Ndoa ndoano, atapataje talaka yake?

Ndoa ndoano, atapataje talaka yake?

mamii1

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2015
Posts
286
Reaction score
126
Kuna malalamiko ya wanandoa, miaka 5 sasa kila mtu analala chumba chake. Mbaya zaidi wana mtoto wa miaka 6, mwanamke ameshachoka kuishi maisha ya jinsi hii.

Ndani ya miaka 5 hata kimwili hawajakutana, inaelekea mwanaume ana matatizo lakini hataki kukubali kama ana tatizo.

Mwanamke alichoamua ni kuachana, mume hataki waachane. Anadai ndoa ya kanisa huwa hawaachani.

Kitendo wanavyoishi ndani ya nyumba mwanamke anadai kitamuathiri mtoto, maana mtoto wa miaka 6 analala na mama tena wa kiume na huyo mumewe ana lala chumba kingine.

Je ni utaratibu gani afuate huyu mwanamke ili aachane na huyu mwanamme? Huyu mama ana miaka 32. Je mahakama inaweza kutengua hii ndoa?
 
huyo mtoto waliambukizana mimba au jamaa alisingiziwa!!?

sasa kinachompa shida nini? jamaa si ameamua kufanya yake na yeye afanye yake pia!!
 
Si aendelee na ustaarabu wake tu?

Ila walishakaa na kuzungumza? Kama wawili hawakufikia muafaka wazee wamehusishwa????
 
Ndoa bila kukutana kimwili haijakamilika bado. Watafute suluhu kabla haijazama kabisa...!
 
Miaka mi 5 na hakuna maridhiano kweli na wote si ni watu wazima, wajaribu counselling from professionals au walezi wa kidini
 
Mambo mengine yanchosha jamani mweh 5 yrs
 
mtoto alipatikanaje?

aende kanisani au mahakamani
 
mkuu hebu tuambie vizuri kabla ya hapo ilikuaje hadi kufikia hatua wakazaa mtoto ba sasa miaka mitano kila mtu na chumba chake ... tueleze vizuri.. ili tujue tunashauri wapi...
 
mtoto alipatikanaje?

aende kanisani au mahakamani

Walikaa vizuri mwaka mmoja hadi kutengeneza mtoto, baada ya mdada kuzaa mume akasema ampe mke muda wa kulea mtoto. Sababu mila za kwao mwanamke akizaa lazima watengane vyumba kwa miaka 3.

Mke alivumilia miaka 3, lakini mume akawa bado hayupo tayari. Wameshafanya vikao vya ndugu, kama ujuavyo wanashauri kuvumilia. Sasa mwanamke anadai haiwezekani huyu mume ana matatizo ndio maana anataka kutafuta talaka tu maana kachoka. Ila cha ajabu mume anagoma kwenda kufile talaka. Huyu mama yeye anataka legal talaka ili awe huru.
 
mkuu hebu tuambie vizuri kabla ya hapo ilikuaje hadi kufikia hatua wakazaa mtoto ba sasa miaka mitano kila mtu na chumba chake ... tueleze vizuri.. ili tujue tunashauri wapi...


Baada ya kuzaa,mume akadai ampe mke muda wa kulea sababu mila za kwao wanatengana chumba miaka 3. Lakini hata baada ya miaka 3 kupita yule mume bado harudi chumbani. Wamekaa vikao vya ndugu, ila kama ujuavyo mdada anaambiwa vumilia. Mdada kachoka maisha hayo ndio kaamua kuangalia kama mahakama inaweza kutengua ndoa. Inaelekea jamaa si mzima, cha ajabu mume hataki kusikia kuachana. Anadai bado mkewe. Mdada hajui aanzie wapi kwenda mahakamani, hajui taratibu.
 
Si aendelee na ustaarabu wake tu?

Ila walishakaa na kuzungumza? Kama wawili hawakufikia muafaka wazee wamehusishwa????

Wazee wamehusishwa,ila mdada anaambiwa vumilia. Mume hataki kuachana anadai yule bado mkewe.

Mke anataka waachane kisheria ili aendelee na life yake, mume hataki.
 
Sasa huyo dada anasubiri nini kuondoka?????
Hapo anazidi kujirudisha nyuma bila kujielewa.
Atoke hapo akajipange upya kimaisha.
Watu wengine wazito kufanya maamuzi magumu hadi kero.
Hicho cheti cha ndoa kinamtesa hivo, mmmh!!!!
 
Baada ya kuzaa,mume akadai ampe mke muda wa kulea sababu mila za kwao wanatengana chumba miaka 3. Lakini hata baada ya miaka 3 kupita yule mume bado harudi chumbani. Wamekaa vikao vya ndugu, ila kama ujuavyo mdada anaambiwa vumilia. Mdada kachoka maisha hayo ndio kaamua kuangalia kama mahakama inaweza kutengua ndoa. Inaelekea jamaa si mzima, cha ajabu mume hataki kusikia kuachana. Anadai bado mkewe. Mdada hajui aanzie wapi kwenda mahakamani, hajui taratibu.
Duuhh, Miaka 3 pasipo kukutana/kukaa chumba kimoja kisa mila, hapo ndio tatizo lilipoanzia. Kwa nini walienda kufunga ndoa kanisani huku wangali wanazikumbatia mila & desturi? Ninachoshauri awaone wana sheria wampe upenyo wa kisheria utakaomsaidia kupata talaka.
 
Wazee wamehusishwa,ila mdada anaambiwa vumilia. Mume hataki kuachana anadai yule bado mkewe.

Mke anataka waachane kisheria ili aendelee na life yake, mume hataki.

Si aende sasa mahakamani?

Au anasubiri mume akubali ampe lifti hadi mahakanai???
 
Huyo mwanamke atumie kigezo cha mila na desturi kama alivyotumia huyo mume wake awali. Kimila ndoa bila unyumba huwa wanaachana
 
5 years! mie siku 5 tu najiondokea zangu kujiunga na maisha ya u-single. watu wanazipenda ndoa as if ndo pumzi!
 
Back
Top Bottom