Jospina
JF-Expert Member
- Apr 19, 2013
- 2,421
- 1,395
Watu wote maana yake watu wote! Watu wakishakuwa na sifa ya kuwa wanandoa, kwa maana ya kupata kibali kwa wazazi na hatimaye mtu kukabidhiwa mke n.k. Ndoa hiyo inapaswa kuheshimiwa!
Hata kama aliyeoa au kuolewa alikuwa girlfriend/boyfriend wako kabla! Ikiwa mtu ameshaingia kwenye ndoa tu! Ni kama mwizi aliyekuwa anakimbizwa hatimaye kufanikiwa kuangukia mikononi mwa police! Bila kujali wa kwenye ndoa hiyo wanaendana au hawaendani, wafanana au hawafanani! Ikiwa ni ndoa tu! Basi! Wameingia kwenye sifa ya kupewa heshima na watu wote!
Wako baadhi ya watu! Hawaziheshimu ndoa za watu; na badala yake wanazivunjia heshima na kuziingilia! Na wengine wanawashawishi wanandoa hao; wafanye nao uzinzi kwa kuwarubuni kwa maneno au kwa vitu ili wawanase! Ndoa inapaswa kuheshimwa na watu wote! Usitumie matatizo ya ndoa za watu kuwarubuni watu!
Eti unasema!
(a) Akiwa na wewe atapata watoto tena wazuri..
(b) Akiwa na wewe utamuonyesha mapenzi ambayo hawezi kuyapata popote
(c) Utamuonyesha upendo ambao hajawahi kuuona
(d) Akiwa na wewe eti atazitimiza ndoto zake na aachane na choka mbaya
N.K.
Wanatumia matatizo yaliyopo katika ndoa za watu kama gia ya kuingizia mambo yao! Sikia wewe ambaye sasa hivi unajiona kama uko salama! Hauko salama hata kidogo! Ndoa inapaswa kuheshimiwa na watu wote! Bila kujali ni wapagani au wakristo au waislamu n.k. Ikishakuwa ndoa tu! Inapaswa kuheshimiwa na watu wote!
Wajomba na mashangazi na mawifi n.k. Ndoa inapaswa kuheshimiwa na watu wote! Ni agizo! Watu wote tunapaswa kuheshimu ndoa za watu! Kama wenyewe hawaziheshimu sisi haituhusu! Sisi tutii agizo letu ambalo tumeagizwa! Tuliishi hilo!