Ni matumaini yangu pasaka inamalizika vizuri wana JF wenzangu.
Ndoa ni jambo la baraka kwetu na hata kwa mungu.Lakini hizi ndoa za siku hizi watu hawaishi kulalamika,si hapa JF tu hata in real lives,Naketi nikijiuliza tumekosa ustahamilivu na staha?Tuna itikadi ya kupenda attention ndio maana malalamiko hayaishi?au tunafunga ndoa na watu wasio sahihi?
Mfano mtu yupo kwenye ndoa lakini haishi kulalamika hana furaha kwenye ndoa yake na haoni umuhimu wa ndoa hio?Hivi mtu huyu anastahiki kweli kuwepo kwenye taasisi hio?Kwenye ndoa, furaha inatakiwa izidi machungu na si vice versa.
Kwa mtazamo wangu ni muhimu sana kufunga ndoa na mtu sahihi.Mwanzoni mwa ndoa shamrashamra zinakuwa nyingi na malavidavi yanakuwa yamenoga.Jinsi muda unavyokwenda ndipo uvumilvu na subira kwa wanandoa inapopimwa kwasababu ndio mnasomana kwa undani,kama kweli mnaweza kuhimili mikiki ya ndoa,ndoa ikiwa imefungwa katika misingi ya mapenzi ya dhati basi ndoa hio inaweza imudu changamoto tofauti.
Utajuaje kama upo na mtu sahihi?
Utajua kutokana na jinsi mnavyolenda,mkiwa na incompatibilities nyingi inabidi mkubali kujishusha au kujiadjust ili mkutane katikati,na kama hilo litashindikana basi bila shaka hamuendani.
Ni jambo la msingi kufahamiana vyema na mtu uliyefunga nae ndoa,nikimaanisha kufahamu background yake na background ya familia yake,ili hata kama ana background ambayo haikupendezei ujue jamii itakutazama vipi na utaweza kuvumilia changamoto zinazokuja na jambo hilo,kubali kasoro za mwenzako na uchunguze kama unaweza kuishi nazo.
Ukiwa kwenye ndoa ujue umeingia miguu yote mwili,sio mguu nje na mguu ndani,inabidi tujifunze kuhimili na kutafuta suluhu za changamoto tofauti hasa ndogondogo ambazo hazihitaji kuhushisha watu wengine zaidi ya wewe na mwenza wako.Tujue mipaka yetu,tusidhihakiane na kutukuanana mbele za watu baki hata watoto wetu,athari tunazowapatia ni zaidi ya maneno yanavyoweza kutafsiri.
Kama wasemavyo wengi haswa walonizidi,ndoa ipo complicated,kwahio ni vyema tukiingia kwenye taasis hii tuwe tayari kugive it all.
Au mnasemaje wenzangu?
Karibuni.
No comment