Ndoa-mtihani

Ni mtihani kama ilivo mitihani mingine ya maisha
 
Mitihani yote ya ndoa utaishinda endapo utakuwa na uvumilivu.
 
Mitihani yote ya ndoa utaishinda endapo utakuwa na uvumilivu.
Hakuna anayeingia kwenye ndoa akiwa amedhamilia, hasiwe mvumilivu. Labda kizazi hiki cha dot.com wanaolewa fashion mara kutoa mikosi n.k.
Shida kubwa inakuja pale ndoa inapokuwa mzigo na utumwa kwa upande mmoja na majaribu yaliyozidi mipaka!
 
Hii kali!ila jitahidi shule hiyo isikushinde!

 
Silaha ya ushindi katika ndoa ni upendo wa dhati, uvumilivu, kuchukuliana, kuaminiana na kusameheana. Ikumbukwe kwa wanandoa kuchukuliana madhaifu yao, kusuluhisha mambo yao wenyewe bila kushirikisha marafiki (maana hawa ni wapotoshaji sana), wazazi au ndugu. Na pia ili ndoa idumu wote wanandoa waepuke kusikiliza maneno ya watu kwani sio wote wanaofurahi kuona meli ya wapendanao ikielea baharini maana watafanya kila njia waifupishe safari. Nahodha wa meli ya wanandoa iwe ni nyie wanandoa wawili tu, hapo lazima cheti cha ushindi wa ndoa kiwe chenu!!
 

mwenzangu upendo wa dhati, uvumilivu, kuchukuliana, kuaminiana na kusameheana kuna kiasi, lakini ndoa nyingi za sikuhizi ambazo naona watu wanaomba ushauri,utasikia mtu anasema mwanaume kila siku anarudi either usiku wa manane au asubuhi, kipigo, haki ya ndoa hatoi (sex) ndani ya nyumba haachi hata senti, sasa hapo kuna uvumilivu kweli? kwanza huwa najiuliza mtu anaombaje ushauri katika swala kama hilo hivi kweli hapo unasubiri tukwambie ondoka?
 
Naomba kukuuliza swali mtoa mada,wewe umeolewa?ni vizuri ushauri atoe mtu amabe yupo ndani ya ndoa si mtu hajawahi hata kuchumbiwa anawaambia wenzie ndoa ndoano..we umejuaje ndoano?ushauri atoe mwenye experience tena yenye miaka si miezi....
 
Ushauri mzuri siku hizi watu hawapigi tena wake zao, kuna sheria inalinda sana wanawake, suala la kurudi usiku wa manane au hata asubuhi kama umemuuliza bado hajirekebishi, umempeleka kwa wazazi, ndugu na bado hajirekebishi, kikubwa cha kufanya ni maombi tu, usimuulize tena chochote, mpe huduma zote kama mume, mwachie chakula kama kawaida hata kama hatokula, funga na omba kwa ajili ya Mungu ambadilishe mume wako, maana katika maandiko matakatifu yanasema 'Mwanamke atamlinda mume wake', na nina amini ukimwomba na kumlilia Mungu ukiwa umesimama (hapa hakuna cha kuwa na kidumu cha kukupooza moyo, kidumu chako kiwe ni Mungu na Maombi) nina hakika atajirekebisha tu. Mungu ni mwaminifu siku zote atakurudishia mume wako tena akiwa amebadilika, au Mungu atamchapa kiboko ambacho kitamfanya ajute aliyokuwa anakutendea. Kikubwa kwa wanawake usilipize kwa kuwa na spare tyre, hii itamfanya akimbie zaidi badala ya kurudi asubuhi basi atarudi baada ya wiki au hata mwezi tena kuja kubadili nguo tu. Ushindi katika maisha ni maombi tu. Nimeongea hivi maana nipo kwenye ndoa huu mwaka wa 19. Milima nilipanda, mabonde nilishuka lakini kwa maombi sasa hivi nipo kwenye tambarare kama vile ndo tunachumbiana, ila kitu kizuri kina gharama, ili ndoa isimame na iwe tamu ni kwa maombi, wanawake tusimame kwenye zamu zetu sawasawa, hawa waibjai wa ndoa za watu hawatomwona mume wako. Ni ushauri tu nimetoa.
 
formula ya kushinda mtihani wa ndoa ni 1+1=1
 
Aisee dada yangu sijui kama ulipitia katika hayo niliyoandika au vipi lakini kama ulivumilia hayo hongera sana, ndoa yangu bado changa sana so siwezi kusema sana ila namshukuru Mungu mume wangu ananipenda na kunijali sana sometimes naona kama vile Mungu alinipa mtu kutokana na mimi nilivyo kwa kuwa mimi uvumilivu huo sina dada yangu ikitokea akabadilika akawa hivyo sidhani kama kutakuwa na ndoa tena ntampisha tu tena wala sihitaji kidumu wala spare tyre nitaishi mwenyewe kwani maisha si kuwa na mwanaume tu, kama ni maombi naomba sasahivi kwamba Mungu aendelee kutulinda na atuepusha na vitu kama hivyo, lakini akibadilika akawa gume gume atajiombea mwenywe
 

Hivi ni kweli why upewe Cheti kabla????????
 
kula like kuubwa! Hongera sana kwa kushinda yote,ni kweli usemayo ushauri unaposhindikana maombi ni silaha tosha,ubarikiwe mama tuombee na sisi tushinde.
 
ndoa nyepesi ikiwa utasimama katika misingi yake ipasavyo....
 
majibu yake mengi yako wazi...

tatizo ni application tu...

ndoa si ngumu... wagumu ni wanandoa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…