Milale
JF-Expert Member
- Aug 29, 2013
- 494
- 189
Habar zenu wana Jukwaa la MMU. Naomba niwaletee huu mkasa wa kaka yangu ambao unaendelea katka ndoa yake. Miaka minne iliyopita alioa mwanamke wa kigoma wakabahatika kuzaa mtoto mmoja ila kulingana na visaa vya yule mwanamke ndoa ilivunjika baada ya mwaka 1na nusu, ikabidi jamaa akae single kwa muda wa miaka 3. Akaona kuwa si vema kuishi mbali na mwanae ikabidi arudi kigoma kwenda kumchukua tena yule mwanamke na kuja nae tena hapa dar, walipofka hapa dar vituko vilianza upya mwanamke akawa hataki kabsa kumsikiliza mwamaume ikawa kila siku ugomvi. Mwanamke akapata ujauzito ugomvi ndo ukazidi mara dufu jamaa ikafikia hatua akapelekwa polisi na yule mwanamke. Alipoona ugomvi unazidi ikabidi ampeleke kwa mama yake yaani mama anayetuzaa na kaka yangu. Alivyomfikisha huko ndo matatizo yakazidi ikafikia hatua anatishia kujinyonga, ikafikia hatua yule mwanamke anamtukana kabsa mzazi wetu,. Mzazi kuona hivyo akasema kuwa kashindwa kwa hiyo kaka yangu akamuchukue mke wake, ikabidi kaka atume nauli ili yule mwanamke arudi dar. Kwahiyo kwa sasa yuko njia panda akikumbuka vituko kutoka kwa yule mwanamke, anaomba ushaur umrudishe kwao kigoma. ilihari ni mjamzito au aendelee kuvumilia maumivu anayoyapata kutoka kwa huyo mwanamke. Ushaur wako ni mhimu sana ili niweze kumsaidia mawazo maana tuko njia panda.