Ndoa nyingine wanaishi kama 'hostel'


tehe tehe tehe tehe..................................
 
wakati mwingine wanaume wenyewe mnasababisha mama aamue kuchukua jukumu la ubaba wenye nyumba kutoka na kushindwa kwenu kuyakabili majukumu yenu ya ubaba ya kila siku. Mama anakuwa ndie wa kutatua mahitaji ya familia kwa uharaka zaidi kuliko mwanaume.
 

Siyo kweli acha kupotosha.
 
huyu kabanga is my role model,for really....na hiyo avatar ya django unchained,ndo umemaliza kabisa...huwa hana mistari mirefu kwenye kuchangia hoja but maneno yake yanaishi aisee...Kabanga,SALUTE!
 
Kwa kijana anaefuta maadili ya kibantu kamwe hawezi kuwa hivyo. Hayo ni matokeo ya tamaduni za kitapeli.
Sifa za kichwa cha nyumba mmeipoteza wanaume wengi, unaishi kwenye nyumba hujui pango ni bei gani, unafungua fridge unatoa beer hujui mke wako ametoa wapi pesa. Hata wife akikwambia anakwenda seminar huna hata nguvu ya kuuliza utakaa muda gani.
 
Mwanamke Mmoja Nimemsikia Kwenye Tv Kwamba Kama Mwanamke Anajitosheleza Kiuchumi, Na Mwanaume Yuko Chini Yake, Wa Nini?
 
Umagharibi umechangia kwa kiasi kikubwa, na uko kwenye kitchen party ndo wanawake wanalishana sumu kabisa sasa akija kwa ndoa anaitapika kama ilivyo. Afu mambo ya mwanaume kutokuwajibika kwa familia nayo ni shiida katika hili.
 
Mwanamke Mmoja Nimemsikia Kwenye Tv Kwamba Kama Mwanamke Anajitosheleza Kiuchumi, Na Mwanaume Yuko Chini Yake, Wa Nini?

That is very wrong, huolewi kwasababu mwanaume mambo super, mwanamke ameumbwa kuwa msaidizi wa mwanaume lakini Mungu anaweza kuleta rizki kupitia mikono ya mwanamke.
 
ukiona unaogopa kuoa ujue una matatizo....sio wanawake wote wako hivyo
 
wanandoa inabidi kila mtu asimame kwenye nafasi yake
 
wadada hawana shida tatizo ni wababa hawasimami kwenye nafasi zao,wababa wanakwepa majukumu yao
 
Hata kabla ya ndoa kero tupu....! Mdada anataka kutoa gundu tu!
Yaah!wenyewe wanaita kaangalie mkato wa chumba ndio kutoa gundu huko kisha waoaji wengine watafuatia.Kuna baadhi ya jamii ni sifa kubwa kwa mwanamke alie olewa mara nyingi.Huku kuna baadhi ya jamii mwanamke alie zaa anakuwa na nafasi kubwa ya kuolewa kuliko ambae bado mwali huku utetezi ukitoka kuwa huyo tayari ameshihirisha ana kizazi.
 
Mie nilikuwa nakampango ka kuoa ila baada ya kuona mwenza hajui hata majukumu yake kama mama nimepata wasiwasi.Eti anadai kuwa dunia ya sasa hamna kazi ya mwanamke wala ya mwanaume hvo asipofanya shughuli flani basi mie niifanye. Duuh... Ndoa za sasa ni kichefu chefu
 

Kuna uzi niliuleta hapa, mtoto wa shost alikutana na boyfriend chuo kikuu, akawa mchumba hatimae mume. Wameanza maisha, baada ya kujifungua ndiyo kijana aliisoma number. Mke analoweka nappy za mtoto mpaka mume atoke kazini afue na kupika. Kijana alipopata upenyo wa kusepa hakugeuka nyuma.
 
Vipi ulishapata mtoto na yule shemeji wetu wa age 31
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…