bahati pia, maana upendo huwa haununuliki hata siku moja.

Ukibahatika basi umeula, ila ukikosea basi umepotea.

Kwa imani yako omba muumba wako akujalie uipate hiyo bahati na sio vyenginevyo. Wewe binafsi hauwezi na hautoweza kuupata upendo wa dhati kwa pesa zako au ujanja wako.

Omba kwa Imani yako, wakati sahihi ukifika basi utampata wa ubani wako.

NB. USILAZIMISHE UPENDO, USITUMIE PESA KUMSHAWISHI MTU AKUPENDE.
 
Mkuu mwenendo wa ndoa sio suala la bahati, ni zaidi ya 70% mchango wa wanandoa husika. Hizo 30% weka marafiki, wazazi, dini, uchumi na mazingira.

Hakuna swala zuri linalobahatishwa, lazima lina mazingira yaliyolivuta kutokea. Uwe unajua au haujui, matukio ni matokeo ya maisha yetu.
 
Kupendana ni bahati na sio Formula.

Ndoa nyingi zimejengwa na upendo wa upande mmoja na sio pande zote mbili, ndio maana malalamiko yanatokea kilasiku kuhusu hizo ndoa.

KUPENDANA NI BAHATI NA SIO VYENGINEVYO.
 
Ngoja waje kataa ndoa , wana majibu yote sahihi kuhusu ndoa .
 
Kupendana ni bahati na sio Formula.

Ndoa nyingi zimejengwa na upendo wa upande mmoja na sio pande zote mbili, ndio maana malalamiko yanatokea kilasiku kuhusu hizo ndoa.

KUPENDANA NI BAHATI NA SIO VYENGINEVYO.
Wewe unapinga kuwa kupendana sio formula, well and good. But hakuna sehemu nimesema kupendana ni formula, so why umeni quote Mkuu?.

Nadhani usome vizuri na ujue kutofautisha hoja/mitizamo ili uweze kupinga au kukubali hoja lengwa.

Mimi nimesea kila kitu kina chanzo, hakuna jambo la bahati. Hata huko kupendana kunasababishwa (chanzo) na jambo fulani.
 
Back
Top Bottom