Ndoa na changamoto zake,uvumilivu umeenda wapi?

Ndoa na changamoto zake,uvumilivu umeenda wapi?

Gorgeousmimi

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
9,296
Reaction score
7,713
Ni matumaini yangu pasaka inamalizika vizuri wana JF wenzangu.

Ndoa ni jambo la baraka kwetu na hata kwa mungu.Lakini hizi ndoa za siku hizi watu hawaishi kulalamika,si hapa JF tu hata in real lives,Naketi nikijiuliza tumekosa ustahamilivu na staha?Tuna itikadi ya kupenda attention ndio maana malalamiko hayaishi?au tunafunga ndoa na watu wasio sahihi?

Mfano mtu yupo kwenye ndoa lakini haishi kulalamika hana furaha kwenye ndoa yake na haoni umuhimu wa ndoa hio?Hivi mtu huyu anastahiki kweli kuwepo kwenye taasisi hio?Kwenye ndoa, furaha inatakiwa izidi machungu na si vice versa.

Kwa mtazamo wangu ni muhimu sana kufunga ndoa na mtu sahihi.Mwanzoni mwa ndoa shamrashamra zinakuwa nyingi na malavidavi yanakuwa yamenoga.Jinsi muda unavyokwenda ndipo uvumilvu na subira kwa wanandoa inapopimwa kwasababu ndio mnasomana kwa undani,kama kweli mnaweza kuhimili mikiki ya ndoa,ndoa ikiwa imefungwa katika misingi ya mapenzi ya dhati basi ndoa hio inaweza imudu changamoto tofauti.

Utajuaje kama upo na mtu sahihi?

Utajua kutokana na jinsi mnavyolenda,mkiwa na incompatibilities nyingi inabidi mkubali kujishusha au kujiadjust ili mkutane katikati,na kama hilo litashindikana basi bila shaka hamuendani.

Ni jambo la msingi kufahamiana vyema na mtu uliyefunga nae ndoa,nikimaanisha kufahamu background yake na background ya familia yake,ili hata kama ana background ambayo haikupendezei ujue jamii itakutazama vipi na utaweza kuvumilia changamoto zinazokuja na jambo hilo,kubali kasoro za mwenzako na uchunguze kama unaweza kuishi nazo.

Ukiwa kwenye ndoa ujue umeingia miguu yote mwili,sio mguu nje na mguu ndani,inabidi tujifunze kuhimili na kutafuta suluhu za changamoto tofauti hasa ndogondogo ambazo hazihitaji kuhushisha watu wengine zaidi ya wewe na mwenza wako.Tujue mipaka yetu,tusidhihakiane na kutukuanana mbele za watu baki hata watoto wetu,athari tunazowapatia ni zaidi ya maneno yanavyoweza kutafsiri.

Kama wasemavyo wengi haswa walonizidi,ndoa ipo complicated,kwahio ni vyema tukiingia kwenye taasis hii tuwe tayari kugive it all.
Au mnasemaje wenzangu?

Karibuni.
 
hili la ndoa no kweli linahitaji uvumilivu sana tu...lakini hili la mtu sahihi bado ni gimu sana kwangu kulimeza...lakini suala la kumtegemea mungu katika kudumisha mahusiano ni muhimu sana tu...
 
hili la ndoa no kweli linahitaji uvumilivu sana tu...lakini hili la mtu sahihi bado ni gimu sana kwangu kulimeza...lakini suala la kumtegemea mungu katika kudumisha mahusiano ni muhimu sana tu...
Ni kweli unayosema,ni muhimu kumtegemea mungu lakini mungu atakusikiliza dua na maombi ako pale na ww unapoonesha juhudi kwenye suala hilo,Ni kama una njaa kisha hufanyi jitahada zozote kupata mlo kisha unategemea mungu akushushie muujiza?
 
^^
Ndoa imetoboka mahali, hakuna namna njema ya kuhabarishana ndani ya mahusiano na taarifa zinazotolewa na kupokelewa tayari zinahisi zisizojenga.
Pili, jamii ya leo haimpi mwanandoa hofu ya kuacha wala kuacha. Mahusiano yaliyovunjika si jambo la kukemewa na jamii ila kuwa katika mahusiano ya kudumu (kwa uaminifu) ni ajabu!
Dunia imebadilika sana, ndoa haitakwepa mabadiliko haya.
Suluhisho nilionalo ni wanandoa kuingia katika ndoa wakiwa na ukomavu wa akili (matured couples) mimi49
^^
 
Last edited by a moderator:

Nina mfano dhahiri kabisa ya wanandoa waliokuwa matured kiumri na wanafanya mambo ya kitoto unaweza kushangaaa au hii inakuwa ni hulka ya mtu na mtu?
 
Last edited by a moderator:
Nina mfano dhahiri kabisa ya wanandoa waliokuwa matured kiumri na wanafanya mambo ya kitoto unaweza kushangaaa au hii inakuwa ni hulka ya mtu na mtu?

Umri mkubwa sio kuwa matured! It involves psychology, readiness, thinking, ability to make decisions etc
 
Umri mkubwa sio kuwa matured! It involves psychology, readiness, thinking, ability to make decisions etc
Sawa kama umri sio kigezo cha kuwa matured basi kuna watu hawatokuwa matured,mfano mtu ana miaka 47 anapiga mkewe,anamkashifu na kumtusi mbele za watu,Unadhani ni kwasababu gani?Kanyimwa busara?
 
^^
Ndoa imetoboka mahali, hakuna namna njema ya kuhabarishana ndani ya mahusiano na taarifa zinazotolewa na kupokelewa tayari zinahisi zisizojenga.
Pili, jamii ya leo haimpi mwanandoa hofu ya kuacha wala kuacha. Mahusiano yaliyovunjika si jambo la kukemewa na jamii ila kuwa katika mahusiano ya kudumu (kwa uaminifu) ni ajabu!
Dunia imebadilika sana, ndoa haitakwepa mabadiliko haya.
Suluhisho nilionalo ni wanandoa kuingia katika ndoa wakiwa na ukomavu wa akili (matured couples) mimi49
^^

..na pia mabaya/madahifu ya taasisi hiyo yanakuzwa mno, yanapewa uzito usiostahili na hali mazuri ambayo wanafurahia kutoka katika ndoa hizo hizo kwa kawaida hawasemi na hivyo vijana na hata watu wazima wengine huogopa taasisi hiyo. Hatukatai kuwa matatizo ya hapa na pale yapo sababu inahusisha watu wawili tofauti. lakini kama mimi49 ulivyosema, ni sahihi kabisa, uvumilivu na uelewa unahitajika pamoja na kumwomba Mungu kila siku muendelee kubebana kwa upendo
 
Last edited by a moderator:
Umeongea mazuri
Tatizo ndoa nying za siku hizi ni fashion only nimeolewa/ nimeolewa kukua kwa utandawazi kumetufanya tusahau mila ,desturi na tamaduni zetu watu wanaingia kwenye ndoa wakitarajia kukuta furaha wanasahau kuwa unatakiwa ujenge hiyo furaha yourself ndo uitumie...
Uvumilivu na usiri wa ndani ya nyumba hakuna jando na kufundwa kumepoteza maana jambo la siri mtu analileta Jf au kuelezea marafiki/ mashosti/bar wakati anakunywa anasahau kuwa kutoa siri na mumeo/ mkeo ni sawa na upo uchi cos nyie ni mwili mmoja.anashindwa kutafuta ushaur mzuri kwa walio wachache

Ishu ya background ni changamoto kubwa tunafahamiana kimjini na meno yet 32 tunapenda na kupeana mimba ndo wazazi wanapewa taarifa.still we fool our self na kusema ooooh mmi namfahamu ana tabia nzuri
Kakudanganya nani hujui background Yang wazazi,, magonjwa ya kurithi,tabia na malezi ya wazazi, na mengineo mengi

Kikubwa ni kumtegemea MUNGU na kuyaishi maandiko .tujitambue ndoa ni uvumilivu kujishusha, kujali, upendo na kutumia busara na hekima kwenye maamuz yoyote
 
Umeongea jambo la msingi sana ICHANA,mambo ya ndani ya ndoa yanatakiwa yawe siri ya ndani ya ndoa,chukulia mfano mtu haeshi kulalamika kuhusu ndoa yake,anamkandia mumewe sana,kisha wakipatana anarudi kwa yuleyule alokuwa anamuona nyoka walipokorofishana,Jamii itamchukuliaje muhusika huyu?Kigeugeu?Hajui anachotaka? haridhiki?
Hivi mfano mtu wa aina hio siku nyingine akileta malalamiko utayatilia manani kweli?
Na kuhusu background rafiki ni muhimu mno,imagine umeoa mke ambae alikuwa analala na kaka yake wa damu?Na mpaka wakati mpo kwenye ndoa anaendelea na kamchezo kake?Unafikiri mhusika huyo angelijua hayo mwanzo yangemkuta yalomkuta au angeendelea na uamuzi wake wa kumuoa mwanamke huyo?
 
Compatibility. Ndo siri ya ndoa tamu
Yessss The Boss,Mkiwa compatible inarahisisha mambo mengi,automatically kila kitu kitaflow kama inavyotakiwa kwasababu kuna maelewano na fikra chanya!Ni kama vile ukiwa umemkera mwenzako na ameshikwa na hasira na kuanza kugomba,unajishusha na kumpa nafasi sio na wewe unakuwa na mdomo mrefu!
 
Last edited by a moderator:
Umeongea jambo la msingi sana ICHANA,mambo ya ndani ya ndoa yanatakiwa yawe siri ya ndani ya ndoa,chukulia mfano mtu haeshi kulalamika kuhusu ndoa yake,anamkandia mumewe sana,kisha wakipatana anarudi kwa yuleyule alokuwa anamuona nyoka walipokorofishana,Jamii itamchukuliaje muhusika huyu?Kigeugeu?Hajui anachotaka? haridhiki?
Hivi mfano mtu wa aina hio siku nyingine akileta malalamiko utayatilia manani kweli?

Ndoa nyingi zinaharibika cos ya hakuna UVUMILIVU na USIRI
Mambo ya ndani jitu linaelezea utafikir ni katiba serial mbil or tatu.
Watu tumekosa hekima ya MUNGU twajidanganya kwa nguvu na akili zetu hatataweza lolote Bali tukiongozwa na MUNGU tutaweza
Mtu anatoa siri afu usiku unaenda kulala nae na kumuita honey huu ni uchizi.fikiri madhara kwanza ya kutoa siri ndo mana weng wanashauriwa vibaya cos tumechoka
 
Hakuna mteremko katika maisha,hakika kuna changamoto katika kila ndoa lakini watu huvumilia na kumezea,usione watu wanacheka na kufurahi usoni,wengi wana machungu mioyoni lakini wanastahamili na kutafuta suluhu!
 
It true what u have said mimi49 , labda kwa kuongezea tu is that change is the law of life, itsn't just abt kufunga ndoa na mtu sahihi but its also being the right person and pia wanandoa should understand kwamba with time; things,feelings etc change but its how u deal with the changes that matters.
 
Last edited by a moderator:
Kumtanguliza Mungu muhimu

Pia ni muhimu sana wanandoa wakijitambua. Na kujua wanapofunga ndoa kuna changamoto. Kuwa tayari kuzikubali

Mwanandoa usimfanyie yale mwenzio yake ambayo hutaki kufanyiwa

Kuyakubali mapungufu ya mwenzio

Ifanye ndoa yako kuwa mpya kila leo

Na changamoto za wanandoa hutatuliwa na wanandoa

Wote wawili mjue mna jukumu ka kuilinda ndoa yenu
Msimamie kiapo chenu
Muwe tayari kujishusha
Muwe tayari kupongezana au kuombana msamaha
Lugha za adabu
Kuheshimu na kuupenda upande wa mwenzio

Samahani pole hongera asante yatawalale nyumba yenu regardless of jinsia

Mheshimiane
Mpendane
Mthaminiane
Mjaliane

Ndoa sio kukata keki wala kufubgua champaign....
 
It true what u have said mimi49 , labda kwa kuongezea tu is that change is the law of life, itsn't just abt kufunga ndoa na mtu sahihi but its also being the right person and pia wanandoa should understand kwamba with time; things,feelings etc change but its how u deal with the changes that matters.
Wengi wapo stuck in time,wanafikiri kwamba yale malavidavi ya awali yataendelea forever,sisemi kwamba watu wasiendelee kupendana ni muhimu kupendana na kujaaliana na the positive thing is that with time you learn more about your fellow parter to know his/her likes and dislikes,so you can take even more consideration about how much care you should shower to this person.Ndoa ni kama maua,yanatakiwa yapaliliwe,yatunze ndo yanachanua…lakini hio ni topic nyingine….
 
Hakuna mteremko katika maisha,hakika kuna changamoto katika kila ndoa lakini watu huvumilia na kumezea,usione watu wanacheka na kufurahi usoni,wengi wana machungu mioyoni lakini wanastahamili na kutafuta suluhu!

Sio machungu tu mioyo inavuja damu imetoboka kuta zinaficha mengi sana
Zaman wazee walikuwa wamafichiana siri ya me/ ke anakuambia ni vibaya watu kujua madhaifu ya mwenzio walikuwa wanakufa na kamba shingoni kwa kutafuta suluhu taratibu na yenye hekima now days kitu kidogo mbona litakuwa tangazo madhaifu ya mwenzio.kila mtu ana udhaifu wake vumilia ...
Tabia ibadilike watu waheshimu ndoa na tuone aibu kutangaza siri za ndan .
 
Back
Top Bottom