Ndoa huvunjwa kwa vitu vitatu.

Ndoa huvunjwa kwa vitu vitatu.

jf user

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2018
Posts
777
Reaction score
625
Nimekua nikiona talaka zikitolewa hovyo hovyo kwa sababu mbalimbali mimi nataka niwaambie kama ulitoa talaka au wewe mwanamke kudai talaka bila hizi sababu tatu basi ndugu yangu unazini, talaka hutolewa na mwanaume kwa hizi sababu tatu na sio mwanamke hilo jukumu sio lenu.
Ndoa huvunjwa kwa vitu vitatu!

1/Kama mwanamke atamsaliti mumewe
Hii imeandikwa iwapo mwanaume atagundua mkewe kamsaliti basi anaruhusiwa kutoa talaka na kumuacha mwanamke huyo aende zake. Mathayo 19:7-9.
Pia soma Kumbukumbu la sheria 24:11-4, Marko 10:1-12, Mathayo 5:31-32

2/Kama mwanamke ni mchawi.
Hapa MUNGU katuruhusu wanaume kutoa talaka kwa wake zetu kama tutagundua ni wachawi! Pia kabla ya Yesu wanawake wachawi walikua wakipigwa mawe hadi kufa ila kwa sasa sheria zimelegezwa.

3/Kama mwanamke ni wa imani nyingine. Ila hii ni kwa mujibu wa maneno ya Paulo mwenyewe sio Yesu! soma 1 Wakorintho 7:12-16
Kwenye agano jipya Mtume Paulo (Kwa maneno yake sio Bwana) anasema iwapo mwanamke atakuwa sio mkristo au ni wa imani nyingine anaweza kuomba talaka kwa mumewe na kuachwa kwa hiyo mwanamke huyo yupo huru kuolewa tena.

4/Kifo cha mume, Warumi 7:2-3.
Mwanamke atakua huru kuolewa tena iwapo mumewe atakua kafariki. Anaweza kuolewa tena kama sio mzee maamuzi ni ya kwake.

MASWALI
1/Nyinyi wanawake mnapata wapi uwezo wa kuwacha waume zenu wakati mwanaume ndie anaetoa talaka tena kwa sababu maalumu 1-3 kama nilivyoweka hapo juu? Wewe mwanamke una akili timamu eti unasema umemuacha mumeo? kwa sheria zipi za MUNGU? Enyi wapotovu acheni kujidanganya kwani shetani kawatawala mpaka kila kisichofaa mnaona kinafaa.

2/Nyinyi watumishi wa MUNGU mnaotoa hati ya talaka mna wazimu?
Napenda sana wakatoliki kwa sababu mambo ya ni strictly yani hamna mchezo mchezo aisee ni mwendo wa sheria na vifungu tuu kama vilivyoandikwa kwenye biblia. MUNGU hapendi talaka sasa wewe unaetoa talaka tena kwa sababu ambazo hazijaainishwa ni mwenda wazimu tena kiongozi wa MUNGU hakika wahitaji maombi. Talaka hazitolewi kama karanga sokoni bali ni swala gumu sana ndio maana MUNGU mwenyewe anakataa na ole wake asababishaye talaka MUNGU anajua haki yake astahiliyo.

3/Suala la ndoa n suala la kiimani sio suala na NGO an serikali.
Sheria za kidunia ni tofauti kabisa na sheria za MUNGU. Ingefaa sheria za NGO na sheria za serikali ziendane moja kwa moja na sheria za dini ya mhusika eitha mkristo au muislamu vinginevyo ni batili. Talaka ni jambo gumu haliendi kidunia bali lipo kiimani zaidi.Kwa hiyo siamini katika vikundi mbalimbali vya kutetea haki za wanawake(NGOs) au serikali labda sababu zao ziwe automatically na za MUNGU.

NB: Nyinyi wanawake acheni kujidanganya pia mkae mbali na hao wanaowadanganya habari za talaka haziendi hivyo. Huko kujidanganya, kutenda dhambi na kumkufuru MUNGU.Sasa wewe ndugu yangu uliedai talaka kwa sababu za kipuuzi ambazo hazijaainishwa kwenye biblia au kitabu chako cha dini ukatubu mapema kabla MUNGU hajakuadhibu kwani talaka yako ni batili.
 
3/Kama mwanamke ni wa imani nyingine.
Kwenye agano jipya MUNGU anasema iwapo mwanamke atakuwa sio mkristo au ni wa imani nyingine anaweza kuomba talaka kwa mumewe na kuachwa kwa hiyo mwanamke huyo yupo huru kuolewa tena.

Naomba reference inayosupport [emoji115][emoji115]
 
akikupa nijulishe
 
Soma 1 Wakorintho 7:15

Ila haya ni maneno ya Paulo sio Yesu unaweza soma zaidi 1 Wakorintho 7:12-16
Cc lolipo
 
Point 3 za mwanzo zote zinamaana moja.
1.Kama mwanamke atamsaliti mumewake.Ki bibilia mwanamke ni kanisa(waumini) mume ni Yesu mwenyewe.Usaliti hapa nikufuata miungu mingine kama ulivyo orodhesha ktk point no 2 na 3.Mfano no 2 uchawi,hapa tiari umemsaliti Mungu(mume) kwakujinajisi na miungu mingine.
no3 imani nyingine hapa napo niusaliti kwa Mume(Kristo)mana kuwa na imani nyingine nikutokuwa na imani na Mungu
 
MSISITIZO UPO MSTARI WA 7-9
Marko 10

2 Baadhi ya Mafarisayo wakamjia wakitaka kumtega, wakamwuliza, “Ni halali mtu kumwacha mke wake?”

3 Yesu akawajibu, “Musa aliwaamuruje?”
4 Wakamjibu, “Musa aliruhusu kwamba mume anaweza kumwandikia mkewe hati ya talaka na kumwacha.”

5 Yesu akawaambia, “Musa aliwaandikia sheria hiyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu.
6 Lakini tangu mwanzo wa uumbaji, ‘Mungu aliwaumba mume na mke.
7 Na kwa sababu hii mume atamwacha baba yake na mama yake na hao wawili, watakuwa mwili mmoja.’
8 Kwa hiyo hawatakuwa wawili tena bali mwili mmoja.
9 Basi, alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.”
 
3/Kama mwanamke ni wa imani nyingine.
Kwenye agano jipya MUNGU anasema iwapo mwanamke atakuwa sio mkristo au ni wa imani nyingine anaweza kuomba talaka kwa mumewe na kuachwa kwa hiyo mwanamke huyo yupo huru kuolewa tena.

Naomba reference inayosupport [emoji115][emoji115]
Wee ni kiboko, unafaa kuwa mtume na nabii wa uongo wa kizazi chetu.
 
Point 3 za mwanzo zote zinamaana moja.
1.Kama mwanamke atamsaliti mumewake.Ki bibilia mwanamke ni kanisa(waumini) mume ni Yesu mwenyewe.Usaliti hapa nikufuata miungu mingine kama ulivyo orodhesha ktk point no 2 na 3.Mfano no 2 uchawi,hapa tiari umemsaliti Mungu(mume) kwakujinajisi na miungu mingine.
no3 imani nyingine hapa napo niusaliti kwa Mume(Kristo)mana kuwa na imani nyingine nikutokuwa na imani na Mungu
One love bro nimekusoma.
Kama Kristo alivyokichwa kwa kanisa mume ni kichwa kwa mkewe.
 
MSISITIZO UPO MSTARI WA 7-9
Marko 10

2 Baadhi ya Mafarisayo wakamjia wakitaka kumtega, wakamwul iza, “Ni halali mtu kumwacha mke wake?”

3 Yesu akawajibu, “Musa aliwaamuruje?”
4 Wakamjibu, “Musa aliruhusu kwamba mume anaweza kumwandikia mkewe hati ya talaka na kumwacha.”

5 Yesu akawaambia, “Musa aliwaandikia sheria hiyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu.
6 Lakini tangu mwanzo wa uumbaji, ‘Mungu aliwaumba mume na mke.
7 Na kwa sababu hii mume atamwacha baba yake na mama yake na hao wawili, watakuwa mwili mmoja.’
8 Kwa hiyo hawatakuwa wawili tena bali mwili mmoja.
9 Basi, alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.”
Hakika ndugu yangu.
 
kuna wanawake wakikosea mapishi tuu tyr talaka tatu zipo mlangoni
 
Back
Top Bottom