Ndoa Inavunjika Hiyo!

Bazazi

JF-Expert Member
Aug 18, 2008
2,806
3,476
Waungwana, Bazazi kasimuliwa na mdau wake jinsi ndoa yake inavyoyumba. Kafumania simu ya mke ikiwa na sms za wasap na za kawaida. Anawasiliana na mpenzi wake wa pili baada ya kiwambo kuondolewa. Ni sms za mahaba hasa tena mazito. Mume kambana mkewe, mke hafunguki. Ana ahidi atavunja mawasiliano lakini havunji (mgogoro umeanza Augost '19)

Hasira za mume zimejaa na kufurika baada ya kuona wasap sms ya mchepuko inayoonesha mke anataka kuvunja ndoa. Mke anabembeleza warudishe majeshi ili wawe pamoja lakini mwanaume hataki (anakwepa majukumu labda wakati alikuwa anamega kisela). Anamshawishi ugomvi na mumewe waumalize kwani wao walikuwa childhood friends tu na kwasasa hawawezi geuza lolote na itakuwa ngumu wao kuwa pamoja. Mwanaume ni Mhadhiri Mwandamizi wa Shule ya Sheria ya UD. Mume ana Uzamili ilhali mke ana Shahada.

Hizi ndoa ni changamoto kuu ktk maisha. Ndoa ya miaka zaidi ya 15 yenye watoto leo inatembea ktk uzi mwembamba uliooza. Nimeamini kuoa mwanamke aliyebikiriwa ni KUOA MKE WA MTU.

NB: Kinachomshangaza Bazazi ni kuwa msomi wa sheria hajui kuwa ni kweli Ugoni ni kesi ya MADAI kwa sheria za nchi lakini ni JINAI kwa sheria za Kitaa? Kweli Plato alisema sawa "Love is a serious mental disorder problem"

Bazazi
 

Attachments

  • IMG_20190908_061505.jpeg
    IMG_20190908_061505.jpeg
    115.3 KB · Views: 98
Back
Top Bottom