ipo siku huyo m.me atashtuka tu,huwezi kumdanganya m.me kwa muda mrefu hivyo.hata awe zoba kiasi gani.za mwizi arobaini,au huyo mwanamke ndio mlishaji kwa huyo mume ambae hajui?na hiyo si ndoa,huyo mwanamke anaidanganya nafsi yake
ipo siku huyo m.me atashtuka tu,huwezi kumdanganya m.me kwa muda mrefu hivyo.hata awe zoba kiasi gani.za mwizi arobaini,au huyo mwanamke ndio mlishaji kwa huyo mume ambae hajui?na hiyo si ndoa,huyo mwanamke anaidanganya nafsi yake
mnh mie siamini kwa mwanamke unaweza olewa mara mbili,na waume zako wasijue kama wako wawili....acha kutupima bana.:twitch::sick:
Mimi bado haijaingia akilini vipi aweze kumudu ndoa mbili bila mmoja wa kwanza kushtuka.
Kama ni kweli nadhani pamoja na makosa ya huyo mama mume wa kwanza naye anamatatizo ya kimaono juu ya mkewe, pia mme wa pili ndio hamna kitu kabisa yaani unaoa mke na unajua ameolewa na unakubali kuwa atawafanyia zamu za kulala, na hapo yeye wapili ndio atanyanyasika zaidi maana anajua anaiba hata akiambiwa tulia mwezi huu siji maana naona kama anastuka itabidi akubali.
Hapa tutamlaumu sana huyu mama lakini stori hii inaonyesha udhaifu mkubwa kwa sisi wanaume, na katika hili ntasimamia kuwa wanaume ndio chanxo cha kupelekea huyo mama kufanya hivyo maana kama mmojawapo angekuwa strong naamini yasingetokea hayo yote
Asante mkuu. So tumshauri je? kwa mwonekano wa nje naona mwanaume wa kwanza yuko fiti, ila sisi watu wa nje hatujui kama yuko strong au vipi! Lakini hivi ni sababu kama zipi zinamfanya mke aamue kuolewa nje??????? Tamaa?? Kukosa huduma ya kimapenzi kwa mumewe?? Au ni nini??
Kuna mama mmoja ameolewa kwa ndoa ya kiislamu. Ana watoto wawili. Mtoto mmoja wa kwanza kamzaa na mume wake wa Kwanza, mtoto wa pili kamzaa na mume wake wa Pili. Huyu mwanamke anafahamika kabisa katika familia zote za wanaume hao. Na anaheshimika kama mke halali. Wazazi wa familia ya mume wa Pili wanamfahamu lakini hawafahamu kuwa ameolewa sehemu nyingine. Mume wa pili anajua ameoa mke wa mtu na yuko comfortable lakini mume wa kwanza hajui lolote. Huyu mwanamke anaamua wiki hii aende kwa mume mmoja. Sehemu moja anadanganya kuwa, mfano: Nasafiri kikazi, mara leo nimefanya kazi hadi asubuhi n.k. Lakini hasa mume wa kwanza ndiye anadanganywa make hajui kuwa mkewe amelowa kwa mume mwingine. Binafsi nimemshauri amwache huyo mume wa Pili na kama ikibidi amweleze mume wake wa Kwanza kuwa mtoto wao wa Pili siyo wa mume huyo wa Kwanza, ili apelekwe kwa mume huyo wa Pili na ikibidi aachane naye kabisa lakini amegoma kabisa kusikiliza ushauri wangu. Jamani wanaJF (hasa akina dada)mnatoa ushauri gani kwa huyo mwanamke mwenzenu??? Toeni ushauri wenu nitaufikisha sasa hivi kwake. Ahsanteni!!