Leo uzalendo umenishinda imebidi nilete kwenu wana JF hili suala. Nipo ndani ya ndoa miaka mingi na tumejaliwa binti mkubwa yupo sekondari. Mimi na wife tunashukuru mungu, wote ni graduates na tuna kazi nzuri tu.
Wife kwao wapo watatu yeye ndio wa kati. Kwao ndio msomi pekee huyo dada mtu kamaliza form IV zile ambazo ni kama la saba tu. Division four karibu na zero.
Amekuja kuolewa wakati wadogo zake wana watoto wakubwa na kwa maelezo ya wife mwenyewe mahari alitoa mwenyewe! Katika ndoa au mahusiano mengine mikwaruzo ya hapa na pale ipo lakini tunai solve bila shida. Lakini miaka hii mitatu imekuwa na mtihani sana.
Tatizo nimegundua hamna kitu wife anafanya bila kupata ushauri kwa dada yake. Nimegundua hata sms na email zangu ana zi-forward kwa dada yake. Kubwa yake nimegundua anajenga kisiri na kiranja wa mpango huo ni dada yake.
Tayari nyumba ipo kwenye lenta na nina picha ya kila hatua. Huyo dada mtu hapatani na mdogo wao maana yupo ngangari hakubaliwa kuingiliwa mambo yake na mumewe.
Tofauti na wife, za kuambiwa anachanganya na zake na kama jibu halimpi hakubali. Sasa imefika mahali najiuliza hivi nimeoa wangapi? Ni kama nakula chakula kisicho na ladha yoyote.
Mwisho nimekuwa mteja wa Massage Parlour moja kujiliwaza na sikosi happy ending hapo. Hapo Massage Parlour nimekuwa nikihudumiwa na binti mmoja tu. So far nime resist kuchukua number yake ya simu wala kumpa yangu.
Isingekuwa binti yetu, na jinsi mama mkwe anavyoniheshimu, ningekuwa nimeishamtema siku nyingi. Najiuliza mtihani huu hadi lini?