Ngoja nichangie bila kusoma mawazo ya wengine ili niwasilishe kile nnachokifikiri bila kuathiriwa na michango ya wengine,kisha ndo ntayasoma mawazo yao.
1.Makosa ya kwanza yanafanyika kwenye urafiki kabla hata ya hiyo ndoa.hapa nakusudia yafuatayo:
A.Hatuna tafsiri sahihi ya mume/mke mtarajiwa! Wengi wanadhani kila mpenzi anaekwambia nakupenda basi anaweza kuwa mume/mke. Si kila mwanamume ni mume, na si kila mwanamke ni mke. Tafsiri sahihi ya mume/mke mtarajiwa inategemea na wewe mwenyewe unataka mume/mke wa aina gani?na kwa ajili gani? Kila siku humu unaona watu wanasema mume pesa, kama unawaza mume ni pesa basi fahamu kuwa hiyo pesa ndio mzimu wa ndoa yenu, lazima itakutesa. Kama unadhani mke ni figa na makali.o makubwa basi jiandae kuteswa na hiyo figure.jiulize unataka mke/mume wa kuishi nae au wa kutoka nae out na watu wakwambie "yeeees umejua kuchagua"?, je unataka mwenza wako kwa kigezo cha dini? Awe na hofu ya mungu kwa vitendo? Je unataka mwenza "bongo fleva"?Ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu wenza walikosa vigezo sahihi vya kutumia wakati wa urafiki
B.kuna wakati tunafumba macho wakati tulitakiwa kuyafungua. Unaona wazi kuwa hamko compatible lakini unajidanganya eti atabadilika.
C.Tunaanza kuishi kama wanandoa kabla ya ndoa yenyewe! Hili lina athari kubwa sana ndani ya ndoa baadae, michepuko haitaisha, na thamani ya mwenza inashuka kwa sababu kama uliwahi kushawishika mkagegedana kwa mfano kabla ya ndoa then kwa mtu makini akikaa na kujiuliza ataona wewe ni cheap na yeyote anaweza kukushawishi hata baada ya ndoa na mkagegedana. Acha kugegedana kabla ya ndoa,jenga uthamani na heshima yako,hii itakusaidia sana ndani ya ndoa
D.Kuamini na kusimamia unachokiamini wakati wa urafiki.ni muhimu mwenza wako ajuwe misimamo yako kabla ya ndoa, usifiche makucha be real ili akiamua kuingia kwenye ndoa basi ajuwe wewe ni type gani. Ukificha makucha then ukaanza kuyatoa baada ya ndoa then hapo subiri majanga.
E.Kuwa na over expectation! Wengi wanakuwa na matarajio yaliyopindukia kabla ya ndoa, akiingia kwenye ndoa kisha akayakosa matarajio hapo kasheshe itaanza! Expect nothing and u will never be disappointed! Ichukulie ndoa kama kwenda nchi usiyoijuwa na tegemea hata usiyoyategemea.ukiwa open minded itakupa nafasi ya wewe kukabili changamoto kadri zinavyojitokeza.
nukta zote hapo juu zinahusu wote Ke/me
NGOJA NIPATE LUNCH KWANZA NTARUDI bi dada
#mimi49