NDOA: Kwanini wanawake hutumia unyumba kama silaha?

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410


nosex.jpg


Imezoeleka na kuonekana kuwa wanawake wananyanyaswa na wanaume hasa linapokuja suala la uaminifu wa mapenzi.

Mbali na hayo wanawake pia wamekuwa wakibakwa na waume zao wa ndoa kwa maana ya kuingiliwa bila ridhaa yao. Katika hilo wanaume nao wanalalamika wanawake kutumia unyumba kama silaha wanapokosewa na wenzi wao.

Imezoeleka na kuonekana kuwa wanawake wananyanyaswa na wanaume hasa linapokuja suala la uaminifu wa mapenzi. Mbali na hayo wanawake pia wamekuwa wakibakwa na waume zao wa ndoa kwa maana ya kuingiliwa bila ridhaa yao. Katika hilo wanaume nao wanalalamika wanawake kutumia unyumba kama silaha wanapokosewa na wenzi wao.

Ikitokea mwanaume amefanya kosa, mwanamke hukaa kimya na kusubiri aombwe unyumba ili akatae , akitumia hatua hiyo kama adhabu kwa kitendo alichotendewa. Hamisi Kizugu anasema kuna vitendo vinavyofanywa na wanawake vinamkera, lakini hiki kinamkera kwa asilimia 100.

Anasema raha ya mapenzi ukifika kwa mkeo ujiachie na kama umekosea akuambie lakini kusubiri wakati unamhitaji kupita maelezo halafu anadengua huwa inamkwaza.

Anafafanua akiwa na umri wa miaka 22 alioa na kudumu na mkewe kwa miezi sita kutokana na tabia yake ya kumnyima unyumba kila anapotaka afanyiwe kitu. Anaeleza mwanamke huyo alikuwa akitaka nguo, viatu kusafiri kwa sababu alikuwa anapenda safari, alikuwa anamnyima unyumba na kumpa masharti kuwa akimpa ampatie anachotaka au amruhusu kufanya anachotaka.

Kizugu anasema alivumilia na kujitahidi kuwa mtumwa wa penzi la halali, akashindwa “Nilishindwa nikaona isiwe tabu, kuku wangu mwenyewe yupo tunduni lakini bado natakiwa kutumia chenga za mchele kumnasa, nilishindwa nikamuacha, ”anasema Kizugu.

Mkazi wa Tabata Segerea, Andrew Charles anasema anakerwa na tabia ya mkewe wakikosana kidogo hupanda kitandani na nguo akiwa amejipanga kumkwaza anapomuhitaji. Anasema atafanya hivyo kwa muda na kila unapofika usiku anapata wakati mgumu wakati wa maandalizi huku akikatalia na akishindwa huamua kumuacha na kulala akiwa na donge moyoni.

“Akicheka namtizama kwa sababu nafahamu nikikosea kidogo anavaa nguo tena wakati mwingine suruali na hufanya hivyo hata kwa makosa yake, nikimsema kama amekosea basi nijue siku hiyo kazi atanionyesha muda wa kulala ukifika anajiandaa kama anakwenda kulinda hivyo anajizuia na mbu, ” anasema Charles huku anacheka.

Charles anasema anakereka sana na tabia ya kutumia unyumba kama silaha, na anaona athari ya hayo mambo ni ndoa kuvurugika. “Nilimkanya kuhusu kulala mzungu wa nne kila anapochukia, akaona tulale upande mmoja lakini avae nguo na kuninyima unyumba, ” anasema.

Naye Imelda William mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam anasema amewahi kufanya hivyo mara kadhaa kutokana na kukosa cha kujitetea na kitu pekee alichonacho na anachoweza kujivunia ni hicho.

Anasema amekuwa akikuta ujumbe mfupi wa mapenzi kwenye simu ya mumewe kutoka kwa wanawake wengine, kila anapouliza hakuna majibu ya maana anayopewa zaidi ya kufokewa, hivyo haoni haja ya kushiriki tendo hilo na mumewe.

Imelda anaongeza kuwa wakikorofishana na mumewe huwa anamtakia kauli za dharau na kejeli, kitu kinachomtia hasira na kuona hakuna haja ya kukutana na mtu kama huyo.

“Anachofanya ananidhalilisha na baada ya saa mbili au tatu anataka nikutane nae kimwili tena kwa mapenzi haiwezekani na nimechoka kuwa mtumwa wa ngono na kumfurahisha yeye, ndiyo maana nakataa, ”anasema. Chiku Mhagama mkazi wa Kigogo Sambusa jijini Dar es Salaam anasema miongoni mwa sababu zinazomfanya atumie unyumba kama silaha ni kukosa la kufanya pindi mumewe anapomuudhi.

Anasema hawezi kumpiga, hawezi kumnyima chakula kwa sababu anakinunua mwenyewe kitu pekee anachoweza kufanya ni kutofanya nae tendo la furaha ambalo ni hilo ili kuonyesha hasira yake.

Anafafanua na akifanya hivyo ndiyo mumewe hufahamu kama amekasirika na hata kumuuliza “Umenuna, lile jambo dogo tu, halijaisha basi yaishe”. “Haniombi msamaha hadi nimnyime unyumba, anapohitaji anakuwa mpole na mnyenyekevu, nikimpa jeuri ipo pale pale , natumia mbinu hiyo kujifariji kwa sababu hunifanya nijione na mimi nina kitu cha thamani,” anasema Chiku.

Chiku anafafanua kuwa anafahamu madhara ya kufanya hivyo ikiwamo kuchangia mwanaume kutafuta mpenzi mwingine akiona kero hiyo inazidi, lakini hana jinsi.

Husna Kibalata anasema miezi kadhaa iliyopita alikuwa kijijini alikopelekwa na mumewe kama adhabu na kufundwa upya kutokana na kupenda kutumia tabia hiyo kama silaha. Anasema mumewe alipata mwanamke na ikawa hafichi tena kila alipomkatalia humpigia simu huyo mwanamke na kuzungumza naye kwa nguvu mbele yake, aliposhindwa kuvumilia akaanzisha ugomvi uliosababisha arudishwe kijijini kwa wazee.

“Baada ya wiki mbili mume wangu alikuja na kueleza kwa nini aliamua kufanya hivyo na kumtaka bibi yangu anielekeze madhara ya kumnyima mume unyumba.

“Aliniomba radhi na kusema yule mwanamke aliyekuwa akizungumza nae alimpanga ili kunitia adabu, nami nimemuomba msamaha na sitorudia tena hata akiniudhi kwa sababu ndoa yangu imenusurika kuingiliwa na kidudu mtu, ” anasema Husna.

Mtaalamu wa saikolojia, Dk John Haule anasema mwanaume na mwanamke wana tofauti kubwa katika maumbile, jambo la msingi kwa wanandoa ni kuzifahamu tofauti hizo ili waishi kwa amani. Anasema licha ya kuwapo tofauti nyingi za kimaumbile kubwa ni hiyo inayoleta mgogoro ya kukutana kimwili.

Anafafanua kuwa mwitikio wa mapenzi kwa mwanaume ni wa haraka zaidi kuliko mwanamke. Mwanaume huweza kusisimka kwa kuona tu uzuri wa mwanamke wakati mwanamke huathirika zaidi kimapenzi kwa kuguswa na kusikia yale anayosikia kutoka kwa mwanaume.

Hivyo anaposikia amenenewa mabaya, au akiamini yaliyonenwa dhidi yake ni dharau, kejeli inakuwa ngumu kushiriki tendo hilo. “Unaweza kuona idadi kubwa ya wanawake wameathirika na kudanganywa na wanaume, wakati mwingine kwa marudio yaani aliwahi kumdanganya akamtenda, lakini akipanga maneno anaweza kumdanganya tena.

“Hii inatokana na hisia zao za mapenzi kuwa ni kwa kuguswa au kusikia maneno mazuri, ikiwamo ya kuwasifu, ”anasema Dk Haule huku akikataa kutaja hospitali anayofanyia kazi kwa madai kuwa siyo msemaji wa hospitali hiyo.


Chanzo: Mwananchi
 
Wanachokifanya wakinamama ni kutaka kuonyesha kwamba sio wanyonge wakati kiuhalisia wanajiona wanyonge
Si kitendo kizuri japo kwa wanaume creative na ambao hawana hasira za mapema huwa halikuwagi tatizo maana anakuwa anajua kwamba wanawake pia huwa wanahitaji huduma
NB: Ni vyema kama kuna ugomvi muumalize kabla ya kupanda kitandani si vyema kutafuta mtoto mkiwa mmenuniana mkizaa jambazi sijui mtamsema shetani!!
 
Hii njia yao inakera aisee..Ukiwa na mwanaume mwenye hasira za karibu mnaweza mkawa mnagombana deile
 
Ukinibania miguu naenda kutafuta mwingine aliyekuwa tayari tu, kwani unayo peke yako mpaka tubembelezane?
 
sasa umetoa KOFI kubwa hata sekunde haijaisha unataka sex,,,,,,, wanawake wanafanya kazi nying hasa ofisni na za nyumban ndo balaa tofaut na mwanaume--------
yeye ni ofsn tu,,,,,, matokeo yake wazo la sex halipo na ukimgusa lazma atakuw kachoka,,,,,,, wanaume wanaopnga hi kitu ebu tuwape madaraka yote ya wanawake alaf muone km unyumba mtakuwa mnanyimwa.
 
Si hivyo tu... huwa poa kosa moja lina mlolongo wa adhabu... sex hupati, hakusemeshi, kama ni pasi hatapiga, lama ni chai hatandaa, chakula dada wa kazi au watoto ndo wataandaa... full adhabu
 
Mh kwakweli hii mada du. Ila wanaume wakumbuke matamanio ya sex yanatofautiana mwanamke anasababu nyingi za kumfanya ataman kufanya sex mwanaume yeye sio nyingi. Angalia unaishije na mkeo unamfurahisha namna gan unampa nafasi namna gan unapokosea unamalizqje. Caring ya mwanaume kwa mwanamke ndo inamfanya mwanamke apate ham ya kufurahia tendo. Sasa wewe umemtibuq huko unakuja na basi yaishe afu baada ya dk Tatu naomba mamiii hiyo ham aitoe wapi. Hebu jaribu kumpenda mkeo weka attention nae unafanya kazi sawa umerudi ukaribu wako kwake uko vip. Ukimjali mwanamke sa nyingine Ni rahis kusamehe Ila ukiendekeza ubabe atagoma akikubali Ni anatega ufanye umalize na ukiendekeza Hilo watakusaidia si bure
 
Mh kwakweli hii mada du. Ila wanaume wakumbuke matamanio ya sex yanatofautiana mwanamke anasababu nyingi za kumfanya ataman kufanya sex mwanaume yeye sio nyingi. Angalia unaishije na mkeo unamfurahisha namna gan unampa nafasi namna gan unapokosea unamalizqje. Caring ya mwanaume kwa mwanamke ndo inamfanya mwanamke apate ham ya kufurahia tendo. Sasa wewe umemtibuq huko unakuja na basi yaishe afu baada ya dk Tatu naomba mamiii hiyo ham aitoe wapi. Hebu jaribu kumpenda mkeo weka attention nae unafanya kazi sawa umerudi ukaribu wako kwake uko vip. Ukimjali mwanamke sa nyingine Ni rahis kusamehe Ila ukiendekeza ubabe atagoma akikubali Ni anatega ufanye umalize na ukiendekeza Hilo watakusaidia si bure
Kwell kbs
 
sioni cha kuchangia ila wanawake nao wameshajua udhaifu wetu hivyo wanatumia hicho kama kiboko cha kutuadhibia
 
Aliyekuwa mke wa mzungu alitupa somo kuhusu hili title ni 'The Power of P...y'.
 
Back
Top Bottom