Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
Ndoa huwa siyo mashindano kati ya mke na mume. Mashindano na mabishano ndani ya ndoa yamekuwa yakiwagharimu wanandoa wengi sana. Kwa sababu tu ya kukosa uwezo wa mtu mmoja mmoja ndani ya ndoa wa kujiongoza.
Wapendwa wanandoa, kama mkitaka muishi kwenye ndoa yenu kwa furaha na amani, kwa kupendana, kwa ushuhuda na kuwa kielelezo kwenye jamii yenu. Mnatakiwa kwa kukusudia mioyoni kila mmoja ajichunguze na kuchukua hatua ya kukuza uwezo wake wa kujiongoza, yaani kujizuia.
Uwezo wa kujiongoza ni ile hali ya kutawala hisia zako, kutawala mawazo yako, kutawala tabia zako, kutawala maneno yako, kutawala matendo yako, kutawala ulimbukeni (arrogance) yako, kutawala kiburi chako nk.
Mtu anayejitawala huwa siyo mbishi, siyo mwenye hasira, siyo mjuaji, siyo mwenye mashindano, siyo mbabe, siyo mpenda makuu, huwa ni mnyenyekevu, mwenye kuwatanguliza wengine kabla yake, kamwe huwa hatafuti mambo yake binafsi bali hufanya kwa ajili ya wote nk.
Mtu unapokuwa kwenye ndoa unatakiwa kutambua kuwa ni makampuni mawili tofati kabisa, yameletwa pamoja yakaunda kampuni moja ya pekee sana.
Lakini makampuni hayo mawili huingia kwenye ushirika wenza (partnership) huo, kila kampuni huwa na matarajio yake kwenye huo ushirika, misimamo yake, mila na desturi zake, inaamini mambo gani, na kuna mambo iliyoaminishwa huko itokako juu ya ushirika wenza huo.
Lazima tukubaliane ukweli huu, kuwa mwanaume na mwanamke waliumbwa tofauti. Na tofauti zao huja kukuzwa sana na mila na desturi za kule alikokulia, yaani malezi kutoka kwa wazazi na jamii iliyomzunguka wakati wa makuzi yake.
Kwa hiyo, kama huna uwezo wa kujisimamia, uwezo wa kujiambia wewe mwenyewe kuwa hili hapana na hili ndiyo. Uwezo wa kujiambia hapa kweli nimemkosea mke au mume wangu ngoja niombe msamaha. Uwezo wa kujiambia hapa ngoja ninyamaze. Uwezo wa kujiongoza mwenyewe kabla ya kutaka kuwaongoza wengine nk. Ndoa lazima itakutoa jasho tu.
Kuza uwezo wako wa kujiongoza na kujisimamia, ndipo utaifurahia ndoa yako.
Kuza misuli ya kujizuia kufoka au kukasirika au kununa hata kama ni kweli umekosewa.
Kuza uwezo wako wa kutojihesabia haki kupita kiasi. Hata kama amekosea, msamehe hata kabla hajakuomba msamaha.